Wanafunzi watatu UDOM wafariki katika ajali ya gari

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,308
5,458
1654496957002.png

Wanafunzi watatu wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) wamefariki Dunia na wengine watano wamejeruhiwa katika ajali ya gari iliyotokea Juni 4, 2022 jioni katika moja ya barabara zilizopo chuoni hapo.

Ofisa Uhusiano wa chuo hicho, Beatrice Baltazar amesema ajali hiyo imetokea jana Juni 4, 2022 saa 2.00 usiku.

Amewataja waliofariki kuwa ni Hana Meshack, Zira Mpenda na Mpeli Mahenge.

Amewataja waliojeruhiwa kuwa ni Fortunata Kingazi, Fibi Julius, Sifa Shora, Enica William na mwingine aliyetajwa kwa jina moja la Furahina.

Amesema majeruhi wa ajali hiyo wamelazwa katika Hospitali ya Benjamin Mkapa na hali zao zinaendelea vizuri.

Taarifa zinasema wanafunzi hao walikuwa wanatoka katika mahafali ya dini yaliyokuwa yakifanyika chuoni hapo.

Baada ya kuulizwa kuhusu tuko hilo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Martin Otieno amesema: "Ni kweli hiz?o taarifa ni za ukweli, ninaandaa taarifa nitaitoa baadaye kidogo."
 
Wapumzike kwa Amani Marehemu wote,Na Mwenyezi Mungu awape Nafuu Majeruhi.
 
Toa taarifa Kwa usahihi kama huna fatilia ndo utoe,,ni hivi wanabodi,,Jana tarehe 4 june,jumamosi wanafunzi walikuwa wanatoka kwenye graduation ya dini CASFETA,walikuwa wamepanda bajaji kutoka Dodoma mjini kwenda udom "COED" bajaji ilikuwa imewabeba watu jumla 8,kama mnavyojua wanachuo hua wanabebana,nyuma wanaingia 5 mbele 2, na dreva 1,jumla 8,walipofika karibu na mwisho wa lami kama unaelekea block T, gari linalosemekana V8,(Sina uhakika kwenye gari)ndo likawangonga uso Kwa uso ,mida ya saa Moja hv,wakafariki wanachuo 3,na dreva mmoja , waliofariki wote ni 3rd yr,,RIP
-Gari iliyogonga ni RAV4 na ilikua inaendeshwa meja
 
Mkuu poleni sana
 
Back
Top Bottom