Watatu wafariki dunia wakiwemo wanafunzi wawili kwa ajali, Morogoro

Watatu wafariki dunia wakiwemo wanafunzi wawili kwa ajali, Morogoro

Richer

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2025
Posts
2,282
Reaction score
3,962
Watu watatu wamefariki dunia wakiwemo wanafunzi wawili wa kidato cha nne, kufuatia ajali ya barabarani iliyohusisha pikipiki yenye namba za usajili MC 534 DYX iliyokuwa ikiendeshwa na Baraka Sajio(22) iliyokuwa ikitoka Kihonda kuelekea Morogoro mjini, kugongana na lori lenye namba za usajili T 310 DQC lililokuwa linaendeshwa na Omary Juma(45) ambalo lilikuwa likitokea Dar es Salaam kwenda Dodoma, katika eneo la Bima, Kata ya Mafisa, mkoani Morogoro, barabara kuu ya Morogoro–Dodoma

Ajali hiyo imetokea leo Julai 18, 2025 majira ya asubuhi na kusababisha vifo vya watu watatu ambao ni Lusajo Mwang’onda(18) mwanafunzi wa kidato cha nne Morogoro Sekondari mkazi wa Kihonda Mkomola, Ghalib Omary(18) mwanafunzi wa kidato cha nne Morogoro Sekondari mkazi wa Kihonda Maghorofani na Baraka Sajio(22) dereva bodaboda mkazi wa Kihonda Maghorofani

Kwa mujibu wa taarifa rasmi iliyotolewa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Morogoro, uchunguzi wa tukio hilo bado unaendelea huku chanzo cha ajali hiyo kikitajwa kuwa ni uzembe wa dereva wa bodaboda aliyekuwa akijaribu kuyapita magari mengine bila kuchukua tahadhari

Jeshi la Polisi Mkoa wa Morogoro limewataka madereva wote kuzingatia sheria na kanuni za usalama barabarani, likitoa onyo kali kwa madereva wote wanaoendesha kwa uzembe kwamba hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yao

1752844304567.png



1752844193672.png


​
Chanzo: Manara Tv
 
Inna lillahi wainna ilayhi rajiuun

Morogoro kwa ajali napo
Ajali ya kuchomoa betri ile ndo iloliza wengi moro
 
Hizi pikipiki kuziendesha ni Bora uwe mpole barabarani, lami isikutie kichaa. Ikiwa mbele Kuna Lori na una pikipiki usijifanye James bond maana Yale ni maigizo.
 
Back
Top Bottom