Wanafunzi waliojiunga kidato cha kwanza katika shule za kata za Halmashauri ya Wilaya ya Uyui wanakaa chini (sakafuni), Wadau wa elimu mko wapi?

THE BREED

JF-Expert Member
Oct 29, 2019
1,195
2,000
Wanabodi za asubuhi

Nimepitapita kwenye shule za sekondari za Halmashauri ya wilaya ya Uyui Mkoani Tabora na kushudia Wanafunzi wa kidato cha kwanza wanakaa chini sakafuni hali inayotia simanzi sana kwa vijana hawa wadogo wanaoanza safari ya masomo!

Utafiti wangu nimeufanya kwa shule zifuatazo;
Tura Sekondari, Goweko, Igagula, Loya, Kizengi, Imalampaka, Kigwa, Mabama, Madaha na Shule nyingine za Uyui.

Natoa wito kwa Wadau wa Elimu Waziri wa Elimu,TAMISEMI, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Uyui, Maafisa Elimu Msingi na Sekondari wachukue hatua stahiki kuondoa janga hili.

Pia kwa Shule za Msingi za Wilaya hii Hakuna Madawati ya kutosha kwa Darasa la kwanza wanaojiunga sasa hivi.

Fanyeni hima hali inatisha sana!!!
Kama hamtaamini taarifa hii tumeni watu makini mje muone hali ilivyo mbaya.
 

THE BREED

JF-Expert Member
Oct 29, 2019
1,195
2,000
Ujinga kabisa, mimi nimemtengenezea mwanangu kiti na meza, anakaaa vizuri huku wengine wakikaa chini, hii elimu bure ni janga, hali ipo hivyo Tanzania nzima.

Sent using Jamii Forums mobile app
Waliuahidi elim bure!sasa wanawatesa watoto hadi wanachukia ufaulu wao!!pesa nyingi wameelekeza kwenye miradi isiyokamilika leo wala kesho!!!
 

Lerionka ole saidimu

JF-Expert Member
Nov 12, 2019
208
250
Kila Jambo linalopangwa halifanikiwi chini ya hii serikali ya awamu ya unyanyasaji

Uongozi ni hekima na busara tulionao hawana hata maarifa wanaongoza kwa sifa

Hii Hali ikiendelea Raisi ajaye anakazi kubwa sana
 

THE BREED

JF-Expert Member
Oct 29, 2019
1,195
2,000
Siyo Uyui tu, hata Dar es salaam watoto wanakaa chini.
Elimu ni bure lakini miundombinu mibovu, hakuna madawati, vyumba havitoshi, hakuna vyoo wala maji.


Sent using Jamii Forums mobile app
Siyo Uyui tu, hata Dar es salaam watoto wanakaa chini.
Elimu ni bure lakini miundombinu mibovu, hakuna madawati, vyumba havitoshi, hakuna vyoo wala maji.


Sent using Jamii Forums mobile app
Kama wameshindwa wawaambie wazazi watengeneze viti na meza kuliko kuwadhalilisha watoto wa watu!!!
 
Top Bottom