Wanafunzi waliojiunga kidato cha kwanza katika shule za kata za Halmashauri ya Wilaya ya Uyui wanakaa chini (sakafuni), Wadau wa elimu mko wapi?

NAMBA MOJA AJAYE NCHINI

JF-Expert Member
Oct 29, 2019
8,225
16,650
Wanabodi za asubuhi

Nimepitapita kwenye shule za sekondari za Halmashauri ya wilaya ya Uyui Mkoani Tabora na kushudia Wanafunzi wa kidato cha kwanza wanakaa chini sakafuni hali inayotia simanzi sana kwa vijana hawa wadogo wanaoanza safari ya masomo!

Utafiti wangu nimeufanya kwa shule zifuatazo;
Tura Sekondari, Goweko, Igagula, Loya, Kizengi, Imalampaka, Kigwa, Mabama, Madaha na Shule nyingine za Uyui.

Natoa wito kwa Wadau wa Elimu Waziri wa Elimu,TAMISEMI, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Uyui, Maafisa Elimu Msingi na Sekondari wachukue hatua stahiki kuondoa janga hili.

Pia kwa Shule za Msingi za Wilaya hii Hakuna Madawati ya kutosha kwa Darasa la kwanza wanaojiunga sasa hivi.

Fanyeni hima hali inatisha sana!!!
Kama hamtaamini taarifa hii tumeni watu makini mje muone hali ilivyo mbaya.
 
Kila Jambo linalopangwa halifanikiwi chini ya hii serikali ya awamu ya unyanyasaji

Uongozi ni hekima na busara tulionao hawana hata maarifa wanaongoza kwa sifa

Hii Hali ikiendelea Raisi ajaye anakazi kubwa sana
 
Siyo Uyui tu, hata Dar es salaam watoto wanakaa chini.
Elimu ni bure lakini miundombinu mibovu, hakuna madawati, vyumba havitoshi, hakuna vyoo wala maji.


Sent using Jamii Forums mobile app
Siyo Uyui tu, hata Dar es salaam watoto wanakaa chini.
Elimu ni bure lakini miundombinu mibovu, hakuna madawati, vyumba havitoshi, hakuna vyoo wala maji.


Sent using Jamii Forums mobile app
Kama wameshindwa wawaambie wazazi watengeneze viti na meza kuliko kuwadhalilisha watoto wa watu!!!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom