SoC02 Wanafunzi wa mchepuo wa sanaa (Arts) kidato cha tatu na nne wapunguziwe idadi ya mada (topics) katika masomo kama "Biology" na Hisabati (Mathematics)

Stories of Change - 2022 Competition

Infantry Soldier

JF-Expert Member
Feb 18, 2012
15,893
16,317
Habari za wakati huu ndugu zangu wa jamiiforums. Mimi Infantry Soldier nipo mzima wa afya.

UTANGULIZI: MUUNDO WA MFUMO WA ELIMU NCHINI TANZANIA KWA UFUPI.

Mfumo wa elimu wa kitaifa kwa hapa Tanzania una ngazi kuu nne. Kwanza miaka saba ya elimu ya msingi ya lazima (kuanzia umri wa miaka sita), pili ni miaka minne katika ngazi ya sekondari, tatu ni miaka miwili ya elimu ya "A Level" na nne ni miaka mitatu mpaka mitano ya elimu ya juu kulingana na taaluma inayosomewa.

images (1).jpeg

(Picha kwa hisani ya tovuti ya Wizara Ya Elimu)

Kuanzia mwaka huu wa 2022, Serikali imeanza kutoa elimu bure kwa ngazi ya msingi na sekondari kwa wanafunzi wote nchi nzima.

Kuingia katika shule ya sekondari kunategemea na mwanafunzi kupata Cheti cha Elimu ya Msingi cha Tanzania kwa kufaulu mtihani wa kitaifa. Kwa sababu ya matatizo ya kiuchumi yanayoendelea hapa nchini kwa sasa wanafunzi wengi hawajaweza kuendelea na elimu zaidi ya ngazi ya msingi.

images (4).jpeg

(Picha kwa hisani ya tovuti ya Wilaya Ya Kilosa)

Elimu ya sekondari bila malipo ilianzishwa ili kusaidia kushughulikia suala hili. Kwa sasa kiwango cha kujua kusoma na kuandika cha Tanzania, ni cha juu kwa nchi za Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara.

PENDEKEZO LANGU JUU YA KUPUNGUZWA KWA IDADI YA MADA (TOPICS)

Ndugu zangu Watanzania, ninapendekeza wanafunzi wa mchepuo wa sanaa (Arts) kidato cha tatu na nne wapunguziwe idadi ya mada (topics) katika masomo kama "Biology" na Hisabati (Mathematics) yasiyowasaidia kuunda "combination" kidato cha tano.

images (5).jpeg

(Picha kwa hisani ya mtandao wa kituo cha habari cha East African Television)

Mwanafunzi wa mchepuo wa sanaa akipunguziwa mzigo wa topics/mada katika masomo tajwa hapo juu, inampa fursa kubwa sana ya yeye kuelekeza nguvu zake nyingi katika masomo kama Historia, Kiswahili, Geography pamoja na English ambayo ana nafasi kubwa ya kuyatumia katika kuunda "combinations" kama HKL (History, Kiswahili, Language), HGL (History, Geography, Language), HGK (History, Geography, Kiswahili) pamoja na HGE (History, Geography, Economics) pindi afikapo kidato cha tano.

Mwanafunzi wa mchepuo wa sanaa unamfundisha mada za Hisabati kama "Circles and Spheres" pamoja na "Trigonometric Ratios" ili zije zimsaidie wapi na katika nini siku za usoni? Wanasheria maarufu walioko hapa Tanzania kama mzee Mabere Marando au Nimrod Mkono, mada ya somo la biology ya kidato cha tatu kama "Classification of living things" imemsaidia vipi katika kufikia malengo yake ya kitaaluma kwa kiwango cha juu?

mwalimu akiwa darasani.jpg

(Picha kwa hisani ya mtandao)

Ndugu zangu watanzania, sasa umefika wakati wa kufanya mabadiliko ya jumla na makubwa sana katika mitaala pamoja na mifumo yetu ya elimu kama kweli tunataka kuwa na Tanzania imara kwa ajili ya kizazi cha sasa na baadae. Viongozi wetu ni lazima watambue ya kwamba Tanzania ya sasa si sawa na ile ya miaka 20 nyuma.

Tanzania ya mwaka 2002 ambayo mimi Infantry nilihitimu kidato cha nne sio sawa na hii ya mwaka 2022 aliyohitimu mtoto wa dada yangu na wala haitakuwa kama ile ya mwaka 2052 atakapokuwa anahitimu mjukuu wake. Katu hazitakaa zifanane. Jamani tunahitaji kubadilika. "We, seriously, need to change."

Moja kati ya hotuba zake, Rais mstaafu wa Marekani ndugu Barack Hussein Obama aliwahi kusema kwa lugha ya Kiingereza, "as time changes, and so must we" akiwa na maana kwamba, "kadri muda unavyobadilika, ni lazima na sisi tubadilike"

61e798e9d64d3677774663.jpg

(Picha kwa hisani ya tovuti ya Wilaya Ya Kilosa)

Jenga picha mwaka jana ulikuwa una watoto wawili wa kike nyumbani kwako ambao walikuwa wakisoma shule mbili tofauti. Mmoja ni mtoto wa dada yako anayeitwa Zakia na mwingine binti yako wa kuzaa anayejulikana kwa jina la Irene. Katika matokeo ya kidato cha nne ya mwaka jana wa 2021, Zakia, aliyekuwa akisoma mchepuo wa sanaa alifanikiwa kufaulu masomo ya Biology na Hisabati kwa Alama "A" yote mawili, na kisha kupata alama "B" kwa yale mengine saba (7).

Binti yako Irene ambaye alikuwa anachukua mchepuo wa sayansi, alifanikiwa kupata alama hizo hizo akiwa katika shule tofauti za ndugu yake Zakia.

Unafikiri ni nani atakuwa na nafasi kubwa zaidi ya kutumia ufaulu wa alama "A" mbili katika masomo ya Biology na Hisabati katika kuunda combination kidato cha tano? Kiuhalisia ni Zakia ndiye atakayetumia Bilogy na Hisabati katika kuunda combinations kama PCB (Physics, Chemistry, Biology), PCM (Physics, Chemistry, Mathematics), PGM (Physics, Geography, Mathematics), CBA (Chemistry, Biology, Agriculture), pamoja na CBN (Chemistry, Biology, Nutrition).

bukimaf1.jpg

(Picha kwa hisani ya mtandao)

Ninajua fika ya kwamba kuna baadhi ya wadau muda sio mrefu watakuja na hoja zao mufilisi na kuanza kuuliza, kwanini kwa masomo ya Biology na Hisabati pekee na sio somo la civics ambalo nalo pia halisaidii katika kuunda combination kidato cha tano?

Kitu ambacho ninapenda kuwakumbusha wadau hao (kama watajitokeza) ni kwamba somo la civics kwa sasa halisaidii katika kuunda combinations kwa wanafunzi wa O Level kwa michepuo yote hata kama akipata alama "A".

Pendekezo la kuunganisha somo la Civics na Historia kuwa moja huu ni mjadala wa siku nyingine utakaohitaji muda na umakini sana katika kuudadavua. Kwa leo ninapenda kuishi hapa. Asanteni sana kwa kusoma.

AMBATANISHO: Mada za Masomo husika kwa kidato cha tatu na nne.

Mada za somo la Hisabati kidato cha tatu

TOPIC 1: Relations
TOPIC 2: Functions
TOPIC 3: Statistics
TOPIC 4: Rates And Variations
TOPIC 5: Sequence And Series
TOPIC 6: Circles
TOPIC 7: The Earth As A Sphere
TOPIC 8: Accounts

Mada za somo la Biology kidato cha tatu.

TOPIC 1: Classification Of Living Things
TOPIC 2: Movement
TOPIC 3: Coordination
TOPIC 4: Excretion
TOPIC 5: Regulation
TOPIC 6: Reproduction

Mada za somo la Hisabati kidato cha nne.

TOPIC 1: COORDINATE GEOMETRY
TOPIC 2: AREA AND PERIMETER
TOPIC 3: THREE DIMENSIONAL FIGURES
TOPIC 4: PROBABILITY
TOPIC 5: TRIGONOMETRY
TOPIC 6: VECTORS
TOPIC 7: MATRICES AND TRANSFORMATION
TOPIC 8: LINEAR PROGRAMMING

Mada za somo la Biology kidato cha nne.

TOPIC 1:GROWTH
TOPIC 2: GENETICS
TOPIC 3: CLASSIFICATION OF LIVING THINGS
TOPIC 4: EVOLUTION
TOPIC 5: HUMAN IMMUNO DEFICIENCY (HIV) ACQUIRED IMMUNO DEFICIENCY SYNDROME (AIDS), AND SEXUAL TRANSMITTED INFECTIONS (STI’s)

OUR MOTTO: ENDELEA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USICHAFUE TASWIRA NJEMA YA TAIFA LAKO. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.
 
Asante sana Askari wa nchi kavu. Mada nzuri na nimeshakupigia kura.

Hata hivyo nina angalizo kidogo.

Kuna sababu wanafunzi wote wanalazimishwa kusoma masomo haya.

1. Hesabu ni somo la muhimu sana na kuna uwezekano mkubwa kuwa huko mbele ya safari watakutana nalo kwa namna moja au nyingine. Kuna wengine watasoma HGE au EGM kidato cha 6. Bila msingi mzuri wa hesabu wanaweza wakatetereka. Hata kwenye Isimu kuna Mathematical na Computational Linguistics. Bila msingi mzuri wa hesabu ni majanga. Kwa maoni yangu somo la Hisabati halikwepeki!

2. Biology ni somo linalohusu viumbe na maingiliano yao na mazingira. Ni somo la muhimu linalomfanya binadamu ajitambue yeye mwenyewe alivyo pamoja na mahusiano yake na viumbe hai wengine na mazingira yao.

Hata hivyo mada yako inachokonoa swali la msingi zaidi na la muhimu pengine kuliko yote. Lengo hasa la hii elimu yetu ni nini? Ni ajira kwa waipatayo? Ni kuwatajirisha? Ni kuwakaramsha waipatayo na kuwafanya kuwa na uelewa wa kiwango fulani wa jinsi mifumo inayoendesha maisha yao inavyofanya kazi kimwingiliano katika mazingira waliyomo?

Ati; lengo hasa la hii elimu yetu ni nini?

Kila la heri katika shindano hili mkuu
 
Habari za wakati huu ndugu zangu wa jamiiforums. Mimi Infantry Soldier nipo mzima wa afya.

Ndugu zangu Watanzania, ninapendekeza wanafunzi wa mchepuo wa sanaa (Arts) kidato cha tatu na nne wapunguziwe idadi ya mada (topics) katika masomo kama "Biology" na Hisabati (Mathematics) yasiyowasaidia kuunda "combination" kidato cha tano.

Mwanafunzi wa mchepuo wa sanaa akipunguziwa mzigo wa topics/mada katika masomo tajwa hapo juu, inampa fursa kubwa sana ya yeye kuelekeza nguvu zake nyingi katika masomo kama Historia, Kiswahili, Geography pamoja na English ambayo ana nafasi kubwa ya kuyatumia katika kuunda "combinations" kama HKL (History, Kiswahili, Language), HGL (History, Geography, Language), HGK (History, Geography, Kiswahili) pamoja na HGE (History, Geography, Economics) pindi afikapo kidato cha tano.

Mwanafunzi wa mchepuo wa sanaa unamfundisha mada za Hisabati kama "Circles and Spheres" pamoja na "Trigonometric Ratios" ili zije zimsaidie wapi na katika nini siku za usoni? Wanasheria maarufu walioko hapa Tanzania kama mzee Mabere Marando au Nimrod Mkono, mada ya somo la biology ya kidato cha tatu kama "Classification of living things" imemsaidia vipi katika kufikia malengo yake ya kitaaluma kwa kiwango cha juu?

View attachment 2308686
(Picha kwa hisani ya mtandao)

Mfumo wa elimu wa kitaifa kwa hapa Tanzania una ngazi kuu nne. Kwanza miaka saba ya elimu ya msingi ya lazima (kuanzia umri wa miaka sita), pili ni miaka minne katika ngazi ya sekondari, tatu ni miaka miwili ya elimu ya "A Level" na nne ni miaka mitatu mpaka mitano ya elimu ya juu kulingana na taaluma inayosomewa. Kuanzia mwaka huu wa 2022, Serikali imeanza kutoa elimu bure kwa ngazi ya msingi na sekondari kwa wanafunzi wote nchi nzima.

Kuingia katika shule ya sekondari kunategemea na mwanafunzi kupata Cheti cha Elimu ya Msingi cha Tanzania kwa kufaulu mtihani wa kitaifa. Kwa sababu ya matatizo ya kiuchumi yanayoendelea hapa nchini kwa sasa wanafunzi wengi hawajaweza kuendelea na elimu zaidi ya ngazi ya msingi. Elimu ya sekondari bila malipo ilianzishwa ili kusaidia kushughulikia suala hili. Kwa sasa kiwango cha kujua kusoma na kuandika cha Tanzania, ni cha juu kwa nchi za Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara.

Ndugu zangu watanzania, sasa umefika wakati wa kufanya mabadiliko ya jumla na makubwa sana katika mitaala pamoja na mifumo yetu ya elimu kama kweli tunataka kuwa na Tanzania imara kwa ajili ya kizazi cha sasa na baadae. Viongozi wetu ni lazima watambue ya kwamba Tanzania ya sasa si sawa na ile ya miaka 20 nyuma.

Tanzania ya mwaka 2002 ambayo mimi Infantry nilihitimu kidato cha nne sio sawa na hii ya mwaka 2022 aliyohitimu mtoto wa dada yangu na wala haitakuwa kama ile ya mwaka 2052 atakapokuwa anahitimu mjukuu wake. Katu hazitakaa zifanane. Jamani tunahitaji kubadilika. "We, seriously, need to change."

Moja kati ya hotuba zake, Rais mstaafu wa Marekani ndugu Barack Hussein Obama aliwahi kusema kwa lugha ya Kiingereza, "as time changes, and so must we" akiwa na maana kwamba, "kadri muda unavyobadilika, ni lazima na sisi tubadilike"

Jenga picha mwaka jana ulikuwa una watoto wawili wa kike nyumbani kwako ambao walikuwa wakisoma shule mbili tofauti. Mmoja ni mtoto wa dada yako anayeitwa Zakia na mwingine binti yako wa kuzaa anayejulikana kwa jina la Irene. Katika matokeo ya kidato cha nne ya mwaka jana wa 2021, Zakia, aliyekuwa akisoma mchepuo wa sanaa alifanikiwa kufaulu masomo ya Biology na Hisabati kwa Alama "A" yote mawili, na kisha kupata alama "B" kwa yale mengine saba (7).

Binti yako Irene ambaye alikuwa anachukua mchepuo wa sayansi, alifanikiwa kupata alama hizo hizo akiwa katika shule tofauti za ndugu yake Zakia.

Unafikiri ni nani atakuwa na nafasi kubwa zaidi ya kutumia ufaulu wa alama "A" mbili katika masomo ya Biology na Hisabati katika kuunda combination kidato cha tano? Kiuhalisia ni Zakia ndiye atakayetumia Bilogy na Hisabati katika kuunda combinations kama PCB (Physics, Chemistry, Biology), PCM (Physics, Chemistry, Mathematics), PGM (Physics, Geography, Mathematics), CBA (Chemistry, Biology, Agriculture), pamoja na CBN (Chemistry, Biology, Nutrition).

View attachment 2308689
(Picha kwa hisani ya mtandao)

Ninajua fika ya kwamba kuna baadhi ya wadau muda sio mrefu watakuja na hoja zao mufilisi na kuanza kuuliza, kwanini kwa masomo ya Biology na Hisabati pekee na sio somo la civics ambalo nalo pia halisaidii katika kuunda combination kidato cha tano?

Kitu ambacho ninapenda kuwakumbusha wadau hao (kama watajitokeza) ni kwamba somo la civics kwa sasa halisaidii katika kuunda combinations kwa wanafunzi wa O Level kwa michepuo yote hata kama akipata alama "A". Pendekezo la kuunganisha somo la Civics na Historia kuwa moja huu ni mjadala wa siku nyingine utakaohitaji muda na umakini sana katika kuudadavua. Kwa leo ninapenda kuishi hapa. Asanteni sana kwa kusoma.

AMBATANISHO: Mada za Masomo husika kwa kidato cha tatu na nne.

Mada za somo la Hisabati kidato cha tatu

TOPIC 1: Relations
TOPIC 2: Functions
TOPIC 3: Statistics
TOPIC 4: Rates And Variations
TOPIC 5: Sequence And Series
TOPIC 6: Circles
TOPIC 7: The Earth As A Sphere
TOPIC 8: Accounts LINEAR PROGRAMMING

Mada za somo la Biology kidato cha tatu.

TOPIC 1: Classification Of Living Things
TOPIC 2: Movement
TOPIC 3: Coordination
TOPIC 4: Excretion
TOPIC 5: Regulation
TOPIC 6: Reproduction

Mada za somo la Hisabati kidato cha nne.

TOPIC 1: COORDINATE GEOMETRY
TOPIC 2: AREA AND PERIMETER
TOPIC 3: THREE DIMENSIONAL FIGURES
TOPIC 4: PROBABILITY
TOPIC 5: TRIGONOMETRY
TOPIC 6: VECTORS
TOPIC 7: MATRICES AND TRANSFORMATION
TOPIC 8: LINEAR PROGRAMMING

Mada za somo la Biology kidato cha nne.

TOPIC 1:GROWTH
TOPIC 2: GENETICS
TOPIC 3: CLASSIFICATION OF LIVING THINGS
TOPIC 4: EVOLUTION
TOPIC 5: HUMAN IMMUNO DEFICIENCY (HIV) ACQUIRED IMMUNO DEFICIENCY SYNDROME (AIDS), AND SEXUAL TRANSMITTED INFECTIONS (STI’s)

OUR MOTTO: ENDELEA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USICHAFUE TASWIRA NJEMA YA TAIFA LAKO. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.
Infantry soldier nakubaliana na wewe 100% kwamba mabadiliko makubwa yanahitajika katika mfumo wetu wa elimu.Swali la msingi ni kwamba ni mabadiliko gani yana-hitajika?

Mimi nilipomaliza Chuo Kikuu kwa mfano, ajira haikuwa issue,ukimaliza Degree yako ya kwanza,unachagua unapo taka kwenda,kwanza waajiri wanakuja vyuoni kujikomba kwenu! Leo hali ni tofauti kabisa.Ajira ni ngumu sana kupata,hasa kama huna connection.Hali hii kwa mtizamo wangu inatutaka nasi mtu mmoja mmoja tubalike kimtazamo,lakini pia hata kama Taifa.

Kwa mtu mmoja mmoja this calls for immediate change, kwa kuwa effect ni immediate.Mimi nashauri hivi,tuachane na dhana na mawazo kwamba kufika Chuo Kikuu na kupata Degree is everything,badala yake tu-opt for alternatives ambazo zitampa mhusika fani.Katika hili kwa hiyo ningeshauri kabla Taifa halija fanya mabadiliko yanayohitaji,ambayo halina budi kuyafanya,sisi kama sisi tu-opt for Vocational Training courses halafu tuende na mkondo huo mpaka mtu anapata Degree yake. On the other hand,kitaifa Vyuo vya VETA viimarishwe zaidi,ili viweze kutoa courses ambazo mtu akitoka huko ataweza aidha kujiajiri au kuajiriwa.Ilivyo sasa hata mtu akitoka VETA bado hajaiva vizuri kuweza kuajirika straight,bado anahitaji on the job training.Hii ni kasoro kubwa.

Hii ina maana gani,ina maana kwamba ipo haja ya kuimarisha na ku-overhaul mfumo wetu mzima wa elimu after STD.VII to University.Mfumo wa STD I-VII ubaki kama ulivyo sasa,ila uwe strengthened zaidi kwa kupata waalimu mahiri
zaidi,vifaa vya kufundishia vizuri zaidi na kuwa wa vitendo zaidi etc.etc..

Natamani mtoto akimaliza Darasa la Saba awe anajua kuzungumza Kingereza,aweze kuchora ramani ya Dunia,in short ajue basics za Geography,Biology,Physics,Chemistry etc na awe na basic skills,kama mimi nilipomaliza STD.VII.,inawezekana,kama iliwezekana wakati wetu.

Ili kuwa-equip watoto na more basic skills, tunaweza kufikiria kurudisha STD VIII, ambayo kwa bahati mbaya tuliifuta badala ya kui-imarisha! Elimu ya sasa actually from Std.I to University ni bora liende,it is simply bullshit.

Baada ya STD VII (or VIII),ushauri wangu ni nini.Mfumo wa VETA uwe adopted kama mfumo formal,na ndio utoe Degrees.Mfumo wa sasa ufutwe,it is out of date and irrelevant.

Masomo gani yafundishwe kwenye hiyo system mpya?Masomo ambayo ni relevant and basic kwa fani husika.Darasa la kwanza mpaka Darasa la Saba iwe Elimu ya Msingi kama ilivyo sasa au la nane,baada ya hapo fani.Fani iwe the main area of emphasis.Wewe kama ni Architecture ukisha maliza Darasa la Saba kama umeonekana unafaa kuwa Architecture,uta-base kwenye masomo yanayohusiana na Architecture tu,na hapa nasisitiza,emphasis iwe kwenye vitendo zaidi,theory iwe na nia ya kumsaidia mwanafunzi kwenye vitendo.

Nimalizie kwa kusema kwamba yapo masomo ambayo ni ya msingi sana katika kumtengeneza mwanafunzi kuwa
raia mwema na pia kumsaidia kwenye mawasiliano,kitaifa na kimataifa,haya ni lazima yafundishwe baada ya Darasa la Saba au la Nane.Masomo haya ni pamoja na Historia,Kiswahili,Kingereza na Civics.Naomba niseme kwamba Historia sio Civics ni vitu tofauti kabisa.Civics ni "the study of the rights and duties of citizenship," wakati History ni "the study of past events, particularly in relation to human affairs."
 
1. Hesabu ni somo la muhimu sana na kuna uwezekano mkubwa kuwa huko mbele ya safari watakutana nalo kwa namna moja au nyingine. Kuna wengine watasoma HGE. Bila msingi mzuri wa hesabu wanaweza wakatetereka. Hata kwenye Isimu kuna Mathematical na Computational Linguistics. Bila msingi mzuri wa hesabu ni majanga. Kwa maoni yangu somo la Hisabati halikwepeki!
Upo sahihi sana mkuu. Hata mimi ninakubaliana na umuhimu wa somo la hesabu katika maisha ya kila siku ya mwanadamu. Mimi nime-suggest topics zipunguzwe na sio somo kupuuzwa kabisa kwa maana mtu mwenye lengo la kuwa engineer sio sawa na yule anayeota kuja kuwa mwanasheria siku moja hivyo hawapaswi kusoma topics za kufanana.
 
2. Biology ni somo linalohusu viumbe na maingiliano yao na mazingira. Ni somo la muhimu linalomfanya binadamu ajitambue yeye mwenyewe alivyo pamoja na mahusiano yake na viumbe hai wengine na mazingira yao.
Mkuu, bila shaka hujanielewa vema katika bandiko langu kuu hapo juu. Mimi siongelea kufutwa moja kwa moja kwa somo la Biology. Lengo la somo la Biology ni kuja kuandaa wanasayansi ndio maana mtu wa HKL hawezi kuwa admitted MUHAS kusomea MD kwa kigezo kuwa hana background ya somo hilo A level.

Hoja kwamba Biology ipo kwa lengo la kumfaanya mwanafunzi ajitambue yeye pamoja na mazingira yake ipo outdated sana katika karne hii ya sayansi na teknolojia. Internet is almost everywhere now. Vijana wana nafasi kubwa ya kupata maarifa yaa utambuzi kupitia mitandao ya kijamii na streaming media kama YouTube and the like.

Mkuu, hii hoja yako ya kutaka vijana wetu wasome topics zoooote kama wale wa mwaka 1999 bado sikubaliani nayo hata kidogo.
 
Hamna logic hapo, wanaosoma sayansi wanasoma masomo 9 ikiwemo masomo ya arts yote, pamoja na hivyo wanafanya vizuri kuliko watu wanaosoma arts.

Fanya research kwenye shule nyingi za sekondari wanafunzi wa sayansi ndio huongoza Hadi kwenye masomo ya arts,

Kama mwanafunzi yupo vizuri yeye mwenyewe ndio ataamua afaulu au asifaulu.

Mfano, classification inamsaidia nini mwanafunzi wa arts??

Hufahamu kwamba Kuna marks za bure za classification kwenye practical??? Hufahamu kwamba biology ni somo rahisi ambalo hata watu wa arts wanafaulu?? Practical peke yake ina marks 50 za bure kabisa.

Kwanini wapunguziwe topics za hesabu, hujui Kuna watu wa arts wengine wanapenda kusoma EGM advance???
 
Infantry soldier nakubaliana na wewe 100% kwamba mabadiliko makubwa yanahitajika katika mfumo wetu wa elimu.Swali la msingi ni kwamba ni mabadiliko gani yana-hitajika?

Mimi nilipomaliza Chuo Kikuu kwa mfano, ajira haikuwa issue,ukimaliza Degree yako ya kwanza,unachagua unapo taka kwenda,kwanza waajiri wanakuja vyuoni kujikomba kwenu! Leo hali ni tofauti kabisa.Ajira ni ngumu sana kupata,hasa kama huna connection.Hali hii kwa mtizamo wangu inatutaka nasi mtu mmoja mmoja tubalike kimtazamo,lakini pia hata kama Taifa.

Kwa mtu mmoja mmoja this calls for immediate change, kwa kuwa effect ni immediate.Mimi nashauri hivi,tuachane na dhana na mawazo kwamba kufika Chuo Kikuu na kupata Degree is everything,badala yake tu-opt for alternatives ambazo zitampa mhusika fani.Katika hili kwa hiyo ningeshauri kabla Taifa halija fanya mabadiliko yanayohitaji,ambayo halina budi kuyafanya,sisi kama sisi tu-opt for Vocational Training courses halafu tuende na mkondo huo mpaka mtu anapata Degree yake. On the other hand,kitaifa Vyuo vya VETA viimarishwe zaidi,ili viweze kutoa courses ambazo mtu akitoka huko ataweza aidha kujiajiri au kuajiriwa.Ilivyo sasa hata mtu akitoka VETA bado hajaiva vizuri kuweza kuajirika straight,bado anahitaji on the job training.Hii ni kasoro kubwa.

Hii ina maana gani,ina maana kwamba ipo haja ya kuimarisha na ku-overhaul mfumo wetu mzima wa elimu after STD.VII to University.Mfumo wa STD I-VII ubaki kama ulivyo sasa,ila uwe strengthened zaidi kwa kupata waalimu mahiri
zaidi,vifaa vya kufundishia vizuri zaidi na kuwa wa vitendo zaidi etc.etc..

Natamani mtoto akimaliza Darasa la Saba awe anajua kuzungumza Kingereza,aweze kuchora ramani ya Dunia,in short ajue basics za Geography,Biology,Physics,Chemistry etc.kama mimi nilipomaliza STD.VII.,inawezekana,kama iliwezekana wakati wetu.

Ili kuwa-equip watoto na more basic knowledge, tunaweza kufikiria kurudisha STD VIII, ambayo kwa bahati mbaya tuliifuta badala ya kui-imarisha! Elimu ya sasa actually from Std.I to University ni bora liende,it is simply bullshit.

Baada ya STD VII (or VIII),ushauri wangu ni nini.Mfumo wa VETA uwe adopted kama mfumo formal,na ndio utoe Degrees.Mfumo wa sasa ufutwe,it is out of date and irrelevant.

Masomo gani yafundishwe kwenye hiyo system mpya?Masomo ambayo ni relevant and basic kwa fani husika.Darasa la kwanza mpaka Darasa la Saba iwe Elimu ya Msingi kama ilivyo sasa au la nane,baada ya hapo fani.Fani iwe the main area of emphasis.Wewe kama ni Architecture ukisha maliza Darasa la Saba kama umeonekana unafaa kuwa Architecture,uta-base kwenye masomo yanayohusiana na Architecture tu,na hapa nasisitiza,emphasis iwe kwenye vitendo zaidi,theory iwe na nia ya kumsaidia mwanafunzi kwenye vitendo.

Nimalizie kwa kusema kwamba yapo masomo ambayo ni ya msingi sana katika kumtengeneza mwanafunzi kuwa
raia mwema na pia kumsaidia kwenye mawasiliano,kitaifa na kimataifa,haya ni lazima yafundishwe baada ya Darasa la Saba au la Nane.Masomo haya ni pamoja na Historia,Kiswahili,Kingereza na Civics.Naomba niseme kwamba Historia sio Civics ni vitu tofauti kabisa.Civics ni "the study of the rights and duties of citizenship," wakati History ni "the study of past events, particularly in relation to human affairs."
Ufafanuzi mzuri sana huu kaka mkubwa. Asante.
 
Back
Top Bottom