Walimu wa sekondari wanatafutwa, wa masomo ya Hisabati na Sayansi Biology, physics na Chemistry (Part time)

FRESHMAN

JF-Expert Member
Sep 29, 2011
8,822
33,527
Habari wadau.

Binafsi ni mmiliki wa app ya kufundisha tution za masomo kwa njia ya mtandao

Ninatafuta walimu wenye uwezo mkubwa wa kuelewa na kufundisha masomo ya o level. Na shule ya msingi somo la hisabati.

Masomo hayo ni hisabati, physics, chemistry na biology only.

Kazi ni part time. Malipo ni makubaliano kutokana na kazi utakayoifanya.

Kazi kubwa ni kutafsiri video content za ufundishaji.

Mfano halisi ni kufanya kama vile azam tv wanavyofanya kwenye tamthilia za ottoman.

Yaani unakuta video ya ufundishaji hesabu topic ya statitics ipo tayari inafundishwa kwa lugha ya kihindi, mwalimu akishirikiana na timu yangu wanapaswa waihamishie ifundishwe kwa kiswahili kwa kutumia content zilezile.

Mfano hapa chini

Hii ni video ya mzungu anafundisha algebra ya form one. Ya one unknown kwa lugha ya kiingereza. Mwalimu naemtafuta atapaswa ajue kufundisha haya haya mafunzo kwa lugha ya kiswahili kwa mifano hiyo hiyo. Ili mwanafunzi asiyejua kiingereza kabisa aelewe vizuri




mfano wa pili hii ni video inayofundisha Biology ya form one kuhusu classification of living things. mwalimu anapaswa aihamishie kuifundisha kwa lugha ya kiswahili ili mwanafunzi wa kayumba ama QT aielewe. sauti ya mwalimu ndio ita replace sauti ya huyo mzungu anayefundisha kwa lugha ya kiingereza


anayehitajika awe mwalimu wa hayo masomo ya sayansi na mathematics.

awe na shahada ya ualimu ama stashahada ya masomo tajwa.

Pia shule za msingi anahitajika mwalimu wa hisabati ama mathematics. Mwenye uzeofu wa kufundisha hesabu za primary

awe na uzoefu wa kufundisha.

gender balance walimu wanahitajika kufanya nao kazi wa kiume na wa kike.

Mwalimu awe anaishi Dar es salaam ama mkoa wa pwani ili iwe rahisi kufanya nae kazi. maana studio za kurekodia ufundishaji wake zipo Dar es salaam.


mfano wa mwisho mzungu anafundisha Archimedes' principle kwa lugha ya kiingereza. mwalimu wangu kazi yake ni kueleza fundisho hilo hilo kwa lugha ya kiswahili. yaani kama AZAM TV ama Star times wanavyofanya kwenye tamthilia wanazoonesha zilizoigizwa na watu wa nchi zingine

kwa wenye sifa zinazotajwa na wapo tayari kwenye hii kazi wanicheki dm ama kwenye namba ya whatsapp 0789 18 70 10
 

Attachments

  • Understanding Archimedes' principle.mp4
    10.6 MB
Back
Top Bottom