Wanafunzi msijichoshe kufaulu sana, ajira haziangalii ufaulu mkubwa

hayo ni maneno ya kuwafariji watu wenye uwezo mdogo darasani au waliofeli makusudi kwa kutokuweka efforts darasani..

top layer wa darasa nilizopita 90% sio failures na kuna baadhi walipata kazi kupitia graduates trainee programs za multinational companies ambazo zilidemand G.P.A kuanzia 4.0

Hivyo msiwafanye watu wawe comfortable na G.P.A za 2 point something maana wanakuwa tayari below the job industry demand kiasi cha kuona vyeti vyao ni useless baadae
 
Acheni kujustify low performance wazee...Kama mtu anaweza kusoma akapata alama za juu afanye hivyo,hayo ya ajira ni majaaliwa tu.Kuna wenye low grades za darasani wengi sana wako mtaani kutokana na grades zao maana pia kuna ajira nyingi tu zinatolewa kwa kigezo cha grade za ufaulu so wewe kupata ajira kwa ufaulu wa chini sio kuwa ndio standard ya maisha.Always be the best on what you do.

Ukipata G.P.A ya kawaida na ukawa na uwezo wa kuonesha upo vizuri kupitia experience, confidence na skills ulizonazo. Unaweza kuwa na nafasi nzuri zaidi kuliko aliepata 4.5 na akashindwa kuimiliki hiyo G.P.A kwenye interview process. Ni kawaida lakini mtu awe na G.P.A nzuri na bado akawa vizuri kwenye demonstration, sidhani kama atashindwa kirahisi
 
Acheni kujustify low performance wazee...Kama mtu anaweza kusoma akapata alama za juu afanye hivyo,hayo ya ajira ni majaaliwa tu.Kuna wenye low grades za darasani wengi sana wako mtaani kutokana na grades zao maana pia kuna ajira nyingi tu zinatolewa kwa kigezo cha grade za ufaulu so wewe kupata ajira kwa ufaulu wa chini sio kuwa ndio standard ya maisha.Always be the best on what you do.
Ajira za ufaulu wa juu labda u lecturer
 
hayo ni maneno ya kuwafariji watu wenye uwezo mdogo darasani au waliofeli makusudi kwa kutokuweka efforts darasani..

top layer wa darasa nilizopita 90% sio failures na kuna baadhi walipata kazi kupitia graduates trainee programs za multinational companies ambazo zilidemand G.P.A kuanzia 4.0

Hivyo msiwafanye watu wawe comfortable na G.P.A za 2 point something maana wanakuwa tayari below the job industry demand kiasi cha kuona vyeti vyao ni useless baadae

Mm nina wanngu tulipiga nao Shule wana GPA za Nusu Mlingoti wameajiriwa Tasac na wakati wale makonki wenye 4 point wapo wanasugua gaga.

Ajira zinahitaji watu wenye vyeti na sio ufauru mkubwa wala mdogo. as long as una cheti unakula ajira safi kabisa
 
Nimecheka leo nilipokuwa maeneo ya mjini huko, nilisikia vijana wakilalamika kuwa; wanajuta kufaulu kwa kiwango cha juu kwani hakuna maana yoyote na haisaidii popote pale.

Nina kiji-internet Cafe changu hapa mjini, sasa baada ya kusikia tangazo la ajira za waalimu na afya, nikasema acha nisimamie shoo mwenyewe kupiga pesa za wasaka ajira. Ofisi yangu ilianza kufurika jana saa tisa na mpaka saa nne usiku nilikuwa nao waomba ajira.

Sasa kinachonifanya niandike hapa, ni mwalimu mmoja mwenye umri wa miaka 29, aliyemaliza mwaka 2015 chuo cha DUCE.
Maneno yake yalinifanya nicheke lakini yalinitafakarisha sana.

Vyeti vyake vya O Level ana divisheni one ya 16 masomo tisa. A'Level ana divisheni one ya 9 Combination ni PCM. Transcript yake niliona anaka-GPA ka 3.8 kutoka pale mlimani/Duce Ambapo GPA hiyo sio haba kwa kweli hasa kwa masomo ya Physics na Mathematics.

Yule kijana alisema akiwaambia wenzake aliokuja naye, baada ya kusifiwa kwa ufaulu huo ambao kimsingi ni mkubwa, yule kijana akasema;

"Kinachoniumiza ni kuwa nilijitesa bure ili nipate ufaulu mkubwa kwa lengo nikimaliza shule na chuo nisipate shida kupata ajira. Ninachoshangaa ni kuwa wenzangu wenye ufaulu mdogo wao ndio wanaajiriwa, mimi niliyekaza na kukesha usiku na kufaulu mpaka sasa nasota. Huu mwaka unaenda wa sita naomba ajira serikalini nakosa"

Maelezo hayo yalinichekesha kwani ni kweli kabisa, na yalinigusa hata mimi kwani mimi nilifaulu kwa madaraja ya mwisho kabisa.
O'Level nilipata divisheni three ya 24, A'Level nikapata divisheni three ya 15, Chuo kikuu nikapata GPA ya 2.6:D:D:D:D:D:D:D:DIngawaje sijasoma ualimu wala udaktari, lakini nilipata kazi mapema sana, miaka ya 2011 licha ya kuwa fani niliyosomea ajira zake ni ngumu kupatikana na wasomi ni wengi. Nilipata kazi nikiwaacha solembe wenye shule na misonge yao:D:D:D:D:D:D

Kufaulu sana sio kupewa kazi, acheni kujichosha vijana walioko chuoni au wanafunzi mlioko shuleni.

Muhimu elimu ikae kichwani zaidi.

Poleni sana mliojifanya chuoni hamli bata kisa kitabu

Povu Ruksa
Yupo mmoja pale afrikana,anauza tu korosho kwenye magari,
 
Mm nina wanngu tulipiga nao Shule wana GPA za Nusu Mlingoti wameajiriwa Tasac na wakati wale makonki wenye 4 point wapo wanasugua gaga.

Ajira zinahitaji watu wenye vyeti na sio ufauru mkubwa wala mdogo. as long as una cheti unakula ajira safi kabisa

Ni kweli mkuu maana kuna kazi nyingi tu zinatoka na kipengele cha G.P.A Hakipo na watu wanaweza kuomba cheti siku ya kuwasili kazini baada ya kupass usahili

ila kwa multinationals na kampuni zilizo strict kwenye qualifications za wafanyakazi wao. Sahau hata kuwa shortlisted kwa ajili ya interview kwa G.P.A ya 2 point something
 
Iyo nadharia inaukweli kiasi, maana hata hapa mm ninapo ishi kuna kijana ni 4m4 failure yaaan div zeroo aka re seat akala four ..akaanza zile foundation course, akaja cheti, dip mpaka degree na gpa yake nahisi itakuwa 2.9 lkn as we speak now jamaa ni mhasibu ktk mamlaka moja ya umma. 😀😀
 
Aombe kurudi chuo huyo akafundishe, ila usiwakatishe tamaa wale wanaotaka na wenye uwezo kufaulu maana inawasaidia pale wanapotaka ufadhiri wa kimasomo nje ya mipaka yetu,
Binafsi kidato cha 4 ni div I.15, kidato cha 6 ni III. 13 chuo G.P.A 3.1 nilibahatika kupata kazi mapema ila mda mwingine natamani nipate ufadhiri nikasome nje ila ndo hivyo GPA kikwazo
 
Acheni kujustify low performance wazee...Kama mtu anaweza kusoma akapata alama za juu afanye hivyo,hayo ya ajira ni majaaliwa tu.Kuna wenye low grades za darasani wengi sana wako mtaani kutokana na grades zao maana pia kuna ajira nyingi tu zinatolewa kwa kigezo cha grade za ufaulu so wewe kupata ajira kwa ufaulu wa chini sio kuwa ndio standard ya maisha.Always be the best on what you do.
Tanzania GPA kubwa hazipatini kwa kukesha Library kubukua.

Ukikariri notes za Lecturer, ukakwepa figisu zote za CATs, Quizzes, Assignments umemaliza.

Private Unis wanafumua maGPAs makubwa siyo kwamba wanasoma sana au wako very skillful.
 
Aombe kurudi chuo huyo akafundishe, ila usiwakatishe tamaa wale wanaotaka na wenye uwezo kufaulu maana inawasaidia pale wanapotaka ufadhiri wa kimasomo nje ya mipaka yetu,
Binafsi kidato cha 4 ni div I.15, kidato cha 6 ni III. 13 chuo G.P.A 3.1 nilibahatika kupata kazi mapema ila mda mwingine natamani nipate ufadhiri nikasome nje ila ndo hivyo GPA kikwazo
Mkuu kusoma nje wanataka GPA kuanzia ngap kwan
 
Na mm nichangie kidogo hapa kufaulu vizur ni jambo jema sanaaaaa .......ndio kwenye ajira inaweza ikawa sio issue maana nazo zina connection nyingi mnooo.

Ilaa napenda kuwaambia tu ukiwez kupata alama nzuri pata bila hivyo scholarship utazisikia tu mda mwingine zinataka ufaulu wa juu
 
Nimecheka leo nilipokuwa maeneo ya mjini huko, nilisikia vijana wakilalamika kuwa; wanajuta kufaulu kwa kiwango cha juu kwani hakuna maana yoyote na haisaidii popote pale.

Nina kiji-internet Cafe changu hapa mjini, sasa baada ya kusikia tangazo la ajira za waalimu na afya, nikasema acha nisimamie shoo mwenyewe kupiga pesa za wasaka ajira. Ofisi yangu ilianza kufurika jana saa tisa na mpaka saa nne usiku nilikuwa nao waomba ajira.

Sasa kinachonifanya niandike hapa, ni mwalimu mmoja mwenye umri wa miaka 29, aliyemaliza mwaka 2015 chuo cha DUCE.
Maneno yake yalinifanya nicheke lakini yalinitafakarisha sana.

Vyeti vyake vya O Level ana divisheni one ya 16 masomo tisa. A'Level ana divisheni one ya 9 Combination ni PCM. Transcript yake niliona anaka-GPA ka 3.8 kutoka pale mlimani/Duce Ambapo GPA hiyo sio haba kwa kweli hasa kwa masomo ya Physics na Mathematics.

Yule kijana alisema akiwaambia wenzake aliokuja naye, baada ya kusifiwa kwa ufaulu huo ambao kimsingi ni mkubwa, yule kijana akasema;

"Kinachoniumiza ni kuwa nilijitesa bure ili nipate ufaulu mkubwa kwa lengo nikimaliza shule na chuo nisipate shida kupata ajira. Ninachoshangaa ni kuwa wenzangu wenye ufaulu mdogo wao ndio wanaajiriwa, mimi niliyekaza na kukesha usiku na kufaulu mpaka sasa nasota. Huu mwaka unaenda wa sita naomba ajira serikalini nakosa"

Maelezo hayo yalinichekesha kwani ni kweli kabisa, na yalinigusa hata mimi kwani mimi nilifaulu kwa madaraja ya mwisho kabisa.
O'Level nilipata divisheni three ya 24, A'Level nikapata divisheni three ya 15, Chuo kikuu nikapata GPA ya 2.6:D:D:D:D:D:D:D:DIngawaje sijasoma ualimu wala udaktari, lakini nilipata kazi mapema sana, miaka ya 2011 licha ya kuwa fani niliyosomea ajira zake ni ngumu kupatikana na wasomi ni wengi. Nilipata kazi nikiwaacha solembe wenye shule na misonge yao:D:D:D:D:D:D

Kufaulu sana sio kupewa kazi, acheni kujichosha vijana walioko chuoni au wanafunzi mlioko shuleni.

Muhimu elimu ikae kichwani zaidi.

Poleni sana mliojifanya chuoni hamli bata kisa kitabu

Povu Ruksa
Uliwezaje kudahiliwa ukiwa na 3 ya point 15, kifupi ni D na E???
 
Ndugu yangu alipata GPA ya 4.7 UDSM akapata scholarship kwenda Canada, masters. Akawa anapewa pesa ya kujikimu kwa mwezi 3000USD kwa mwaka 36000USD.

Naomba nijumlishie mshahara wako kwa mwezi ni shilingi ngapi Mkuu. Alafu gawanya kwa hizo hela hapo.
 
Kuna jamaa nilimaliza nalo form four 2008 likapata div.four 30, likawa halina hata D 4 za kusoma certificate kozi yoyote. Baada ya hapo likaanza kurudia mitihani mara 2 ndo likafikisha D4 likaanza kusoma certificate CBE likaunga Diploma hadi degree. Kabla halijamaliza degree mwaka wa tatu likaomba kazi kwa kutumia cheti cha diploma. Likapata. Sasa hivi taasisi ya serikali yenye pesa. Lina safiri na ndege lina cheo kikubwa. Ndo maana natamani nijilipue.
 
Back
Top Bottom