Jokajeusi
JF-Expert Member
- Jun 1, 2018
- 6,305
- 10,564
Nimecheka leo nilipokuwa maeneo ya mjini huko, nilisikia vijana wakilalamika kuwa; wanajuta kufaulu kwa kiwango cha juu kwani hakuna maana yoyote na haisaidii popote pale.
Nina kiji-internet Cafe changu hapa mjini, sasa baada ya kusikia tangazo la ajira za waalimu na afya, nikasema acha nisimamie shoo mwenyewe kupiga pesa za wasaka ajira. Ofisi yangu ilianza kufurika jana saa tisa na mpaka saa nne usiku nilikuwa nao waomba ajira.
Sasa kinachonifanya niandike hapa, ni mwalimu mmoja mwenye umri wa miaka 29, aliyemaliza mwaka 2015 chuo cha DUCE.
Maneno yake yalinifanya nicheke lakini yalinitafakarisha sana.
Vyeti vyake vya O Level ana divisheni one ya 16 masomo tisa. A'Level ana divisheni one ya 9 Combination ni PCM. Transcript yake niliona anaka-GPA ka 3.8 kutoka pale mlimani/Duce Ambapo GPA hiyo sio haba kwa kweli hasa kwa masomo ya Physics na Mathematics.
Yule kijana alisema akiwaambia wenzake aliokuja naye, baada ya kusifiwa kwa ufaulu huo ambao kimsingi ni mkubwa, yule kijana akasema;
"Kinachoniumiza ni kuwa nilijitesa bure ili nipate ufaulu mkubwa kwa lengo nikimaliza shule na chuo nisipate shida kupata ajira. Ninachoshangaa ni kuwa wenzangu wenye ufaulu mdogo wao ndio wanaajiriwa, mimi niliyekaza na kukesha usiku na kufaulu mpaka sasa nasota. Huu mwaka unaenda wa sita naomba ajira serikalini nakosa"
Maelezo hayo yalinichekesha kwani ni kweli kabisa, na yalinigusa hata mimi kwani mimi nilifaulu kwa madaraja ya mwisho kabisa.
O'Level nilipata divisheni three ya 24, A'Level nikapata divisheni three ya 15, Chuo kikuu nikapata GPA ya 2.6Ingawaje sijasoma ualimu wala udaktari, lakini nilipata kazi mapema sana, miaka ya 2011 licha ya kuwa fani niliyosomea ajira zake ni ngumu kupatikana na wasomi ni wengi. Nilipata kazi nikiwaacha solembe wenye shule na misonge yao
Kufaulu sana sio kupewa kazi, acheni kujichosha vijana walioko chuoni au wanafunzi mlioko shuleni.
Muhimu elimu ikae kichwani zaidi.
Poleni sana mliojifanya chuoni hamli bata kisa kitabu
Povu Ruksa