Ufaulu kidato cha nne ni upeo mkubwa wa kuelewa wa wanafunzi au uchakachuaji wa mitihani ili kupaisha ufaulu?

Mzee wa Twitter

JF-Expert Member
Nov 5, 2023
1,272
2,037
Wadau nawasabahi.

Kutokana na ufaulu mkubwa wa wanafunzi wa kidato na cha 6 kupanda sana kuanzia awamu ya 4 mpaka hii ya 6 nimekuwa najiuliza kuna nini kinachosababisha ufaulu kuwa mkubwa ili hali wanafunzi hao hao wakifika vyuoni wanafeli vibaya mfano Law School na Muhimbili?

Je, huu ufaulu ni wanafunzi kuwa na upeo mkubwa wa akili au ni uchakachuaji wa mitihani unaofanywa na necta ili kupaaisha ufaulu wa wanafunzi na kuwafurahisha wazazi?
 
Mfumo wa mitihani ya kikoloni na kizazi cha sasa wanajua sana ndio maana wanafaulu..

Materials kupata rahisi sehemu kibao ..Niliona ticha ameweka projector wanafunzi wanaangalia practical live bila ta chenga ,tena video anayefundsiha ni mzungu .

Mitihani hata ya zamani tuwe wakweli kwa kizazi hiki wanaipiga fresh tu 🤣 One za kutosha.
 
Mitihani ya siku hizi ni ujinga mtupu, tangu lini kukawa na mitihani ya "ku-bet"?
Ndio maana Wakifika LAW SCHOOL au Chuo cha Madaktari Muhimbili Wanafeli vibaya
Nakumbuka wakati wa Utawala Awamu ya 4 wanafunzi walifeli saba Mzee PINDA akaaguza kurekebisha Viwango vya ufaulu kuanzia hapo ni mwendo wa KUFAULU Serikali inaandaa Taifa la Kubet Mitihani

Sent from my SM-A145R using JamiiForums mobile app
 
kuna ile ya mfumo wa alama kubadilishwa, alama A kuanzia 75 wakati ilikua inaanzia 81, sina uhakika lakini

halafu sidhani kama zamani mitihani ilikua ina 'format' sina uhakika wajuzi wanirekebishe

mimi nimefanya NECTA ya 2020, nakumbuka tulipewa format za mitihani yote, zinatolewa na TIE sijui NECTA, yaani inajulikana swali namba flani litatokea mada fulani, inarahisisha mambo

kwahiyo msidhani watoto wanasoma mtaala, wanakariri 'format'
 
Mfumo wa mitihani ya kikoloni na kizazi cha sasa wanajua sana ndio maana wanafaulu..

Materials kupata rahisi sehemu kibao ..Niliona ticha ameweka projector wanafunzi wanaangalia practical live bila ta chenga ,tena video anayefundsiha ni mzungu .

Mitihani hata ya zamani tuwe wakweli kwa kizazi hiki wanaipiga fresh tu 🤣 One za kutosha.
Lakini mbona haiakisi maarifa na utambuzi wanachokijua huku mitaani.
Utamkuta mtoto form 4 anayo 1-7, form six anayo 1-3 ila ukimuuliza kuwa waziri mkuu na spika wa bunge kwa Tanzania wanapatikanaje ...anabaki amekodoa macho.
Ukimuiza Wilaya ya Chunya ipo Mkoa gani anabaki ameshangaa.
Ukimuuliza ni mazingira gani yanasababisha Rais kukoma kuwa Rais hapa Tanzania ...hajui.
Ukimuuliza akutajie haki zake angalau tano, wapi.
Hayo maswali ya biolojia na kemia alizopata A baada ya miezi 6 hawezi tena kuyajibu.
Kuna shida sehemu.
 
Ndio maana Wakifika LAW SCHOOL au Chuo cha Madaktari Muhimbili Wanafeli vibaya
Nakumbuka wakati wa Utawala Awamu ya 4 wanafunzi walifeli saba Mzee PINDA akaaguza kurekebisha Viwango vya ufaulu kuanzia hapo ni mwendo wa KUFAULU Serikali inaandaa Taifa la Kubet Mitihani

Sent from my SM-A145R using JamiiForums mobile app
Pale Law ni habari nyingine 😅
 
kuna ile ya mfumo wa alama kubadilishwa, alama A kuanzia 75 wakati ilikua inaanzia 81, sina uhakika lakini

halafu sidhani kama zamani mitihani ilikua ina 'format' sina uhakika wajuzi wanirekebishe

mimi nimefanya NECTA ya 2020, nakumbuka tulipewa format za mitihani yote, zinatolewa na TIE sijui NECTA, yaani inajulikana swali namba flani litatokea mada fulani, inarahisisha mambo

kwahiyo msidhani watoto wanasoma mtaala, wanakariri 'format'
Du Hadi format wanapewa,hapo kazi
 
Nenda huko vyuoni ndipo utaona madudu aisee. First year hajui tofautisha former letter na non-formal letter.

Ukiwapa computer hakuna wanachojua anatype kama ile keyboard inawaka moto.
Et keyboard inawaka moto😀😀😀
 
Division 1.7 imekuwa kama maandazi vile...

Inapatikana kimdebwedo kabisa kama njugu vile....
Screenshot_20240125-183502_1.jpg
View attachment 2882606

Sent from my Infinix X657B using JamiiForums mobile app
 
kuna ile ya mfumo wa alama kubadilishwa, alama A kuanzia 75 wakati ilikua inaanzia 81, sina uhakika lakini

halafu sidhani kama zamani mitihani ilikua ina 'format' sina uhakika wajuzi wanirekebishe

mimi nimefanya NECTA ya 2020, nakumbuka tulipewa format za mitihani yote, zinatolewa na TIE sijui NECTA, yaani inajulikana swali namba flani litatokea mada fulani, inarahisisha mambo

kwahiyo msidhani watoto wanasoma mtaala, wanakariri 'format'
Format sio shida maana ukicheki format ya kila somo unakuta imecover topics zote, unaweza taja somo flani topic ipi haipo kwenye format? Nb: masomo ya sayansi na hesabu
 
Tusidanganyane, serikali inaharibu hawa vijana haya matokeo ni tofauti kabisa na uelewa wa walio wengi. Mimi mwenyewe kijana wangu amepata division one ya point 10 lakini nikiri ni wazi hakustahili kuwa na kiwango hicho cha ufaulu hasa kwa kuwa ninaufahamu vizuri uwezo wake. Kuna shida mahali sio bure. Serikali iache siasa kwenye swala la elimu.
 
Back
Top Bottom