Wanadiplomasia wetu waliopo Zambia na DRC Congo kwanini wanashindwa kumwambia Rais ukweli? Watanzania wanateseka kwenye hizi nchi hakuna wakuwatetea

Resilience

JF-Expert Member
Jan 4, 2023
877
4,106
Tanzania nadhani tunashindwa kuelewa kwamba nchi yetu ili iendelee lazima wafu wetu wasafiri nje . Tunashindwa kuelewa ili nchi iweze kupunguza changamoto za ajira lazima watu wake wakatafute fursa Sehemu nyingine

Tumekuwa wepesi sana kutetea wageni badala ya kutetea watu wetu. Raia wa Kongo DRC wanaingia Tanzania bila visa ila watanzania wananyanyasika huko Kongo kwa kulazimishwa walipe visa. Hakuna Sehemu yoyote utasikia mwanasiasa wa Tanzania au mwanadiplomasia akikemea au kuwasemea Watanzania. Watu wetu wanateseka utadhani kusafiri nje kwetu ni kosa kisheria.

Watanzania wanateseka sana Zambia hasa Kusaka na Kitwe, hakuna balozi wala kiongozi anayesimama kuwatetea. Wanatozwa hadi dola 500 wakiwa Zambia sisi huku tunasema waingie wakae siku 180. Tunatengeneza ushirikiano wa aina gani? Leo tulitegemea kusikia Zambia wanatoa neno kuhusu uhuru wa Watanzania kwenda Zambia lakini hakuna msamaha wa masharti uliotolewa badala yake sisi tumekwenda kuwaongezea muda wakukaa Tanzania bila kutoka. Tunakwenda wapi?

Hatuwezi kupromote uchumi na biashara kwa kukwepa principle ya reciprocity; lazima diplomasia makini ijenge msingi wake kwenye reciprocity in most of issues. Wewe ukiwa na diplomasia ya upande mmoja it can't work . Tunachowafanyia Raia wetu dhidi ya mataifa jirani siyo sawa. Kwamba Kenya tupate shida, Uganda shida, Zambia kelele, Mozambique ndo useme huku mataifa hayo yote yakiingia Tanzania bila masharti yoyote....it's not fair at all

Mnao wajibu wakuwatetea watanzania wasinyanyaswe nje, mnaowajibu wakiwasaidia Watanzania kulinda mitaji yao nje, na mnao 2ajibu wakumlinda mtanzania awe mzuri au Mbaya.....Ulinzi wa Mtanzania nje ndiyo misingi ya uwepo wa diplomasia ya Kimataifa.

Leo Raia wa Kongo akipata changamoto Tanzania viongozi wote wataingilia kati, same applies to other countries......sisi kwanini tunajidharau?
 
Back
Top Bottom