Wana CCM naomba mhalalishe picha hizi

Ama kweli hatujui tunachofanya. We take for granted some facts about the way Tanzania is for sometime now and forget the very same fact that times change.
 
Mnyika ni kweli mnaonekana mpo serious na huenda siku moja mkafanikiwa/tukafanikiwa, maana ukweli unabaki wazi kwamba mna mikakati mingi lakini haitekelezeki kwa haraka na kuleta tija inayoonekana mara moja.
Badala ya kulalamikia CCM, tunataka tuwapime na nyie na hizo operesheni. Tungependa tufaham katika uchaguzi wa 2010 malengo ni majimbo mangapi? Tunataka kufaham tunakwenda nyuma au mbele? Maana wakati fulani mnaonekana kama asasi za kiraia, TAMWA nk. Au kwenu nyie kipimo ni nini? Serikali tunaipima kwa sera na hali halisi ya maisha, nyie hamna standard ambazo zinapimwa na watu nje?
Pia wakati fulani huwa najiuliza mkienda mkalundikana katika eneo fulani sustainability yake ikoje? Naamini mkiondoka katika eneo husika na uhai wa chama ubaki muda mfupi na kutoweka kabisa. Wajengee uwezo viongozi wa maeneo husika hao ndiyo wanajua wananchi wao na ndio wapo karibu zao. Msiwaze kuwaza na nchi nzima haraka, hakikisheni kwenye nguvu km Karatu huko CCM hawafukuruti then mnaongeza wigo na maeneo mengine. Soon or later tutawajoin baada ya majukum haya mengine
 
Mimi nadhani kwa muda uliobaki mambo sijui ya sera, strategic plans blah blah yamepitwa na wakati. Issue iliyobaki ni kuangalia namna serikali inavyotumia pesa za walipa kodi kwenye mambo ambayo hayana maana na kuacha mambo yenye faida kwa wananchi kama elimu, afya, kilimo, miundombinu kuzorota.

Issue ni hii tu, Picha za magari ya thamani kubwa vs shule mbovu, picha za viongozi wakimbembea ulaya vs hospitali mbovu, picha za viongozi wakitumbua hela kempinski kwenye semina vs wananchi vijijini wakilima kwa jembe nk ndio issue ambayo itakuwa rahisi kueleweka.

Tukishindwa na hili then tunadeserve yote tutakayofanyiwa na Jk na kundi lake 2010-2015 maana I can predict disaster. Kama Mkapa alibadilika vile kipindi cha mwisho huyu mkware si ndio itakuwa kilio??

Mungu Ibariki Tanzania.
 
dr slaa
je kwanini nyinyi na cuf msikae mkafikiria kuungana jamani.
Hichi ni kilio kikubwa sana cha wananchi.
Freeman hataki kugombea urais, mumsimamishe lipumba na nyinyi wengine msukume chama mbele na muongeze idadi ya wabunge
naunga mkono alicho sema, mwenzetu hapo juu, Chadema washirikiane na CUF, na kumuunga Mkono Lipumba kwenye Uraisi , na sehemu za Wabunge wapime ni mwanachama gani anaye faa wa Chadema/CUF, ingawa ningependekeza Wapitishwe wabunge wengi wa Chadema ilikuwepo na uwiano katika kuongoza Nchi, simple as that.
 
The Boss,

Umejitahidi sana kutetea maneno yako. Binafsi ninaamini sasa kuwa Tanzania ina sura mbili kama zilivyo picha hizo hapo juu. Sehemu kubwa ya watanzania wanaishi kwenye Tanzania inayowakilishwa na picha ya pili, lakini wewe kulingana na maneno yako, utakuwa unatoka ile Tanzania inayowakilishwa na hilo jumba la gavana; so you are right.


Kama akina mama hao walifanya makosa kubeba mimba wakati hawana uwezo wa kwenda hospitali za kulipia, je watoto hawa walifanya makosa gani?








​
 

Mmmh, humo simo! CHADEMA na CUF wapi na wapi? Bora hata ungesema na NCCR-mageuzi. Na kwanini CHADEMA imuunge mkono Lipumba na si Lipumba amuunge mkono Mbowe au huyo mgombea ambaye CHADEMA wanamuandaa? By the way, ninaweza nikashangaa sana iwapo Lipumba atagombea tena urais na mwaka huu. Maana tushamzoea na tumeshamchoka. Kwani CUF ni mali yake binafsi hadi aendelee kugombea yeye tu kila siku? Hamuoni mfano mzuri wa Mbowe, kagombea mwaka jana, sasa hivi anasema anakwenda kugombea ubunge. Huyo Lipumba tangu 1995 anagombea urais hapati na wala haachi. haoni kama ana kasoro? Lipumba na Seif lao moja tu. Tena nina wasiwasi wakiingia madarakani watabadilisha katiba ili watawale milele.
Tunataka chama kitakachobadilisha huu ufujaji mbaya wa pesa unaoendelea hivi sasa. Tunataka chama kitakachojali zaidi maisha ya watu,kitakachowatoa akina mama na akina baba kwenye mateso ya huduma mbovu za afya na elimu mbovu kama iliyopo sasa. Sasa mtu anayetafuta madaraka hakomi akipewa atawakumbuka wananchi kweli huyo? Simqualify kabisa Lipumba kwa nafasi hiyo awaachie wengine sasa.
 
Kubwajinga; Huwa nikisema tunahitaji mapinduzi si mnauliza ni mapinduzi gani?Na kwamba ninayoongea ni maneno mabaya na yenye kuchochea vurugu na uvunjifu wa amani?Haya sasa....
 

The Boss inawezekana ni mfurukutwa tu,ama inawezekana ni JK mwenyewe,you never know behind haya majina vivuli.
So therefore hoja zinawatosha only wasitumie lugha chafu....Tukisema "Huu ni wazimu" na wakati ukweli wazimu huo ndio unaotuongoza na kutuamulia watanzania itakuwa sawa na ile kauli maarufu ya "Utopian"
Ukweli ni kwamba nchi inaendeshwa "Kiwazimu wazimu" Na kama kweli hatutaki kuthink in that utopian ways and manners,basi ni lazima tupambane na wazimu huo mumo kwa mumo.
 
Mh Dr. Slaa,

Vipi suala la kuwa na Redio yenu......je hamuonikuw aredio itakuw ani njia moja muhimu sana kuafikishia wananchi ujumbe........pamoja na hilo hongereni sana na juhudi zenu za " Op....Sangara"


Ni kweli, badala ya kununua Helikopta, ni afadhali mnegununua Redio au TV station yenye nguzu za kurusha matangazo nchi nzima.
 

Naku-support mkuu 100%, ni kweli kabisa, na nafikiri ukiacha ufisadi janga lingine linalopaswa kutibiwa haraka iwezekanavyo ni huko kuzaliana hovyo wakati uwezo wa kutunza haupo, sioni hatari tukichukuwa hatua kama china, tuweke limit ya idadi ya watoto (siyo lazima iwe mmoja kama china) ili wale wachache watakao zaliwa waweze kukua kwenye mazingira bora.
 
Kama serikali ya CCM haikufanya lolote kwa miaka kuhusu ufisadi wa benki kuu hadi kelele zilipozidi, mnafikiri watakuwa na sababu ya kufuatilia tujisenti twa bilioni 2? Kama Kikwete hakushtushwa na "vijisenti" vya Chenge na kumuacha aendelee kuwa Waziri mnafikiri atashtushwa na hili?

change is necessary; change is inevitable.
 
Kama Kikwete hakushtushwa na "vijisenti" vya Chenge na kumuacha aendelee kuwa Waziri mnafikiri atashtushwa na hili?

Kikwete anajitahidi sana asiwe raisi bora. Inakuwa vigumu kuelewa wakati unapokabiliana na tatizo ambalo ufumbuzi/suluhisho lake linakuangalia usoni, lakini kwa makusudi kabisa hutekelezi suluhisho hilo. Ni sawa na kupasiwa mpira kwenye lango la adui, na kipa akiwa ameshatoka nje, lakini kwa mshangao wa wengi, kwa makusudi badala ya kufunga goli unarudisha mpira kati au kuutoa nje.
Maajabu.
 
hapa tatizo sio ccm!.............
 
Kwa kuanza, tatizo ni viongozi. What is CCM? Huwezi ku-point kitu fulani ukasema hii ni CCM. Naamini katiba ya CCM hairuhusu uzembe, kutokuwajibika n.k. Lakini viongozi wakuu wa CCM wanapotenda kinyume na katiba yao, sasa nani wa kuwakemea? Inabaki kulindana tu. Lakini uzembe na kutowajibika kunapokithiri, tatizo sasa linakuwa ni CCM vile vile kwani mwenendo huo unakuwa katiba yake (isiyo rasmi) bali inayotekelezwa.
 

Man you seem not to have reached academic maturity, I would say go back to school
 
Kuna Binti wa Kitanzania, USA. Huwa anatoa bure Vitanda kwa Hospitali mbalimbali za Bongo. Kule Singida ametoa Vitanda Vizuri sana sijui kama hawezi kusaidia Hospitali ya (Mkoa) Temeke, Dar es Salaam. Ambayo Mnyange Naomi Campbell alitembelea?
 
Kuna Binti wa Kitanzania, USA. Huwa anatoa bure Vitanda kwa Hospitali mbalimbali za Bongo. Kule Singida ametoa Vitanda Vizuri sana sijui kama hawezi kusaidia Hospitali ya (Mkoa) Temeke, Dar es Salaam. Ambayo Mnyange Naomi Campbell alitembelea?

tatizo siyo vitanda hata mimi naweza kusaidia vitanda!
 

The boss nafikiri unafika mbali, wewe unaishi tanzania au nchi gani? unadiriki kusema mambo kama haya?

kwangu mimi hayana mantiki yoyote, you need to be great thinker..!!!
i doubt kama ulishalazwa hata siku moja hospitali ya serikali au ndugu yako wa karibu alijifungua katika moja ya hostpital hizi.

Hata wewe ni tatizo.

We have a long way to go.......
 

Kwa mwendo huu hata hao 'sisiemu' wenyewe watakukana!
 
tatizo siyo vitanda hata mimi naweza kusaidia vitanda!
Mzee, Nimefungua Vitabu kidogo, nimegundua tatizo ni mfumo mbovu wa Afya, tena kuna Tafiti imefanywa na Marehemu Dr. Nassor Hamudu na Wenzake ina mapendekezo mazuri sana mojawapo ni?
Jiji la Dar es Salaam , linahitaji Hospitali tatu kama Muhimbili na Hospitali ndogo kumi, kama Mwananyamala, Temeke, Amana. na Vituo vya Afya kama Sinza na Mnazi Mmoja Thelathini. Ili kuweka uwiana wa Vitanda na Wagonjwa kwa Idadi ya Watu, Maradhi ya Mfumuko etc.
Ikumbukwa Muhimbili, Amana, Temeke na Mwananyamala zilijengwa Jiji la Dar es salaam likiwa na Watu laki Nane na Nusu sio Milioni Nne au Tano wa sasa hivi.
Bila Mfumo thabiti, Mipango na Vipaumbele vya Uhakika, Wakinamama na Wagonjwa Wengine Wataendelea Kulala Chini.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…