KaziIendelee
JF-Expert Member
- Oct 30, 2013
- 327
- 231
JK JK JK hufai wala hukufaa kuwa kiongozi mkubwa katika taifa hili
hizo akili na busara atavitoa wapi?Amani haiwezi kulindwa kwa kuwachonganisha watu. italindwa na sheria. Haiwezekani Kiongozi mzima tena raisi ulopoke na watu wakuache unaendekeza ujinga. Nivizuri atumie akili na busara.
Naunga mkono kauli ya JK, ccm kama ilivyo kwa raia wengine wana haki ya kujilinda. Ningeshangaa kama JK angesema ccm wawe wanyonge. Kazi ya kujilinda sio jukumu la polisi ambao ni wachache kukidhi mahitaji, ni kazi ya kila chama na kundi la watu wenye nia moja njema. Kwanza JK kachelewa kutoa hii kauli kiasi cha watu kupoteza maisha kwa unyonge. Baba aliniambia usichokoze ila ukichokozwa na mchokozaji akadhamilia kukujeruhi, usiwe mnyonge. Pigana naye then baba yake na mimi tutakaa kuongea nakumaliza.
Hongera JK, tuko nyuma yako.
viva rais wetu...
viva mwenyekiti wetu....
tunaukataa unyonge kwa nguvu zetu zote... kwa mioyo yetu yote na kwa akili zetu zote...
binadamu ana kikomo cha uvumilivu na hatuwezi vumilia madhila makubwa namna hii yawapate wenzetu
nilimwambia Baba V kuwa safari hii KALENGA ccm hatutakuwa wanyonge....
me nadhani safari za mara kwa mara zimemchosha akili. uwezo wa kufikiri unapungua sana.
Ameidhinisha piga nikupige jino kwa jino
Bila kufuata tatatibu za kisheria
Anaungana sasa na waziri mkuu aliyesema "utapigwa tu"
Ni kiashirio kwamba uchaguzi ujao kutakuwa na vipigo kwa sababu kibali kuacha unyonge kimetolewa rasmi.
Jensene, kwahiyo unachosema mwenyeketi wa chama alitakiwa aseme kwamba wana chama wake wawe wanyonge wanapochokozwa au kutolewa macho, ati kwasababu yeye ni rais? Yeye ni mwenyekiti kwanza kabla ya urais na a lion gear kwenye mkutano wa chama chake. Akina Lipumba walipokua wanasema watakuwa ngangari au Slaa aliposema nchi haitatawalika mbona walieleweka bila chenga? Ukweli hauchagui wala kuchaguliwa msemaji.Nafikiri mgojwa ukimwi midadi ya uchama ndiyo inakuongoza. Fikiria kila chama, makundi ya kikabila, dini na wengine wakihamasisha waondoe unyonge na kukubiliana na wengine. Nchi hii itakwenda wapi? Fikiri kwa makini huyu ni rais wa watanzania wote. Cio CCM tu.
Sikuwa karibu na Runinga, ila nilipofika nyumbani binti yangu akanieleza hakumuelewa Kikwete na kauli yake. Nikamuuliza kauli gani? Akaniambia amewambia ccm waache unyonge! wasitishwe na wapinzani, wagombee nafasi yoyote wanayotaka'.
Hii nchi JK haiachi salama, take my word! Nilishasema sisem wako tayari kua ilimradi wasalie madarakani. Hii haikubaliki. CDM nendeni jimbo la kalenga bila uoga. Wambie tume ya uchaguzi kuboresha daftari. Wambie polisi wasithubutu kulinda waiba kura, wasithubutu kuingilia kampeni za uchaguzi huo. Waandaeni green guard kulinda kura za wapiga kura. Nchi hii yetu sote....hakuna mwenye hati miliki ya uongozi. Ni box la kura linalohamua nani awe nani. si polisi, si jk, si mahakama. Ccm acheni haki ndiye awe mtawala.
sijaielewa hii kauli ya kikwete alikuwa anamaanisha nini.
ameyasema hayo wakati wa kikao cha NEC alipokuwa anazungumzia machafuko yanayotokea kwenye chaguzi ndogo especially ile ya kahama.
amewataka wana CCM kuacha unyonge. hapa nimeshindwa kumuelewa; anataka wana CCM wareact vipi? kwa kuua au?
na amejihami kwa kusema kwamba hata kama alichokisema kitakuwa ndio habari nzito kwenye vyombo ya habari sawa tu.
source: news, TBC1