Wana CCM acheni unyonge - Kikwete

Wana CCM acheni unyonge - Kikwete

Mbona hukusema haya wakati wana CCM wamechomewa nyumba, wamekatwa mikono na kutolewa macho huko kahama?

Mbona hukuwashitaki Mbowe na Slaa wanaotembea kwa chopper kushinikiza ngumi na mapanga kila siku?

Mchochezi ni nani? Umemwelewa JK we Kubenea au ni muendelezo wa majungu yako ya kukosa kuteuliwa nae tangu 2005?

JK hakumaanisha mapanga wala ngumi, na kama unapenda haki dhidi ya wachochezi basi faili la kwanza Mahakamani washitakiwe Mbowe na Slaa pamoja na wabunge wao kwa uchochezi na utekelezaji wa mauaji.

Nenda Bugando Mwanza ukawaone majeruhi ndo uje uandike makala yenye haki.

Kubenea unajiaabisha.
Hata wao chadema watakushangaa kama unasimama kuwatetea.

Ushahidi wa mwanzo ni namna wananchi walivyoamua kuwakataa kupitia kura na kuambulia kata 3, je unadhani hiyo ni kawaida?

Kubenea vua miwani ya ushabiki uitendee haki kalamu yako.
 
nyie mlitaka jeeeeeeeeeeeeeeeeeee, meza wembe km unahasira
 
Kwani wapinzani huwa wanawafanyia nini CCM hadi waonekane wanyonge? Kwa nini watu mstuke hivyo baada ya kauli hiyo?
Labda alimaanisha wasiwe wanyonge kwa kuona wenzao wanaruka na chopa hivyo na wao wajibu mapigo kwa kutafuta chopa?
 
Kila siku watu wapinzani wanalia kuwa ccm ndo chanzo cha uvunjifu wa amani kina maboya humu wanapinga Jk kalopoka sasa kama kawaida yake mngojeeni Rweyemamu
 
Mungu akunyime yote lakni sio busara(wisdom) akikunyima hiyo kitu unaweza kuwa kama MTOTO mdogo
 
Siyo siri
Katika miaka ya hivi karibuni CCM imekuwa weak kutokana na kukosekana itikadi na taratibu zinazojenga mshikamano ndani ya chama.

Lakini matokeo ya uchaguzi hayaonyeshivyo, labda tofauti ya takwimu ya idadi za kura.
 
Na Said Kubenea

JAKAYA Mrisho Kikwete, mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) taifa, anapaswa kushitakiwa kwa uchochezi.

Akifungua mkutano wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya chama chake mjini Dodoma leo, Kikwete alichochea wanachama wa CCM kuwapiga wapinzani kwa kudai kuwa, “Uvumilivu una kikomo.”

Amewataka wana CCM kuacha unyonge kwa madai kwamba wapinzani wamekuwa wakiwapiga huku wao wakisubiri polisi kuchukua hatua za kisheria.

Hii ina maana kwamba, Kikwete ambaye ni Rais wa Jamhuri ya Muungano, amewataka wanachama wa CCM, kuchukua sheria mkononi. Ametaka wananchi kuumizana, kupingana na kuuana. Huu ni uchochezi unaoweza kuingiza nchi katika machafuko ya kisiasa, kidini na kijamii.

Kama Kikwete alitaka urais, bila shaka alijipima na kujiona anaweza kufanya kazi hiyo. Kama alikuwa anajua anakwenda Ikulu kujaribu, basi alikuwa amekosea. Ikulu siyo sehemu ya kujaribu.

Kauli ya Kikwete ya kutaka wananchi wajibu mapigo, ni ishara kwamba ameomba kazi ambayo haiwezi.

Rais wa nchi hawezi kuchochea raia wake kupigana. Anapaswa kutumia vyombo alivyonavyo kusimamia sheria.

Ni lazima akumbushwe kwamba nchi hii ikiingia katika machafuko au mauaji ya halaiki, yeye ndiye atakuwa wa kwanza kuulizwa. Anaweza asiulizwe na vyombo vya sheria vya hapa, lakini ataulizwa na vyombo vingine vya dunia.

Alicho sema sawa tu.
Kama vyama vingine vina fanya uhuni na ugaidi ili kuwatusha watu wasipige kura njia nzuri ni kujibu mapigo kwa kuwalinda wakapige kura.
Wakizongea vituo vya kuisabia kura nao ccm wazongee
Fujo za uchaguzi za wengine jawabu ni jino kwa jino
 
sijaielewa hii kauli ya kikwete alikuwa anamaanisha nini.
ameyasema hayo wakati wa kikao cha NEC alipokuwa anazungumzia machafuko yanayotokea kwenye chaguzi ndogo especially ile ya kahama.
amewataka wana CCM kuacha unyonge. hapa nimeshindwa kumuelewa; anataka wana CCM wareact vipi? kwa kuua au?
na amejihami kwa kusema kwamba hata kama alichokisema kitakuwa ndio habari nzito kwenye vyombo ya habari sawa tu.

source: news, TBC1

Jino kwa jino
Fujo za kuwatisha watu wasipige kura
Kuvamia na kuviweka chini ya ulinzi vituo vya kupiga kura
Hayo ndio anawambia wasikubali
Kama hamtaki fujo acheni uhuni huo
Ushindi wa chadema umekuwa influenced na fujo huku ccm ikiangalia tu.
Sasa unyonge huo bas
 
Mbona hukusema haya wakati wana CCM wamechomewa nyumba, wamekatwa mikono na kutolewa macho huko kahama?

Mbona hukuwashitaki Mbowe na Slaa wanaotembea kwa chopper kushinikiza ngumi na mapanga kila siku?

Mchochezi ni nani? Umemwelewa JK we Kubenea au ni muendelezo wa majungu yako ya kukosa kuteuliwa nae tangu 2005?

JK hakumaanisha mapanga wala ngumi, na kama unapenda haki dhidi ya wachochezi basi faili la kwanza Mahakamani washitakiwe Mbowe na Slaa pamoja na wabunge wao kwa uchochezi na utekelezaji wa mauaji.

Nenda Bugando Mwanza ukawaone majeruhi ndo uje uandike makala yenye haki.

Kubenea unajiaabisha.
Hata wao chadema watakushangaa kama unasimama kuwatetea.

Ushahidi wa mwanzo ni namna wananchi walivyoamua kuwakataa kupitia kura na kuambulia kata 3, je unadhani hiyo ni kawaida?

Kubenea vua miwani ya ushabiki uitendee haki kalamu yako.

Mbona unaongea hovyo? Aibu hiyo. Sasa kuna kata CDM imepoteza? Ama kweli magamba mmetingwa kisaikolijia,mwisho wenu tayari.
 
Acha uchochezi we Kubenea. Unadhalilisha taaluma ya uandishi wa habari maana siku zote habari zako zimejaa majungu tupu. Umeshindwa kuuona uchochezi unaofanywa na akina Slaa, Mbowe na Msigwa kwenye majukwaa kila siku, umeiona kauli ya Kikwete tu. Laanakum sheitwan mk...ubwa wee!
 
ahadi ya kupewa ubunge wa viti maalum na chadema imemtia uchizi huyu kubenea,hajui kwamba viti maalum vimefutwa? mbowe na slaa wamemdanganya, huyu kubenea toka amwagiwe tindikali akili zake haziko sawa, kiufupi tu, ni kwamba KUBENEA KAWA CHIZI...
 
Mbona hukusema haya wakati wana CCM wamechomewa nyumba, wamekatwa mikono na kutolewa macho huko kahama?

Mbona hukuwashitaki Mbowe na Slaa wanaotembea kwa chopper kushinikiza ngumi na mapanga kila siku?

Mchochezi ni nani? Umemwelewa JK we Kubenea au ni muendelezo wa majungu yako ya kukosa kuteuliwa nae tangu 2005?

JK hakumaanisha mapanga wala ngumi, na kama unapenda haki dhidi ya wachochezi basi faili la kwanza Mahakamani washitakiwe Mbowe na Slaa pamoja na wabunge wao kwa uchochezi na utekelezaji wa mauaji.

Nenda Bugando Mwanza ukawaone majeruhi ndo uje uandike makala yenye haki.

Kubenea unajiaabisha.
Hata wao chadema watakushangaa kama unasimama kuwatetea.

Ushahidi wa mwanzo ni namna wananchi walivyoamua kuwakataa kupitia kura na kuambulia kata 3, je unadhani hiyo ni kawaida?

Kubenea vua miwani ya ushabiki uitendee haki kalamu yako.

Hapa hatushindani kuorodhesha maovu wanayofanyiwa wafuasi wa vyama, kikubwa hapa ni kuwa JK kaongea kama RAIS na AMIRI JESHI MKUU.
 
Dhaifu ni dhaifu tu na ukweli ni kwamba jei kei ni dhaifu na uozo mkubwa.

Na c .c.yem ni legelege na nionavyo mwisho wao utakuwa mmbaya sana!

Wafanye wafanyavyo wajue nasisi tumechoka na tuko tayari kwa lolote,heri tufe kwaajili ya ukombozi kuliko kufa na kipindupindu.

Ole wao sisi tuko tayari,
ee mungu ibariki chadema.
Eee mungu ibariki tanganyika!
 
Aaah!! Kikwete ni Rais asiyejua madhara ya kauli zake. He's too weak to be the President.
 
Uongozi wa TBC ulishatoa taarifa serikalini kuwa mitambo yao ina tabia ya kubadirisha kauli za watu hasa viongozi wa juu, na kuwafanya wasikike tofauti na walivyoongea.
Hivyo basi tunapenda kuwahakikishia watanzania kuwa, rais hakupata kuongea kauli hiyo mahala popote, ni bahati maya kuwa tatizo hilo la kiufundi, safari hii limeathiri kauli ya rais.
Wizara imeshaongea na makandarasi kutoka China na Madagascar ambao wataingia muda wowote kuanzia mwezi October kwa ajili ya kushughulikia tatuzo hilo.
Tunawaomba radhi wananchi kwa usumbufu uliojitokeza baada ya kauli na maelezo ya rais kuharibiwa na mitambo.

Imetolewa na Kurugenzi ya mawasiliano hapa kwenye Magogo.

Mkurugenzi wa hayo mawasiliano.
Saa ya silva Rey na Mamuu.
 
Amechoka na amani ana taka kujaribu kwanza ya Rwanda na Burundi.

naunga mkono kauli ya mh.mwenyekiti hatutakuwa wapole wapole tena hadi mbowe anasdma ngumi zitalika ikibidi mbungen,sugu anarusha gumi bungen
 
Hapo tuna kazi kwelikweli "imbombo jilipo"Kama kiongozi wa nchi ana toa kauli kama hiyo wakati anahimiza utawala bora,na ameridhia jeshi la Polisi liboreshwe kwa gharama kubwa,Pia anaelewa vema jinsi watu wake wasivyojua kutafakari na kupambanua kauli za watawala wao!Mfano ni utekelezaji wa oparesheni tokomeza.Lakini si shangai sana,yaweza kuwa ndiyo lugha ya awamu hii ya utawala"aha wapigwe tuu,maana tumechoka sasa"
 
Alicho sema sawa tu.
Kama vyama vingine vina fanya uhuni na ugaidi ili kuwatusha watu wasipige kura njia nzuri ni kujibu mapigo kwa kuwalinda wakapige kura.
Wakizongea vituo vya kuisabia kura nao ccm wazongee
Fujo za uchaguzi za wengine jawabu ni jino kwa jino

Hapana! Kujibu mapigo haipaswi kuwa justified unless we're a failed state which is far from being true. Ingawa sikupata nafasi ya kusikia alichokisema rais lakini sidhani kama tumeelewa kama alivyokusudia kueleweka. Sidhani kwa kuwaambia wana CCM wasiwe 'wanyonge' alimaanisha wapambane, nahisi alikuwa na maana wana CCM wasiogope kufanya siasa halali kwa kuogopa nguvu ya upinzani kisiasa. Kama mwenyekiti wa CCM, si kama rais, ana jukumu la kuwatia moyo wanachama wake wafanye siasa za ushindani bila woga, bila mapambano ya nguvu. Siwalaamu wanaotafsiri kauli hii kama wito wa mapambano lakini siami ndivyo ilivyokusudiwa.
 
Back
Top Bottom