Wana CCM acheni unyonge - Kikwete

Wana CCM acheni unyonge - Kikwete

Na Said Kubenea

JAKAYA Mrisho Kikwete, mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) taifa, anapaswa kushitakiwa kwa uchochezi.

Akifungua mkutano wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya chama chake mjini Dodoma leo, Kikwete alichochea wanachama wa CCM kuwapiga wapinzani kwa kudai kuwa, “Uvumilivu una kikomo.”

Amewataka wana CCM kuacha unyonge kwa madai kwamba wapinzani wamekuwa wakiwapiga huku wao wakisubiri polisi kuchukua hatua za kisheria.

Hii ina maana kwamba, Kikwete ambaye ni Rais wa Jamhuri ya Muungano, amewataka wanachama wa CCM, kuchukua sheria mkononi. Ametaka wananchi kuumizana, kupingana na kuuana. Huu ni uchochezi unaoweza kuingiza nchi katika machafuko ya kisiasa, kidini na kijamii.

Kama Kikwete alitaka urais, bila shaka alijipima na kujiona anaweza kufanya kazi hiyo. Kama alikuwa anajua anakwenda Ikulu kujaribu, basi alikuwa amekosea. Ikulu siyo sehemu ya kujaribu.

Kauli ya Kikwete ya kutaka wananchi wajibu mapigo, ni ishara kwamba ameomba kazi ambayo haiwezi.

Rais wa nchi hawezi kuchochea raia wake kupigana. Anapaswa kutumia vyombo alivyonavyo kusimamia sheria.

Ni lazima akumbushwe kwamba nchi hii ikiingia katika machafuko au mauaji ya halaiki, yeye ndiye atakuwa wa kwanza kuulizwa. Anaweza asiulizwe na vyombo vya sheria vya hapa, lakini ataulizwa na vyombo vingine vya dunia.

Yeriko hampaswi kumsuta JK kwa kauli yake, mnapaswa kujiuliza kama aliyoyasema ni ya kweli na kamani ya kweli basi muone umuhimu wa kubadilika amani ya Tanzania haitalindwa na rais KIKWETE au CCM peke yao, ni jukumu la taifa zima mkiwemo ninyi mnaolalamkiwa.
 
Kujibu mapigo mhimu,chadema wakipelekwa mahakamani wanafutiwa mashitaka! Sasa lazima wajibiwe on time! Una beep una pigiwa! Namuunga mkono JK kwa hili
 
Kubenea umekurupuka kuandika haya, taarifa kama hizi peleka fb....kwani alitaja matumizi ya silaha?, wana ccm udhaifu wao ni kwamba si wepesi wa kuongea kwa kubishana kama walivyo wanachadema..kipimo cha busara ya wana cdm kinaonekana wazi hapa Jf (chadema forum)....je jina Slaa waliosema NCHI HAITATAWALIKA? kauli gani inaambatana na vitisho vya wazi?...sit down and rethink kama we ni Great thinker au ni kama hawa wenzio chagadema victims..
 
Raisi wetu ana stress, ametoka kuulizwa maswali juu ya ujangili na mabwana zake wa ulaya, angesubiri akatulia kabla ya kutoa kauli yoyote
 
Na Said Kubenea

JAKAYA Mrisho Kikwete, mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) taifa, anapaswa kushitakiwa kwa uchochezi.

Akifungua mkutano wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya chama chake mjini Dodoma leo, Kikwete alichochea wanachama wa CCM kuwapiga wapinzani kwa kudai kuwa, “Uvumilivu una kikomo.”

Amewataka wana CCM kuacha unyonge kwa madai kwamba wapinzani wamekuwa wakiwapiga huku wao wakisubiri polisi kuchukua hatua za kisheria.

Hii ina maana kwamba, Kikwete ambaye ni Rais wa Jamhuri ya Muungano, amewataka wanachama wa CCM, kuchukua sheria mkononi. Ametaka wananchi kuumizana, kupingana na kuuana. Huu ni uchochezi unaoweza kuingiza nchi katika machafuko ya kisiasa, kidini na kijamii.

Kama Kikwete alitaka urais, bila shaka alijipima na kujiona anaweza kufanya kazi hiyo. Kama alikuwa anajua anakwenda Ikulu kujaribu, basi alikuwa amekosea. Ikulu siyo sehemu ya kujaribu.

Kauli ya Kikwete ya kutaka wananchi wajibu mapigo, ni ishara kwamba ameomba kazi ambayo haiwezi.

Rais wa nchi hawezi kuchochea raia wake kupigana. Anapaswa kutumia vyombo alivyonavyo kusimamia sheria.

Ni lazima akumbushwe kwamba nchi hii ikiingia katika machafuko au mauaji ya halaiki, yeye ndiye atakuwa wa kwanza kuulizwa. Anaweza asiulizwe na vyombo vya sheria vya hapa, lakini ataulizwa na vyombo vingine vya dunia.

Itakuwa kama Somalia kabla haijasaidiwa na mataifa jirani; itakuwa mwenye nguvu ndiye muamuzi wa lolote. Ni kiashirio cha kukosekana hekima ya kiuongozi.
 
Nadhani ataomba radhi kwa hili; nayeye ni binadamu ulimi unaweza kuteleza tuuu hasa kama mtu ana hangover
 
UTAIFA ndio kumtukana Rais? Rais hawezi kutukanwa na hawa wahuni halafu sisi watanzania wazalendo tukanyamaza.

Sawa nakubali Rais katolewa kauli zisizo na staha! Je! Wewe kwa upande wako umejiuliza ni nini kauli za Rais zenye UKAKASI KIASI HICHO?!
Yeye ni kiongozi wa Nchi, kauli aliyoitoa inajenga?
 
gazeti.JPG
 
CCM Mmechoka na M/Kiti wenu amechoka mno!
Tuhuma kwa upinzani;Mlianza udini mkashindwa, Ukabila Mkashindwa, Ukanda Mkashindwa, Ugaidi Mkashindwa sasa mnaleta ngonjera kuwa mnashambuliwa na cdm. Watanzania wanajua kila kitu, subiri moto wa 2015!
 
Anataka wachukue hatua kama hizi bila hofu. Maana hakuna wa kupelekwa Polisi wala mahakamani kama ilivyotokea hapo
ImageUploadedByJamiiForums1392537752.531452.jpg
ImageUploadedByJamiiForums1392537792.060006.jpg
 
Kikwete ana mengi sana ya kujibu. Kwanza majeshi yote yako chini yake na Polisi na Wanajeshi wametesa na kuua raia kwa maagizo yake. Pili anapaswa kushtakiwa kwa kukalia list ya wauza madawa ya kulevya na tatu sasa anakalia list ya majangili.

AIBU!
 
Hao wanaofanya hayo maovu,
Hao wanaojiita Makamanda,
Hao wanaojiita Red Brigade,
Hao wote wanaongozwa na watu,

Watu hao ni Mbowe na Slaa Mkiti na Katibu wa Chama,

Washitakiwe hawa kwanza na wabunge kama Msigwa,Kasulumbayi na Lema hawa wamesababisha vifo,fujo na majeraha yasiyopona.

Mathalani watu wamekatwa mikono utamlipa nini masikini huyu kinacholingana na mkono wake? Kisa chadema.

Kuna watu Bugando wamenyofolewa Macho,utamlipa nini mtu huyo ili aone haki imetendeka? kisa Chadema.

Stahili ya mauaji,fujo,mapanga,Tindikali,uvamamizi na nondo ndio demokrasia?

Washitakiwe Mbowe na Slaa,Lema,Kasulumbayi na Msigwa ili haki ipatikane.

kama ni kweli wamefanya maovu hayo uliyoyataja hapo juu, na hawajashtakiwa, nalazimika kuamini kwamba; Raisi na serikali yake ni Dhaifu na hawafai kuiongoza Tanzania.
 
Raisi wetu ana stress, ametoka kuulizwa maswali juu ya ujangili na mabwana zake wa ulaya, angesubiri akatulia kabla ya kutoa kauli yoyote

Hata alipoulizwa kuhusu msimamo wake juu ya 'USHOGA' jamaa alishindwa kujibu jambo ambalo ni aibu na fedheha kwa rais wa nchi kutokuwa na msimamo kwa mambo ya kipuuzi kama hayo. Kila kitu kwake hajui hata siku za nyuma alipoulizwa sababu za Tanzania kuwa maskini alisema pia hajui.
 
Tanzania tunamajanga mengi ila janga kuu ni Kikwete.
 
Huyu Kubenea ni Mtanzania kweli!?

Unashindwa kuelewa hata hii mada! Ndiyo maana unaiunga mkono CCM ya leo; understanding capacity yako iko chini sana? Au wewe si M-Tz (unako kwenu kwingine) itakapotokea tukapata mwenyekiti mwingine kwenye Chama cha upinzani mwenye maamuzi kama ya Kikwete, halafu yakaanza mapambano wewe utaihama nchi hii uende kewnu? Lakini ungekuwa M-Tz ungeona hatari inavyotafutwa na kiongozi wetu huyu. Afrika ya kati ni hivihivi, Somalia ni hivihivi nk. Naamini hata Shetani anakushangaa.
 
Aisee kweli kuna watu vichwa ngumu, sasa Dr Slaa na Mbowe wanaingiaje hapa, kumbuka ccm wakianza kutekeleza kauri ya uchochezi ya Kikwete, hata ndugu zako waliopo upinzani hawatapona, au unafikiri wewe kuwa ccm, na ndugu zako wote wapo ccm, hao unaosema wamekatwa mikono waliopo Bugando, kawaulize ccm wenzio, wakupe siri ya kitu walichokifanya kwa hao wenzenu waliokatwa mapanga, hiyo ndiyo ccm bwana, na wewe endelea kushangaa huko, waje wakutoa mhanga ili wao wafanikiwe wanachokitaka.
 
Na Said Kubenea

JAKAYA Mrisho Kikwete, mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) taifa, anapaswa kushitakiwa kwa uchochezi.

Akifungua mkutano wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya chama chake mjini Dodoma leo, Kikwete alichochea wanachama wa CCM kuwapiga wapinzani kwa kudai kuwa, “Uvumilivu una kikomo.”

Amewataka wana CCM kuacha unyonge kwa madai kwamba wapinzani wamekuwa wakiwapiga huku wao wakisubiri polisi kuchukua hatua za kisheria.

Hii ina maana kwamba, Kikwete ambaye ni Rais wa Jamhuri ya Muungano, amewataka wanachama wa CCM, kuchukua sheria mkononi. Ametaka wananchi kuumizana, kupingana na kuuana. Huu ni uchochezi unaoweza kuingiza nchi katika machafuko ya kisiasa, kidini na kijamii.

Kama Kikwete alitaka urais, bila shaka alijipima na kujiona anaweza kufanya kazi hiyo. Kama alikuwa anajua anakwenda Ikulu kujaribu, basi alikuwa amekosea. Ikulu siyo sehemu ya kujaribu.

Kauli ya Kikwete ya kutaka wananchi wajibu mapigo, ni ishara kwamba ameomba kazi ambayo haiwezi.

Rais wa nchi hawezi kuchochea raia wake kupigana. Anapaswa kutumia vyombo alivyonavyo kusimamia sheria.

Ni lazima akumbushwe kwamba nchi hii ikiingia katika machafuko au mauaji ya halaiki, yeye ndiye atakuwa wa kwanza kuulizwa. Anaweza asiulizwe na vyombo vya sheria vya hapa, lakini ataulizwa na vyombo vingine vya dunia.

Wakataze wanachama wenzio kushambulia.
Usipofanya hivyo basi mtashambulia na mtapigwa!!
Hamna nguvu ya hoja, hamna nguvu ya umma, hamna nguvu ya mwili na hamna akili.
Sheria ipo in your favour, the weak and minority. Mkiivunja then you're done, that's it!!
 
Mbona hukusema haya wakati wana CCM wamechomewa nyumba, wamekatwa mikono na kutolewa macho huko kahama?

Mbona hukuwashitaki Mbowe na Slaa wanaotembea kwa chopper kushinikiza ngumi na mapanga kila siku?

Mchochezi ni nani? Umemwelewa JK we Kubenea au ni muendelezo wa majungu yako ya kukosa kuteuliwa nae tangu 2005?

JK hakumaanisha mapanga wala ngumi, na kama unapenda haki dhidi ya wachochezi basi faili la kwanza Mahakamani washitakiwe Mbowe na Slaa pamoja na wabunge wao kwa uchochezi na utekelezaji wa mauaji.

Nenda Bugando Mwanza ukawaone majeruhi ndo uje uandike makala yenye haki.

Kubenea unajiaabisha.
Hata wao chadema watakushangaa kama unasimama kuwatetea.

Ushahidi wa mwanzo ni namna wananchi walivyoamua kuwakataa kupitia kura na kuambulia kata 3, je unadhani hiyo ni kawaida?

Kubenea vua miwani ya ushabiki uitendee haki kalamu yako.

Ndugu tatizo linalolisibu Taifa la wapinzani na wana-CCM kupigana linatokana na haki kutokutendwa kwa makundi yote mawili. Mara ngapi wapinzani wamekuwa wakipigwa na kuumiza huku Serikali na vyombo vyake vya ulinzi na usalama wakifumba macho as if walioumizwa ni mapaka!!! In fact Rais hakupaswa kutoa kauli kama hiyo. Huo ni udhaifu wa wazi wazi. Kwani wapinzani sio raia wa Tanzania?!!!
 
Back
Top Bottom