Wana CCM acheni unyonge - Kikwete

Wana CCM acheni unyonge - Kikwete

Mkuu chuki naona amekula kona!
 
Last edited by a moderator:
wapi rais alipohamasisha mauaji? Mbona mnatekwa na hizi siasa uchwara za chadema?

mwambieni wanachadema tuko tayari kuifia nchi yetu kwa ukombozi wa pili dhidi ya mkoloni mweusi c.c .yem!
 
YERICKO NDIE MCHOCHEZI.HII TAARIFA KAILETA YERICKI NA SI KUBENEA.HIVYO WA KULAUMU KWA UCHOCHEZ NI YERICKO NA KIMBELEMBELE KAMA MAFUA YA ASUBUHI.KWANZA YERICKO Mzushi sana kuliko pepo mchafu.we tangu lini na wapi dunian rais aliagiza raia wake hususan wanachama wake wapigane na wapinzani;?rais anamiliki vyombo vya mabavu kuliko wanachama,kwa nini asitume hivo vyombo atume wanachama?hamuwezi kuona yericko alivo mnafiki na mzushi?mi nadhani hii habar imetungwa na yericko na kumsingizia kubenea.

Kwani YERICKO ndiye aliyemtuma mh.Rais atoe kauli hiyo ya uchochezi? Hata kama Kubenea ama Yericko hawakuyasema haya, umma na ulimwengu mzima tumesikia. Inashangaza kuona Rais wa nchi anachochea vurugu kwa kufata ITIKADI, wakati yeye ni RAIS wa wananchi wote.
 
Sasa ndio kikwete ameonyesha udhaifu wake watu waliposema ni dhaifu ilionekana anaonewa, haiingii akilini kwa rais wa nchi kutoa kauli za kipumbavu kama hizi hii inazihilisha kuwa hatuna viongozi ktk nchi hii kauli nyingine tata aliitoa mh pinda[wapigwe tu] hii ni hatari sana ktk taifa letu, tujiandae kushuhudia umwagikaji mkubwa wa damu ktk uchaguzi wa ubunge jimbo la kalenga.
 
Acha dharau wewe kila mtu ana haki ya kuandika anachokiona

huyu kubenea kachanganyikiwa, forum yake aliyoianzisha kabaki mwenyewe na malaria sugu na yericko nyerere, watu wenye akili timamu hawawezi kumsikiliza kubenea, labda misukule ya pale mtaa wa ufipa, kwanza huyu kubenea sio mtanzania huyu
 
Hao wanaofanya hayo maovu,
Hao wanaojiita Makamanda,
Hao wanaojiita Red Brigade,
Hao wote wanaongozwa na watu,

Watu hao ni Mbowe na Slaa Mkiti na Katibu wa Chama,

Washitakiwe hawa kwanza na wabunge kama Msigwa,Kasulumbayi na Lema hawa wamesababisha vifo,fujo na majeraha yasiyopona.

Mathalani watu wamekatwa mikono utamlipa nini masikini huyu kinacholingana na mkono wake? Kisa chadema.

Kuna watu Bugando wamenyofolewa Macho,utamlipa nini mtu huyo ili aone haki imetendeka? kisa Chadema.

Stahili ya mauaji,fujo,mapanga,Tindikali,uvamamizi na nondo ndio demokrasia?

Washitakiwe Mbowe na Slaa,Lema,Kasulumbayi na Msigwa ili haki ipatikane.
Uliyoyaongea yawezekana ikawa kweli,Lakini unapaswa uangalie kauli ya mtu aliyeitoa anawadhifa gani kwa Taifa,Rais wa nchi anatoa kauli tata kama hii wewe kwa ujinga wako unaona ni sawa,unataka Slaa,Mbowe na Msigwa washitakiwe,uliwahi kuwasikia wakitamka wanachadema wawapige CCM? Sasa unaonaje Rais wako akiwa wakwanza kushitakiwa kwa mauaji ya Mwangosi,mauji ya Arusha na pengine popote pale mauaji yalipotokea yaliyofanywa na polisi wake,ambayo yeye ndiye anaewatuma kutekeleza mauaji hayo.?Usiwe mbumbumbu wa sheria kiasi hicho kisa unalipwa na CCM hizo7000.
 
Mbona kila jambo la KIUTAIFA mnaingiza vyama!? Fungueni akili zenu waTanzania wenzangu.

UTAIFA ndio kumtukana Rais? Rais hawezi kutukanwa na hawa wahuni halafu sisi watanzania wazalendo tukanyamaza.
 
Mbona hukusema haya wakati wana CCM wamechomewa nyumba, wamekatwa mikono na kutolewa macho huko kahama?

Mbona hukuwashitaki Mbowe na Slaa wanaotembea kwa chopper kushinikiza ngumi na mapanga kila siku?

Mchochezi ni nani? Umemwelewa JK we Kubenea au ni muendelezo wa majungu yako ya kukosa kuteuliwa nae tangu 2005?

JK hakumaanisha mapanga wala ngumi, na kama unapenda haki dhidi ya wachochezi basi faili la kwanza Mahakamani washitakiwe Mbowe na Slaa pamoja na wabunge wao kwa uchochezi na utekelezaji wa mauaji.

Nenda Bugando Mwanza ukawaone majeruhi ndo uje uandike makala yenye haki.

Kubenea unajiaabisha.
Hata wao chadema watakushangaa kama unasimama kuwatetea.

Ushahidi wa mwanzo ni namna wananchi walivyoamua kuwakataa kupitia kura na kuambulia kata 3, je unadhani
Unachosema ni kumtetea mtu ambaye hakustahili kutoa kauli kama ile,mara ngapi vijana wa green gard wamewapiga wanachama wa chadema? kuna mtu alichinjwa kule arusha,sasa kwanini tusiamini ni walitekeleza agizo la raisi?
 
Ndo tatizo la kuchagua rais weak km kikweche........Yaani jamaa hamnazo sana
 
kwani?, munashanga nini?, 2010 pindi anafungua kampeni pale Dar es salaam aliwambia wanaccm , kuwa kampeni si lelema mama, kampeni ni vita

mungu asaidie aondoke zake, huyu ni takataka tu,
kiongozi mkubwa kama yeye hawezi sema maneno, kama hayo tena aliyasema mara mbili mbili,

na akawambia wandishi wa habali kuwa mengine yote musiandike, andika hili yaani
uvumilivu basi, Jamani hivi ni uvumilivu gani walioufanya?
 
Nirudie kushangaa !!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!


Jueni Mungu anawapenda wanadamu wote

Kwa vyovyote mtu atakavyofanya Mungu ajua kumwadibisha hivyo vyama vyote ni mipango ya wanadamu ili waweze kuishi pamoja kwa upendo na ushirikiano .tukimuhusisha yeye atabariki kazi za mikono yetu.

Amani kwa watu wote.
 
Na Said Kubenea


JAKAYA Mrisho Kikwete, mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) taifa, anapaswa kushitakiwa kwa uchochezi.

Akifungua mkutano wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya chama chake mjini Dodoma leo, Kikwete alichochea wanachama wa CCM kuwapiga wapinzani kwa kudai kuwa, “Uvumilivu una kikomo.”

Amewataka wana CCM kuacha unyonge kwa madai kwamba wapinzani wamekuwa wakiwapiga huku wao wakisubiri polisi kuchukua hatua za kisheria.

Hii ina maana kwamba, Kikwete ambaye ni Rais wa Jamhuri ya Muungano, amewataka wanachama wa CCM, kuchukua sheria mkononi. Ametaka wananchi kuumizana, kupingana na kuuana. Huu ni uchochezi unaoweza kuingiza nchi katika machafuko ya kisiasa, kidini na kijamii.

Kama Kikwete alitaka urais, bila shaka alijipima na kujiona anaweza kufanya kazi hiyo. Kama alikuwa anajua anakwenda Ikulu kujaribu, basi alikuwa amekosea. Ikulu siyo sehemu ya kujaribu.

Kauli ya Kikwete ya kutaka wananchi wajibu mapigo, ni ishara kwamba ameomba kazi ambayo haiwezi.

Rais wa nchi hawezi kuchochea raia wake kupigana. Anapaswa kutumia vyombo alivyonavyo kusimamia sheria.

Ni lazima akumbushwe kwamba nchi hii ikiingia katika machafuko au mauaji ya halaiki, yeye ndiye atakuwa wa kwanza kuulizwa. Anaweza asiulizwe na vyombo vya sheria vya hapa, lakini ataulizwa na vyombo vingine vya dunia.


Sasa jeshi la polisi likae kando tuwashughulikie vizuri hawa mende wa kijani maana wanabebwa sana na Polisi. Sengikyu Mista Prezidenti!
 
Nadhani ataomba radhi kwa hili; nayeye ni binadamu ulimi unaweza kuteleza tuuu hasa kama mtu ana hangover
 
Back
Top Bottom