Wameanza Tena: Meseji usiku wa manane

There is nothing wrong with the message. kwani shida hizo zimeanza leo? so tangu awamu ya kwanza. why freak out now?

Nikiwa nimelala. Joto kali. Umeme hakuna. Nimeoga maji ya chumvi. Ya kunywa nanunua ndoo sh.600. Kero.

Mara napokea hii crap kutoka kwa namba ambayo ata siijui:

"WANANCHI TAFADHALI, WAKUJENGA NCHI NI SISI NA WA KUBOMOA NI SISI, TUNAPODAI HAKI PIA TUTIMIZE WAJIBU, MIGOMO NA MAANDAMANO KILA KONA NI SULUHU YA MATATIZO? TUSILAUMU JESHI LA POLISI, TUACHE SIASA ZA MIGOGORO NA KUTAFTA UMAARUFU, UCHAGUZI UMEPITA, TUKUBALI UKWELI"TUMA KWA WATU 10.

MY TAKE:
Hakuna haki bila wajibu; hakuna wajibu bila haki
 
Hizo ni message za CCM,tumeshazizoea na hazituzuii kuendelea na mapambano ya ukombozi wa nchi yetu!!
 
There is nothing wrong with the message. kwani shida hizo zimeanza leo? so tangu awamu ya kwanza. why freak out now?

Vipi mbona mnamkingia sana kifua jamaa yenu?kwa nini hamtaki kukubali amepoteza mwelekeo?mbona hawamu ya pili haikupigiwa kelele kama watu wana udini?someni alama za nyakati!!jamaa yenu amechemsha na habebeki hata kwa mbeleko ya chuma!!
 
Tujitulizeni jamani akilini, tuongeze taabu zetu kama taifa na maombi kwa Mwenyezi Mungu na wadhalimu wetu wote watadondoka kiajabuajabu tu na wengi wetu wala tusiweze kuamini kama ni kweli.

Nakubaliana na wewe kwamba tuongeze maombi ili Mungu awaangamize wadhalimu.
Ila maombi yetu yaambatane na matendo.

Kwenye historia ya kale watu wa Mungu WALIPOTESWA na kunyanyaswa na watawala wa enzi hizo aliwainulia wapiganaji kama Musa, Samsoni, Yefta, Joshua n.k!
Mimi naamini anatupigania kupitia wapiganaji ndani ya CUF, CDM na Activists wengine.
Watanzania tumenyanyasika ndani ya nchi yetu wenyewe aliyotubarikia Mungu, hatuna uwezo wa kumudu maisha. Wageni wanakula nchi kama haina mwenyewe. Kwenye mashirika na makampuni wageni wachache ndio wanalipwa karibu 50% ya mishahara ya wafanyakazi wote.
Mtanzania huna hata akiba ya kufurahia maisha na familia yako, ukijitahidi sana sana waenda Coco beach na kuwanunulia wanao mihogo ya kuchoma maana huwezi kuthubutu kuwapeleka Zamani Kempinski.

Kinachouma ni pale mtanzania mwingine anapokubali kutumika kuendeleza ufedhuli huu ama kwa udini, mabavu (polisi, jeshi), hadaa (kama sms hii), taaluma (mawakili, waandishi) yet ukiangalia maisha yake binafsi bado ni duni. Hata hawa kina Ngereja wanaopigania masilahi ya wachache bado familia na jamii yao ni masikini wa kutupwa. Au tuviweke vijumba vya jamaa zake huko Sengerema?? Kwa nini tunapenda kuogelea kwenye utajiri huku tumezungukwa na watanzania masikini???

Kutuma meseji kwa watu kumi za namna hiyo ni sawa na sh 590, ukipata watanzania milioni 1 tu wenye fikira mgando watatumia their hard earned half a billion kupropagate mbinu ya watawala (divide and rule).
Whoever wants to see some change for this Nation should start with the people around him/her(family, friends, work mates etc).

Inauma sana unapomjua mwizi wako halafu unashindwa kumwadhibu!!!!!!!!1
 
Whoever who is behind that sms, must be a chicken head!!! We are unstoppable... and they know that very well... let them continue to hit around the bush!!!
 
umenena vyema mkuu.

lakini hapo kwenye red naona unanipa 'za uso' bure tu. unanionea mkuu.
Inakubidi Ng'wanangwa ukubali tu! Maana wanaona kana kwamba wewe ndio mtuma meseji na si kwamba umetumiwa!!

Watu wana machungu... vumilia mkuu mradi ujumbe umefika.
 
Ng'wanangwa Ujumbe umesomeka nashukuru kwa ku2juza pia umeonyesha uzalendo.wanatafuta pa kufia mafisadi wakubwa.
 
Ndo maana walitaka watu wasajili namba,ili wasambaze 'cheap propaganda'!
 
asante kwa taarifa mkuu, mfa maji haishi kutapatapa sasa wanaanza kutumia vi sms vya kijinga kujisafisha. HATUDANGANYIKI NG'O
 
Poleni sana waungwana sasa ni bora hii msg haichefui sana kama ile ya PCCB...WEWE NI MLA RUSHWA TUNAKUJUA NA TUTAKUKAMATA....
 
Back
Top Bottom