Wameanza Tena: Meseji usiku wa manane | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wameanza Tena: Meseji usiku wa manane

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Ng'wanangwa, Jan 14, 2011.

 1. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #1
  Jan 14, 2011
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,180
  Likes Received: 897
  Trophy Points: 280
  Nikiwa nimelala. Joto kali. Umeme hakuna. Nimeoga maji ya chumvi. Ya kunywa nanunua ndoo sh.600. Kero.

  Mara napokea hii crap kutoka kwa namba ambayo ata siijui:

  MY TAKE:
  Hakuna haki bila wajibu; hakuna wajibu bila haki
   
 2. Kiranja Mkuu

  Kiranja Mkuu JF-Expert Member

  #2
  Jan 14, 2011
  Joined: Feb 18, 2010
  Messages: 2,100
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  C C C kazi yao ni kuvunja kubomoa na kuharibu mahusiano mazuri kwenye jamii.
  Hiyo ni meseji ya kichochezi.
  nawaonya mara moja CCM waache kusambaza meseji hizo za kichochezi.
   
 3. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #3
  Jan 14, 2011
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Ni nani wapuuzi hao tena?..ni chama cha jirani zetu nini?
   
 4. n

  niweze JF-Expert Member

  #4
  Jan 14, 2011
  Joined: Oct 21, 2009
  Messages: 1,008
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  I Thought They Have Brain But They are Out of It. Wanafikiri Kila Baada ya Miaka Mitano Kukubali Bila Kuchallange Matokeo Kumekuleta Nini Tanzania. Unafikri Jk na CCM Wataondoka Bila Maandamano na Nguvu ya Wananchi. Wananchi Tunaona "Waoga na Weak People" Wanaanza Kuvuta Mikia Chini ya Tumbo.

  This Time Hatuta Kaa Kimya.

  Mwananchi Gani Atakaa Kimya kwa Dowans? Mwananchi Yupi Atakaa Kimya Bila Umeme Wakati JK Anamlipa Rostam. Mwananchi Yupi Atakaa Kimya Bila Chakula Nyumbani? Mwananchi Yupi Atakaa Kimya Bila Pesa za Huduma Hospitalini? Mwananchi Yupi Atakaa Kimya Bila Pesa za Kupeleka Watoto Shule?

  CCM Wanafikiri Rostam Anatupenda Sana na Anawatakia Watanzania Maisha Mazuri Sana...
   
 5. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #5
  Jan 14, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Its too late... Hivi hawajatambua kwamba hata zile sms za wakati wa uchaguzi hazikuwasaidia??

  Actually kwa sasa ndio wanongea kero na kupandisha zaidi chuki na rais aliyepo kwani hiyo mitandao inayotumika ndio ile iliyotukana wengine, ni mabilioni ambayo yangeweza kuwalipa dowans... kama wana upendo sana na nchi yao,

  Ni mradi wa mtu kuingiza pesa kupitia vodacom

  Kikwete, quit using those junk sms, zinaweza kuhitajika siku moja na watu wakadharau kwani mna-abuse information systems
   
 6. Husninyo

  Husninyo JF-Expert Member

  #6
  Jan 14, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 23,814
  Likes Received: 592
  Trophy Points: 280
  Wanatuma hizo sms na si ajabu gharama ya hiyo sms tunalipia wenyewe tunaotumiwa. Lol!
   
 7. C

  Chief Rumanyika Senior Member

  #7
  Jan 14, 2011
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 138
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ha ha ha haaa, imagine meseji hiyo kakutumia FISADI ORIJINO Rostam Aziz aliyekufanya ulale giza, oga chumvi nusu ndo, kula joto kwa sana na mlo ulioupata tu mchana halafu awe anakuja na BEMBELEZA MJINGA wa aina hii!!!

  Watanzania HATUDANGANYIKI tena, minyororo yote lazima tukayakatishe na kufungua ukurasa mpyaaaaaa!!!!!!!!!!!!!!
   
 8. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #8
  Jan 14, 2011
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  Its too late kwao tena wasije wakathubutu kunitumia meseji kama hizo nafikiri hiki ni kile chama cha majirani zetu
   
 9. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #9
  Jan 14, 2011
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,481
  Likes Received: 5,862
  Trophy Points: 280
  Poleni nyote wawili kwa kuguswa na maswahibu haya ya nchi hii.....kumbatianeni yaishe
   
 10. C

  Chief Rumanyika Senior Member

  #10
  Jan 14, 2011
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 138
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ndugu NIWEZE, kweli umemva bwana Ng'wanang'wa jumlajumla kimakosa tu.

  Huyu ndiye aliyekuwa AKITONGOZWA NA SERIKALI YA KIKWETE usiku wa manane ili akubali tu kupumbazika na vile vile akawasaidie kuwapumbaza na Watanzania wengine zaidi kwa msingi ule ule wa AMANI NA UTULIVU LAKINI BILA HAKI kwa kuwa dhawabu itakuwa inawasubili mbinguni tu wakifanya hivyo na kuwafanikishia RA na EL waendelee tu kutafuna nchi.

  Ng'wanang'wa mtu AKIKUTONGOZA USIKU WA MANANE tena mwambie hudanganyiki!
   
 11. P

  Phillemon Mikael JF Gold Member

  #11
  Jan 14, 2011
  Joined: Nov 5, 2006
  Messages: 8,856
  Likes Received: 2,432
  Trophy Points: 280
  Kwenye uchaguzi rais alimpa mwanaye Miraj bilioni 1 ,akishirikiana na mateja wenzake wa VIJANA ZAIDI .....kwa ajili ya kusambaza meseji za kuwatukana wapinzani.......hii ya sasa sijui atakuwa amempa shilingi ngapi kufanya kazi hii rahisi....najuuta kusajili namba yangu!!
   
 12. Joseph

  Joseph JF-Expert Member

  #12
  Jan 14, 2011
  Joined: Aug 3, 2007
  Messages: 3,527
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  chukua chako mapema!!!vita ni vita mura!
   
 13. M

  Mkeshaji JF-Expert Member

  #13
  Jan 14, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 4,264
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  wananchi tumetimiza wajibu zetu nyingi tu, lakini cha kushangaza hawatupi haki yetu. so hayo maneno walitakiwa wajiambie wao wenyewe sio sisi.

  "Justice delayed is justice denied"
   
 14. Saharavoice

  Saharavoice JF-Expert Member

  #14
  Jan 14, 2011
  Joined: Aug 30, 2007
  Messages: 2,644
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Wanaogopa Nguvu ya wananchi
   
 15. Edson

  Edson JF-Expert Member

  #15
  Jan 14, 2011
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 9,202
  Likes Received: 722
  Trophy Points: 280
  na mimi nimetumia uchafu huo leo saa saba usiku.........ccm wapuuzi sana na hawana.......
   
 16. C

  Chief Rumanyika Senior Member

  #16
  Jan 14, 2011
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 138
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ni kweli utawala wa kidhalimu husababisha taifa kuishi kwa hasira isiyoisha na watu kurukwa akili katika mengi sana. Tusameheane bure katika hali ya aina hii inapojitokeza hata bila ya sisi kutambua hilo.

  Jamani ukiangalia hali iliyojitokeza hapa juu kati ya ndugu zetu NIWEZE kwa kumva moja kwa moja NG'WANANG'WA kwa hasira kali bila hata kutafakari maelezo na mazingira yake ni KIELELEZO TOSHA KWAMBA MPAKA SASA WATANZANIA WAMEGHADHABIKA kiasi kwamba kuna uwezekano akatenda tendo lolote la ajabu kama vile kumua mtu ndiyo baada aje agundue kwamba alifanya hivyo kimakosa.

  Tujitulizeni jamani akilini, tuongeze taabu zetu kama taifa na maombi kwa Mwenyezi Mungu na wadhalimu wetu wote watadondoka kiajabuajabu tu na wengi wetu wala tusiweze kuamini kama ni kweli.

  Ng'wanang'wa bado nakukumbuka na Thread yako ya Kikwete kwenye vita vya ajabu mno na waasi wa KIFIKRA. Mapambano mbeleee mpaka kieleweke!!!
   
 17. T

  Tata JF-Expert Member

  #17
  Jan 14, 2011
  Joined: Dec 3, 2009
  Messages: 4,741
  Likes Received: 661
  Trophy Points: 280
  Umenena vyema na ningependa kuangalia kwa undani ulichonena kwa muktadha wa Tanzania.

  Ni kweli kuwa wajenga nchi ni sisi wananchi wenyewe na wabomoa nchi ni sisi wananchi. Ili wananchi waweze kujenga nchi lazima washiriki kikamilifu kwenye mchakato wa ujenzi wa nchi. Wanashiriki mchakato huo kwa kuwachagua wawakilishi wanaowataka na kuwasimamia ili watekeleze yale waliyowatuma kuyasimamia.

  Ili uweze kuwachagua na kuwasimamia wawakilishi unahitaji mchakato endelevu wa KISIASA ambao siyo tu utawapa wananchi fursa ya kuchagua wawakilishi bali pia uwezo wa kuwasimamia utendaji wao wa kila siku na kama hawafikii malengo waliochaguliwa kuwaondoa madarakani ili kuchagua wengine. Mchakato wa aina hii hauwezi kuwa wa msimu wa uchaguzi peke yake. Kwa ufupi huwezi kufananisha mchakato wa KISIASA na ununuzi wa wa mazao ya kilimo kama korosho au pamba wakati wa msimu wa mavuno. SIASA ni mchakato endelevu na unakuwepo muda wote ili kuwawajibisha wawakilishi watekeleze wajibu wao. Tatizo letu Tanzania tunadhani siasa ni shughuli ya msimu ambayo inaanza na kuisha baada ya mchakato wa uchaguzi.

  Umenena vyema kuwa HAKI inadaiwa haiombwi. Ukiona mpaka mtu anafikia hatua anadai haki yake ujue amenyimwa na yule aliyepaswa kumpatia. Suala la msingi hapa siyo kuangalia ni jinsi gani haki inadaiwa na mdai haki bali ni kuangalia kwa nini mpaka mtu adai HAKI yake ambayo alitakiwa aipate katika utaratibu wa kawaida usio na mizengwe wa mtoa haki.

  Katika mazingira ambapo KATIBA inatoa HAKI kwa wananchi halafu serikali inatunga sheria na kuweka taratibu ambazo kimsingi zinazuia hiyo haki kutolewa basi sioni ni jinsi gani mdai HAKI ataweza kuipata bila kuingia kwenye mgogoro na waliopewa dhamana ya kutoa haki hiyo bila mizengwe. Kwa ufupi ninakunyima haki yako halafu ninakupangia utaratibu wa jinsi ya wewe kunidai haki yako bila kunibughudhi. Utaipata kweli hiyo haki?

  Kwa suala la maandamano Tanzania kuna ushahidi kuwa hakuna maandamano ya kudai haki ya kisiasa au kijamiii (mfano wanafunzi) yanayoruhusiwa nchini bila ya wadai haki kuingia kwenye mgogoro na jeshi la polisi. Kiini cha tatizo hili ni kuwa wanaodaiwa haki ndio wenye mamlaka ya kuwaamuru hawa mapolisi watoe ama wasitoe "kinachoitwa kibali" cha maandamano ili wale wanaodai haki waweze kuandamana. Sasa kwa akili ya kawaida kabisa je unadhani hakuna mgongano wa kimaslahi hapa hasa pale watoa haki wanapokuwa wameacha kutekeleza wajibu wao kwa makusudi na kupelekea mgogoro wa kudai haki?

  Umeshauri tuache siasa za mgogoro na kutafuta umaarufu. Hapa nashindwa kuelewa ufahamu wako kuhusu maana ya neno Mgogoro na hasa dhana ya siasa isiyokuwa na mgogoro. Ninavyofahamu siasa inahususha mapambano ya hoja na maoni baina ya wanasiasa kila mmoja akiwashawishi wapiga kura kuwa yeye ana njia nzuri zaidi ya kutatua matatizo yao. Tofauti za hoja na maoni ya wanasiasa zinajitokeza pia kwenye makundi mbali mbali yanayokuwa na misimamo tofauti kuhusu masuala mbalimbali ya kisiasa. Mgongano wa maoni unaweza kutokea ndani ya chama kimoja au baina ya chama na chama. Mgongano wa hoja na maoni unapoendelea bila kufikia muafaka wa haki kwa pande zote zinazohusika unageuka na kuwa kuna mgogoro hasa pale kila kundi linapo simamia upande wake na kupelekea sintofahamu inayoathiri watu wengi zaidi.

  Hivyo kwa mantiki hiyo hapo juu huwezi kuwa mwanasiasa halafu ukaogopo siasa za migogoro kwani siasa yenyewe inajengwa kwenye tofauti za maoni na mitazamo ambayo ndio kiini cha migogoro. Kinachotakiwa ni kutafuta jinsi nzuri zaidi ya kutatua tofauti hizi za maoni na mawazo ambazo mara nyingi huwa ni za ndani na kuepusha kutokea kwa migogoro.
   
 18. Iza

  Iza JF-Expert Member

  #18
  Jan 14, 2011
  Joined: Jan 8, 2009
  Messages: 1,848
  Likes Received: 120
  Trophy Points: 160
  Ukimaliza kuisoma sms ya namna hiyo DELETE..
   
 19. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #19
  Jan 14, 2011
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,180
  Likes Received: 897
  Trophy Points: 280
  umenena vyema mkuu.

  lakini hapo kwenye red naona unanipa 'za uso' bure tu. unanionea mkuu.
   
 20. Y

  Yaptz Member

  #20
  Jan 14, 2011
  Joined: Oct 29, 2010
  Messages: 43
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mfa maji huwa haachi kutapatapa, wamerikologa sasa wanatafuta mchawi wamshushie Lawama zote...... Wewe unaua watu alafu hunajaribu kutafuta every existing jusfication to justify killing...... Haikubaliki
   
Loading...