Wameamua wawe na mtoto moja tu licha ya kuwa na uwezo wa kuongeza na kulea, je hii ni haki kwa mtoto wa kiafrika?

NetMaster

JF-Expert Member
Sep 12, 2022
1,454
4,853
Ni wazazi wawili, mke ni mhasibu taasisi ya kiserikali, mme ni engineer, kielimu wapo vizuri kuna moja aliweza kusoma masters yake nje ya nchi na mwingine ni hapa hapa bongo ila ana elimu kubwa. Mtoto walie nae ni moja tu yupo darasa la saba.

Sababu kuu ya kuwa na mtoto moja ni mke kutotaka mimba kumuharibia malengo yake ya career / ofisini, inabidi awe anaenda kazini kila siku za kazi.

Wazazi ni wasomi na wapo focused sana na career zao, mtoto wanamjali sana katika masomo yupo moja ya shule poa sana, ni ya day ila ada yake imechangamka.

Lakini je hii ni sawa kwa mtoto wa kiafrika kutokuwa na kaka, dada ama wadogo zake ?
 
Ni wazazi wawili, mke ni muhasibu taasisi ya kiserikali, mme ni engineer, kielimu wapo vozuri kuna moja aliweza kusoma masters yake nje ya nchi na mwengine ni hapa hapa bongo ila ana elimu kubwa.

Mtoto walienae ni moja tu yupo darasa la saba.

Wazazi ni wasomi na wapo focussed sana na career zao, mtoto wanamjali sana katika masomo yupo moja ya shule poa sana, ni ya day ila ada yake imechangamka.

lakini je hii ni sawa kwa mtoto wa kiafrika kutokua na kaka, dada ama wadogo zake ?
Mwambie huyo unaemtetea, akikuwa akazae anaohitaji
 
Ukiona mtu anakomea mtoto mmoja jua wana matatizo kwenye mfumo wa uzazi.

Kuwa na watoto wengi, maana yake ukoo wako utakuwa mkubwa zaidi
 
Kuzaa zaa sana ni tabia za Maskini.. huoni hata kina Bill Clinton na mahela yao yote wana mtoto mmoja?? George Bush wawili, Barack Obama wawili n.k. Matajiri wanatafuta pesa kwa kizazi kijacho hayo mambo ya kila mtoto atakuja na ridhiki yake ni ya zama za ujima.
Kabisa
 
Kuzaa zaa sana ni tabia za Maskini.. huoni hata kina Bill Clinton na mahela yao yote wana mtoto mmoja?? George Bush wawili, Barack Obama wawili n.k. Matajiri wanatafuta pesa kwa kizazi kijacho hayo mambo ya kila mtoto atakuja na ridhiki yake ni ya zama za ujima.


sio kila mifano hao uliowataje ni.wa kupigiwa mfana.
 
Back
Top Bottom