Wamachinga hawachukiwi- Wanasiasa acheni taaluma ifanye kazi ili kupanga miji

crome20

JF-Expert Member
Feb 5, 2010
1,130
721
Ni ukweli usio na shaka mahali popote duniani kuwa miji na matumizi ya maeneo katika miji hupangwa. Mipango miji ni TAALUMA na inasomewa.

NI ukweli pia usiopingika kuwa kuwa MAZINGIRA ni taaluma, inasomewa pia BIASHARA ni taaluma .
Katika manispaa na miji wataalamu hawa wameajiriwa ili kuratibu maendeleo na ukuaji wa miji na majiji.

Ni ukweli pia kuwa wamachinga wanafanya shughuli zao kinyume na sheria, na tatizo la wamachinga limetokana na wanasiasa kuingilia taaluma kwa maslahi yao ya kisiasa.

Miji ikipangwa vizuri inarahisha shughuli nyingi kufanyika kwa urahisi na kupunguza athari za kiafya ikiwemo kupunguza stress zinazotokana na msongamano, hewa chafu n.k.

Fikiria wamachinga wamefika hatua ya kufunga kituo cha daladala pale Congo Kariakoo, Manzese, halafu eti traffic Police anatoka jasho kuongoza magari kutokana na daladala kutokuwa na sehemu ya kushusha abiria

Wale mliowahi kufika katika miji iliyopangwa mtakuwa mashahidi kwamba unaweza hata kwenda mahali kama kutalii ndani ya mji kufurahia mandhali, hewa, taaluma ya usanifu n.k

Wamachinga wasiondolewe tu maeneo ya watembea kwa miguu, bali vibanda vyao vimekuwa ni UCHAFU unaotia doa kazi ya usanifu wa majengo na barabara. Mfano, fikiria mandhali sehemu katikati ya mji, halafu unakuta kipanda cha mabati, mabox, mbao, n.k.

Hata kama hakiko barabarani ni UCHAFU. Hivi vile vibanda vya mabati na mabox nje ya mlimanCity si ni UCHAFU, au ukute kibanda cha viroba pale Ubungo interchange si ni sawa na kutengeza bustani nzuri halafu mtu mtu aanze kutengezea gari ndani ya bustani.

Muda ni sasa, elimu ya ujasiliamali itolewe, ubunifu uongezeke, na isiwe kila kijana anafikiria biashara ya umachinga. Hii dhana kuwa watageuka kuwa vibaka ni UDHAIFU wa mawazo, kwa kuwa kuna mamilioni ya vijana ambao wanafanya shughuli nyingine.

TUACHE taaluma ifanye kazi, wakipangwa wakapangika, watu wa kuhitaji bidhaa zao watazifuta ziliko, kama tunavyofuata ndizi mabibo, kama tunavyofuata samaki ferry n.k

Wasalaam
 
16329038065642058018503.jpg
Ni ukweli usio na shaka mahali popote duniani kuwa miji na matumizi ya maeneo katika miji hupangwa. Mipango miji ni TAALUMA na inasomewa. NI ukweli pia usiopingika kuwa kuwa MAZINGIRA ni taaluma, inasomewa pia BIASHARA ni taaluma . Katika manispaa na miji wataalamu hawa wameajiriwa ili kuratibu maendeleo na ukuaji wa miji na majiji. Ni ukweli pia kuwa wamachinga wanafanya shughuli zao kinyume na sheria, na tatizo la wamachinga limetokana na wanasiasa kuingilia taaluma kwa maslahi yao ya kisiasa. Miji ikipangwa vizuri inarahisha shughuli nyingi kufanyika kwa urahisi na kupunguza athari za kiafya ikiwemo kupunguza stress zinazotokana na msongamano, hewa chafu n.k. Fikiria wamachinga wamefika hatua ya kufunga kituo cha daladala pale Congo Kariakoo, Manzese, halafu eti traffic Police anatoka jasho kuongoza magari kutokana na daladala kutokuwa na sehemu ya kushusha abiria Wale mliowahi kufika katika miji iliyopangwa mtakuwa mashahidi kwamba unaweza hata kwenda mahali kama kutalii ndani ya mji kufurahia mandhali, hewa, taaluma ya usanifu n.k Wamachinga wasiondolewe tu maeneo ya watembea kwa miguu, bali vibanda vyao vimekuwa ni UCHAFU unaotia doa kazi ya usanifu wa majengo na barabara. Mfano, fikiria mandhali sehemu katikati ya mji, halafu unakuta kipanda cha mabati, mabox, mbao, n.k. Hata kama hakiko barabarani ni UCHAFU. Hivi vile vibanda vya mabati na mabox nje ya mlimanCity si ni UCHAFU, au ukute kibanda cha viroba pale Ubungo interchange si ni sawa na kutengeza bustani nzuri halafu mtu mtu aanze kutengezea gari ndani ya bustani. Muda ni sasa, elimu ya ujasiliamali itolewe, ubunifu uongezeke, na isiwe kila kijana anafikiria biashara ya umachinga. Hii dhana kuwa watageuka kuwa vibaka ni UDHAIFU wa mawazo, kwa kuwa kuna mamilioni ya vijana ambao wanafanya shughuli nyingine. TUACHE taaluma ifanye kazi, wakipangwa wakapangika, watu wa kuhitaji bidhaa zao watazifuta ziliko, kama tunavyofuata ndizi mabibo, kama tunavyofuata samaki ferry n.k Wasalaam

Back
Top Bottom