Kwanini Wamachinga hawaondolewi 'kiakili' miaka nenda rudi?

The Boss

JF-Expert Member
Aug 18, 2009
49,110
115,885
Kila Mkuu wa mkoa Dar ana kibarua cha wamachinga, why akili huwa haitumiki kabisa?

Toka Marehemu Ditopile Mzuzuri anaongea live kwenye tv DTV kuhusu kuwaondoa wamachinga .hadi Leo mambo ndo yanazidi.

Serikali inashindwaje kufanya hivi kuondoa wamachinga kwa akili.

Agiza wamachinga wote wajiandikishe manispaa. Chukua data zao zote.
  • Wametokea wapi? Mikoa ipi?
  • Bidhaa wanazouza wananunua wapi?
  • Maduka yapi?
  • Mitaji Yao iko kiasi gani?
  • Maeneo wanayouza yana sifa ipi?
Halafu hizi data zifanyiwe kazi.

Kwanza ni Ku identify bidhaa popular za wamachinga na kuangalia kama haiwezekani zikatengenezwa hapa nchini

Halafu kuangalia maduka maarufu wanako nunua hizo bidhaa na kuangalia kama maduka hayo yanaweza kubanwa kwa njia ya leseni. Mfano mtu ana duka la mitumba la jumla asiruhusiwe kumuuzia mtu ambae Hana TIN no, mauzo yote yawe kwenye systems.
Na ambae Hana location maalum ya kuuza bidhaa asiuziwe.

Au zile bidhaa kama makava ya simu na mitumba viwe na leseni yake maalum ambayo sehemu ya masharti ni kuwa na eneo rasmi la biashara.

Serikali ikifanya hivi itajikuta idadi ya wamachinga inayohitaji kuwasaidia ni ndogo kuliko iliyopo sasa

Machinga halisi ni wale wauza mihogo, wapika vyakula n.k. Hawa serikali inawatafutia maeneo wanafanya biashara bila usumbufu manake sio wengi

Lakini wale wenye mitaji ya kukodi fremu lakini hawataki sababu wanaona kuna faida zaidi kutandaza barabarani kuliko kuwa na fremu wale watungiwe sheria za kukwepa Kodi washitakiwe.

Serikali ifanye hili zoezi kiakili kuna wamachinga halisi wa kusaidiwa na kuna wafanyabiashara ambao simply wanakwepa kodi...

Uwepo mfumo wa kukusanya taarifa za kila mmachinga ili kuwachekecha na baadhi ya bidhaa serikali ipige tu marufuku kuingia nchini iwe kichocheo watanzania watengeneze wenyewe. Kuna ulazima wa kukimbizana na wamachinga wanao tandaza makava ya simu barabarani?

Kuhusu mikoa wanayotoka Originally wamachinga walikuwa wauza mitumba barabarani na wengi walitoka mikoa ya kusini hasa wilaya ya mchinga. Ingawa siku hizi wamachinga wanatoka mikoa yote na wapo wengi wenye elimu ya chuo kikuu. Kuchukua data serikali itapata jibu.

Mfano ukigundua kama wamachinga wenye elimu ya chuo kikuu wengi wamesomea taaluma fulani. Mfano sociology, unakaa chini kujiuliza kama kuna ulazima kwa vyuo vyetu kuendelea kutoa graduates wengi wa taaluma hizo ambazo zinazalisha wamachinga.

Kukusanya data kutasaidia sana kujua mambo mengi.
  • Mikoa ipi inazalisha wamachinga?
  • Kwa nini?
  • Shule zipi?
  • Vyuo vipi?
  • Wafanyabiashara wakubwa wanao wakopesha baadhi yao hizo bidhaa.
  • Wanalipia kodi stahiki?
  • Je, Sera za serikali zinazalisha wamachinga? Kodi nyingi kwa bidhaa za ndani na Kodi kidogo kwa wanao agiza?

Hili suala la wamachinga Hadi aje mtu wa kuli-solve kiakili vinginevyo kila Mkuu wa mkoa Dar na mikoa mingine kibarua hiki kinawasubiri.
 
Hizo maneno ndio zitafanya waondoke mjini kwenye maeneo yasiyoruhusiwa?

Wakati mwingine wabongo huelewa kwa njia hii 👇

2952362_Q0f.jpg
 
Hakuna mfanyabiashara mwenye akili timamu atakataa kumuuzia mtu kisa tin no.

Zaidi atahamishia mali zake godown ambapo wewe huwezu fika atawauzia huko.

Siku unataka alipe kodi atakwambia mauzo yameshuka simply hajauza kwasababu wateja hawana tin no.

Dawa ya machinga ni kutumia sheria kali waondolewe.

Jiwe alifuga kansa kama hii.
 
Wafanyabiashara wakibanwa vizuri hawatawauzia trust me.

Mtu anyang'anywe Hadi kibali cha kuagiza hizo bidhaa lazima ataacha tu.
 
Mtoamada! Nimependa hii ndio mana nina wazo kwamba hili suala likifanyika hivi miez 3 mbele watatulia lakin haifiki mi5 watarudi tena barabarani. Mbaya zaid wakijenga masoko nani ana uhakika waliojengew hayo masoko watapata!? Utakut mwanajeshi mmoja kachukua vizimba 7 kaajir wat ambao ukiwakagua utakuta kweli wamachinga
 
Wataleta maembe, machungwa na hata nazi ikibidi. Wengine bila kutembea tembea na vitu vya kubeba maisha hayajawa kamili. ila wengine ni kweli wanatafuta riziki
 
Ushajiuliza kama kweli mamlaka hazijui idadi ya wahitimu waliotoka vyuoni ambao hawajapata ajira rasmi kuanzia 2015 hadi leo mpaka wawafuate mtaani kujua idadi yao? Mbona kuna marejesho ya mkopo kwa waliopata?

Kunahitajika sensa kweli kujua idadi ya hao waliofunga mizigo yao na kuwapa vijana wazunguke nayo mitaani ambapo unaona kabisa mtu kapanga majora ya vitambaa, madftari na vitabu mfano wa stationery, vinywaji kama bia, pombe kali na wines kisha kaweka meza naye pia ni mmachinga? Kwanza mmachinga ni mtu wa bidhaa za mtaji wa thamani gani?

Angalia maeneo waliyotengewa baadhi yao wamekuja kabisa na magari yao binafsi wapepark wanajenga vibanda je hao pia tuwaite wamachinga?

Mwisho wa siku yatakuja yaleyale ya machinga complex. Ukipata majibu ya maswali haya kisha rudi usome mada yako kama inabeba uhalisia.
 
By the way, bado wanalipia vile vitambulisho vyao? walivitumia vile kuweka biashara kila maeneo. Ingawa nahisi kama wangetumia busara, hata kwa vile vitambulisho, wangeweza kupangwa vizuri na kulindwa na interest zao
 
Ushajiuliza kama kweli mamlaka hazijui idadi ya wahitimu waliotoka vyuoni ambao hawajapata ajira rasmi kuanzia 2015 hadi leo mpaka wawafuate mtaani kujua idadi yao? Mbona kuna marejesho ya mkopo kwa waliopata?

Kunahitajika sensa kweli kujua idadi ya hao waliofunga mizigo yao na kuwapa vijana wazunguke nayo mitaani ambapo unaona kabisa mtu kapanga majora ya vitambaa, madftari na vitabu mfano wa stationery, vinywaji kama bia, pombe kali na wines kisha kaweka meza naye pia ni mmachinga? Kwanza mmachinga ni mtu wa bidhaa za mtaji wa thamani gani?

Angalia maeneo waliyotengewa baadhi yao wamekuja kabisa na magari yao binafsi wapepark wanajenga vibanda je hao pia tuwaite wamachinga?

Mwisho wa siku yatakuja yaleyale ya machinga complex. Ukipata majibu ya maswali haya kisha rudi usome mada yako kama inabeba uhalisia.
Wewe mwenyewe unasema wamachinga wanapaki magari kujenga vibanda

Halafu unajiuliza Mimi kama mada ina uhalisia?

Wakati unaona kabisa nataka serikali iweke data base na wachunguze?

Huoni unakubaliana na Mimi kuna wamachinga wengi sio wamachinga kweli?

Ni wafanyabiashara wasilolipa kodi?
 
Kwa mtazamo wangu umeandika theory ambayo haipo practical.

Unatakiwa ujue tatizo sio wamachinga, tatizo ni ukosefu wa ajira

Naona study case yako imejikita kwa wamachinga/ wauza mihogo (matawi) bila kujua source ya tatizo ( mizizi) ni ukosefu wa ajira kwa vijana.

Namaanisha: hata mtu/kijana aliyekwenda dukani akajipatia bidhaa kidogo auze ili apate commission/faida kidogo aweze kuendesha maisha huwezi kumtenga na wamachinga kwani hana ajira hivyo anajishuhulisha ili aweze kuishi.

Sana sana ni kuwawekea utaratibu kama Mama alivyoelekeza ili waweze kuchangia kiasi kidogo kila siku ili serikali ikusanye mapato kama kwa wafanya biashara wengine.

Nafikiri unatakiwa kudefine mmachinga kwa maana pana zaidi; Think out of the box brother!!!!
 
Nimesema serikali iangalie bidhaa popular za wamachinga kama zote ni za kuagiza nje

Je, hakuna uwezekano wa kutengenezwa ndani hizo bidhaa?

Zikitengenezwa ndani sio ndo ajira?

Kama unafikiri lazima serikali iajiri vijana wote
Wanaotafuta ajira hakuna serikali iliweza Hilo dunia nzima
 
Sehemu zote ambazo machinga wameondolewa ziwe chini ya uangalizi wa JWTZ Kwa kipindi kisichojulikana.Machinga akijichanganya tu inakula kwake mazima. Hapo Ndio tatzo litaisha.vinginevyo michezo itaendelea
 
Data is good for research purposes na maamuzi in the long run

In the Interim.,walau tuanze kufata sheria zilizopo kwanza...tusipofata mji hautakalika

Shida kubwa ilianzia kwa JPM

Otherwise taratibu zinajulikana
 
Wamachinga watapungua kama nchi itakuwa ina viwanda vya kutosha, makampuni makubwa ya kutoa huduma (services) na kilimo na ufugaji wa kibiashara utakaoleta ajira za kutosha lakini siyo kwa hali ya sasa ya kutegemea misaada.
 
Labda tatizo ni vyuo yebo yebo
Kama tunao Vijana wa kuajiriwa
Why hawatoki nje kwenda kuajiriwa?
 
Dawa ni kuhakikisha kuwa sehemu waliyoomdolewa hawarudi tena. Machinga wabaki kuuza vitu nyumba kwa nyumba. Wasiruhusiwe maeneo ya masoko au barabarani.

Kinachokwamisha ni siasa. Rais anaingilia mamlaka ya serikali za mitaa na kusema machinga wapige kazi. Suala la machinga siyo la serikali kuu hata.
 
Back
Top Bottom