SoC02 Acheni kutusimanga sisi wasomi wa Tanzania

Stories of Change - 2022 Competition

Mnyakyusa5000

Member
Sep 21, 2021
61
117
Sio kwa nia mbaya ila ni ukweli kuwa kwa miaka ya hivi karibuni imezuka kasumba ya kila mtu anayetaka hoja zake kuhusu maendeleo zisikilizwe basi lazima awaseme vibaya wasomi wa nchi (Tanzania) na kubeza kabisa mfumo wa elimu yetu.

Kama wasomi hatukatai kukosolewa lakini kwa sasa watu wanafikiri kuwa ni sifa kuwasema vibaya watu ambao kwa uhakika ndio wanaoihudumia nchi hii kupitia taaluma zao na wengine wapo mbioni kufanya hivyo pindi watakapomaliza masomo yao. Kila sehemu, bungeni, vijiweni, makanisani, misikitini, kila mtu hata yule asiyejua kusoma na kuandikwa anajisikia fahari kuwasema vibaya wasomi wa nchi yetu. Hii sio sawa kabisa.

Katika makala hii nitajitahidi kuelezea maana halisi ya msomi ambaye mara zote ndiye anayesimangwa kila siku na watu, kwanini watu huwa wanamsimanga, kwa vipi wanakosea wanapofanya hivyo na ni nini hasa wanachotakiwa kukifanya badala ya kutoa masimango na kuwadharau watu ambao kiukweli ndio waliofanikisha maendeleo ya nchi hii kufika hapa ilipo.

Msomi ni nani?
Kulingana na uelewa wa watu wengi ambao ndio hasa vinara wa kuwabeza wasomi, neno msomi kwao linasimama kwa mtu aliyesomea taaluma fulani kama vile ualimu, afisa mifugo, mipango miji, usimamizi wa fedha, mhasibu n.k.. kwa wengine msomi husimama badala ya mtu mwenye utaalamu wa juu kabisa katika taaluma fulani. Watu kama Hawa mara nyingi hujulikana kama madaktari au maprofesa.

Kwa hivyo mara zote watu hawa wanapobeza kwa kuanza na kauli za kusema 'wasomi wetu' humaanisha watu kati ya hao walioorodheshwa hapo juu.

Kwanini watu huwa wanatusimanga wasomi?
Kuna sababu nyingi sana zinazopelekea watu wa nchi yetu kuwasimanga na kuwasema vibaya wasomi wake lakini kwa maneno machache tunaweza kuzikusanya sababu hizo na kuwa sababu moja kubwa ambayo ni watu wanaoitwa wasomi kushindwa kutimiza matarajio ya watu hawa katika jamii zao.

Watu wa nchi yetu wanatarajia kuwa mara zote msomi awe na majibu sahihi kwa kila aina ya tatizo linalohusiana na taaluma yake. Watu huamini kuwa hali ya kuwa msomi ni tiketi ya kujua kila kitu katika taaluma ya msomi husika.

Watu wa nchi yetu wanatarajia kuwa msomi lazima awe na tabia nzuri, njema na zisizotilwa shaka. Wakati wote msomi anatakiwa kuwa kama malaika. Hatakiwi kukosea. Anatakiwa kuwa mtu wa mfano katika jamii. Anatakiwa kuwa kiongozi hodari na mshauri mwema kwa mambo yanayohusu taaluma yake na mambo mengine yote.

Watu wa nchi yetu wanatarajia kuwa msomi anatakiwa kutokuwa na shida yoyote katika nyanja zote za maisha. Msomi hatakiwi kuwa na shida za kiuchumi, kijamii, kisiasa nk. Wanatarajia kuwa msomi hatakiwi hata kuingia kwenye migogoro ya kifamilia yaani kugombana na hata mke au mume wake.

Matarajio haya ambayo kiukweli ni mzigo mzito kwa mtu yoyote na sio msomi peke yake huongeza presha kwa wasomi hasa kwa sababu hata wengi kati ya wasomi wenyewe huamini katika matarajio yanayofanana na haya.

Matarajio haya yanaposhindwa kutimia ndio kwa ghadhabu watu wanaofikiri kwamba wao ni malaika husimama hata bungeni na kuanza kuwashambulia wasomi. Jambo hili ni kosa kubwa na zifuatazo ni sababu zake.

Kwanini ni makosa makubwa kuwasimanga wasomi wa nchi yetu?
Kuna madhara lukuki ya kuwasimanga na kuwasema vibaya wasomi wa nchi yetu lakini moja kubwa ni presha kubwa tunayoipata sisi wasomi. Presha hii ya kutaka kutimiza kila aina ya matarajio ambayo watu huwa nayo kwetu ndiyo inazidi kutuzika kwenye shimo kubwa la kutoweza kutimiza matarajio hayo kwa watu.

Hakuna haja ya kusemana kwa kashfa pale matarajio waliyonayo watu juu ya wasomi wa nchi yetu yanapokuwa hayatimizwa. Hii ni kwa sababu kiukweli wasomi sio malaika. Ni watu. Watu wanaopitia changamoto ambazo kwanza kila mtu huzipitia. Kitendo cha kuwasimanga ni njia nyingine ya kuwaongezea nafasi ya kufanya makosa zaidi.

Wasomi wengi wamejiingiza kwenye vitendo vya rushwa kwa sababu ya matarajio makubwa ya kufanikiwa kiuchumi kwa wasomi yaliyopandikizwa vichwani mwao tangu wakiwa wadogo.

Wasomi wengi wamejiingiza kwenye mikondo isiyofaa ya siasa za uongo na kweli kwa sababu ya matarajio ya wao kuwa viongozi hodari na wenye mafanikio yaliyopandikizwa vichwani mwao na jamii zao.

Wasomi wengi wameachana na shughuli za ubunifu kwa sababu ya masimango ya kuwa wanajishughulisha na shughuli zisizolipa. Mfano mzuri ni waalimu. Luna waalimu ambao hawana mawazo yoyote ya ubunifu na kazi yao kwa sababu wanasimangwa kuwa ualimu haulipi na hivyo wamejikita kufanya shughuli nyingine.

Nini kinatakiwa kifanyike?
Kama nikivyobainisha hapo awali kuwa hakuna mkamilifu. Kama watu wataacha masimango kwa wasomi kuna nafasi nzuri ya wasomi kufanya mambo makubwa kwaajili ya maendeleo ya nchi yetu.

Wasomi wa nchi yetu ni watu hodari sana hasa katika kipindi hiki. Lakini matarajio makubwa ya watu wa nchi yetu na masimango yanayotokana na matarajio hayo kutotimia yanapelekea uhodari huo kupotea kabisa.

Hata katika nchi zilizoendelea sio wasomi wote ambao wanatimiza matarajio ya jamii zao kwa kiwango kama ambacho watu wa nchi yetu wanakitarajia. Lakini watu wa nchi hizo ni rahimu kwa wasomi wao. Jambo hilo linawafanya wasomi wa nchi izo kufanya mambo makubwa kutokana na utulivu walio nao.

Mkitaka wasomi tufanye mambo makubwa kama wasomi wengine basi mjifunze kutuheshimu na kutupa muda wa kujaribu kufanya kile ambachotinaweza kufanya. Kama mtaendelea kutusimanga basi nasisi tutaendelea kufanya tunavyofanya hii ni kwa sababu hata nyie ambao sio wasomi hakuna lolote la maana mnalofanya zaidi ya lawama.

TUHESHIMIANE.​
 
hakika umesema kwa niaba ya wasomi wengi, ukwel inakatisha tamaa wengi kwa maneno ya dharau kwa wasomi wetu, kura yangu umeipata
 
Back
Top Bottom