Mystery
JF-Expert Member
- Mar 8, 2012
- 15,484
- 30,162
Hilo ndilo swali kubwa ninalojiuliza, ni kwanini hao watendaji wetu wa Serikali, ambao wanafahamika hata Kwa majina, waliotajwa kwenye ripoti ya CAG, kuwa wamefisadi mabilioni ya shilingi za Umma, ni kwanini Rais Samia Suluhu Hassan, hawatengui kwenye nafasi zao, wakati ni yeye mwenyewe ndiye aliyewateua na ni yeye mwenyewe pekee mwenye uwezo wa kuwatengua kwenye hizo nafasi na badala yake anawasihi Kwa unyenyekevu mkubwa, kuwa watupishe??
Ukiangalia kutokana na ripoti ya CAG, ameyataja mashirika ya Umma ambayo yanaitafuna hii nchi bila huruma, ambao wenyeviti wao wa Bodi, wanateuliwa na Rais, ni kwanini Rais hatumii mamlaka aliyo nayo ya kikatiba, kuwatengua wenyeviti hao wa mashirika yanaotuibia hayo mabilioni ya shilingi za pesa za Umma??
Vile vile wakurugenzi wa Halmashuri za wilaya, ambako huko nako, CAG amefichua madudu ya kutisha, jinsi wanavyojipigia hizo pesa, wakurugenzi hao nao, wanateuliwa na Rais, hivi Kwa nini hawatengui kwenye nafasi zao??
Kama Katiba yetu ya nchi inasema kuwa watu wote tuko sawa mbele ya Sheria, ni kwanini Jela zetu zimejaza wafungwa wenye makosa madogo madogo, kama vile wezi wa simu za mkononi, wakati wezi wakubwa wa mabilioni, wakiachwa huru??
Naona hii nchi imekuwa ya kulalamika miaka yote, wananchi tunalalamika maisha yalivyo magumu, kutokana na gharama za maisha kuwa juu Sana na Rais naye mwenye mamlaka ya kuwatengua hao watendaji wa Serikali wabadhirifu naye analalamika!
Hicho ni kitendawili, naomba mwenye kuweza kukitengua hapa JF, anipe jibu