KARLO MWILAPWA
JF-Expert Member
- Apr 10, 2019
- 2,590
- 4,601
Nitaanza na swali kabla ya 'content' ya mada hii na swali langu ni: kuongoza taasisi za Umma au taasisi yoyote inahitaji uzoefu mkubwa au uwezo mkubwa wa kiuongozi?
swali la pili: Je, mtu ambaye hana uzoefu(graduate) hawezi kuongoza Taasisi Kwa mafanikio?
Lengo la mada hii ni kupata mtazamo juu ya kipaji Cha uongozi na uzoefu, kipi kinachohitajika zaidi ili kupata matokeo makubwa katika Taasisi za Umma na pia kumshauri Rais ikimpendeza badala ya kuteua watu wenye uzoefu mkubwa basi awatazame na vijana ambao hawana uzoefu lakini wana vipawa kikubwa Cha uongozi ambavyo vingine vinapotea kutokana na uzoefu.
Uteuzi na utenguzi ni siri ya mteuaji, wengi wa wateuliwaji wanateuliwa wakiwa hawana taarifa za uteuzi wao kabla na vivyo hivyo wanaotumbuliwa wanatumbuliwa bila Umma kujulishwa sababu lakini Kwa mtazamo wa wengi sababu kuu za kutenguliwa ni za utendaji zaidi kama Kushindwa kufikia malengo husika.
Wengi wa wanaoteuliwa kwenye utendaji wa taasisi za Umma ni wenye uzoefu mkubwa lakini pia inashangaza baada ya muda mfupi huyu aliyeteuliwa na CV inaonesha ana uzoefu mkubwa anatumbuliwa au anasimamishwa. Je, ni nini huwa kinawakumba?
Ninatambua uzoefu ni msingi mzuri wa matokeo makubwa ya kiutendaji lakini kujaribu njia nyingine pia ni jambo jema na linaweza kuleta matokeo chanya kwenye utendaji.
Tumshauri Rais ikimpendeza aangalie kwenye uteuzi vijana ambao hawana uzoefu lakini wana kipawa Cha uongozi ' hawa ni watu 'potential' sana na wanaweza kusaidia kuleta matokeo makubwa Kwa sababu:
i. Vijana wanapoaminiwa kuongoza taasisi watatumia Kila mbinu kusaidia taasisi kukua Kwa sababu ndani ya ufahamu wao wataamini matokeo ndio yatakayowabeba
ii. Vijana ni watu wa matokeo, watapambana kufanikisha matokeo na 'spirit' ya kutaka matokeo itasaidia kuleta ufanisi ndani ya Taasisi husika. Mfano ni makonda
iii. Vijana wana uthubutu na utayari wa kujaribu mawazo mapya ili kuona matokeo makubwa.
iv. Mtazamo wa vijana kwenye mambo mengi ni wa kileo na kisasa, mabadiliko mengine yanakuja Kwa kuendana na usasa. Vijana watakuja na mbinu na mikakati ya kisasa.
Kwa kuwa lengo la mada hii ni ushauri Kwa Rais wetu, Kwa namna ya pekee kabisa namshauri Rais aangalie vijana wenye utayari na kipwa Cha uongozi na sio lazima awe na uzoefu mkubwa kwenye nafasi ya Kamishna wa NCAA , naamini mtu wa namna hii atatusaidia kukuza utalii na kuongeza mapato na fedha za kigeni.