mbingunikwetu
JF-Expert Member
- Feb 17, 2015
- 13,663
- 18,037
Hii imekaaje? Waliosomea nyanja ya mifugo, misitu, kilimo, uuguzi, nk katika ngazi ya shahada na kuendelea hutambuliwa kama maafisa katika nyanja zao kama vile afisa mifugo, afisa misitu, afisa kilimo, afisa uuguzi nk, na jamii kukubali kuwa wanastahili kutunukiwa uafisa katika maeneo yao ya utaalamu.
Linapokuja suala la waliosomea nyanja ya ELIMU katika ngazi ya shahada ikaonekana HAWASTAHILI KUITWA MAAFISA katika eneo lao la utaalamu!! Waitwe tu waalimu!
Hapo awali walikuwa wanaitwa maafisa elimu, lakini WAKAFUTIWA hadhi hiyo ya uafisa!! Sielewi kitu gani kinafanya walimu wabaguliwe hivyo kwa wazi kabisa!
Hii ni dharau kubwa kwa wataalamu wetu wa elimu, halafu watu wanashangaa kwa nini elimu yetu inashuka!