SoC03 Mabadiliko ya matumizi ya kutoka nishati chafu hadi nishati safi kwa kutumia zao la mtama

Stories of Change - 2023 Competition

Hadassah ciara

New Member
Jul 4, 2023
1
1
YALIYOMO
1.0.KICHWA
2.0. UTANGULIZI
2.1. Jinsi gani BINADAMU anachangia kuharibu mazingira kwenye matumizi ya nishatii
nchini
2.1. maelezo mafupi kuhusu zao la mama Tanzania, Africa Mashariki na duniani kote
2.2Jinsi gani BINADAMU anachangia kuharibu mazingira kwenye matumizi ya nishati
3.0 MADA KUU;ZAO LA MTAMA KAMA CHACHU YA MABADILIKO.
3.1.kwa Nini kipaumbele kipewe mtama kama zao litakaloleta mabadiliko katika matumizi ya nishati mbadala?
3.2. mapendekezo jinsi gani mtama unaweza kutoa nishati mbadala Kwa jina rahisi ambayo itachochea utunzaji wa mazingira.
3..3. Ni Kwa jinsi gani MABADILIKO ya matumizi ya nishati mbadala yatachochea UWAJIBIKAJI
4.0. HITIMISHO


UTANGULIZI
Duniani kote kutia ndani nchi yetu ya Tanzania kumekuwawa ujarbifu wa uoto wa asili kwa ajili ya matumizi mbalimbali kama vile uanzishwaji wa viwanda,ujenzi miundo mbinu kma vile barabara reli migodi nk .
UKATAJI MITI kwa ajili ya matumizi ya nishati nchini Tanzania limekuwa TATIZO kubwa.kwani miti inapungua kw kazi kubwa sana kutokana na ongezeko la watu.

Hii ni Kwa sababu watanzania wengi ni watu wa kipato cha chini Kuni na mkaa ndo chanzo rahisi Cha nishati Kwa familia nyingi Tanzania matumizi ya umeme Tanzania Kwa ajili ya kupikia ni asilimia Tano,3% na gesi ni asilimia 5%.

Mpaka Sasa hivi uharibifu wa mazingira Kwa ajili ya kupata nishatii ya kupikia ni mkubwa na matokeo yake mabaya yanaonekana wazima sehemu mbalimbali za nchi kwa mifano miwili tu
Sehemu nyingi Tanzania wanawake hasa hulazimika kusafiri umbali mrefu ili kutafuta kuni.

Mbaya zaidi mikoa ya kati kama vile Dodoma na Singida wananchi wa kipato cha chini wnalazimika kupikia nishati itokanayo na kinyesi cha punda na ngombe.matokeo yake kiafya yanaweza kuwa hatari sana.
Hivyo basi; Ikiwa MABADILIKO madhubuti ya matumizi nishati safi ya kupikia hayatafanyika haraka, HATARI NI KIBWA SANA mbele yetu
Tunahitaji kubadili haraka matumizi ya nishati hasa ya kupikia kabla Hali haizijawa mbaya hata zaidi.

Mabadiliko yanaweza kuwa katika nyanja tofauti ikutia ndani kwenye hili zao la MTAMA (sweet sorghum bicolor) ambao unaweza kutokeza nishati safi ya kupikia.

HILI LINAWEZEKANAJE?
MTAMA si zao geni miongoni mwa jamii nyingi za watanzania,nchini Tanzania mtama hulimwa karibu Kila kona ya Tanzania ingawa si zao ambalo limepewa kipaumbele kama mazao mengine husuani mahindi lakini halina kipaumbele katika sehemu yoyote isipokuwa kama chakula cha binadamu..tunapaswankutilia ukkulima wa zao la Mtama
Nci nyingi duniani kutia ndani marekani Brazil india Nigeria zao la MTAMA hulimwa sana zao la ambapo Huwa na matumizi mengi kutia ndani chakula Cha mifugo kutokeza suka,pamoja na gesi safi ya kupikia.

Kwa kuongezeasababu zinazofanya gesi ya ethanol ambayo kutengenezwa Kwa wingi nchini Brazil kutokana na zao la miwani Hali ya hewa upatikanaji wa ardhi ya kilimo na wafanyakazi wapi wa kutosh pia serikali imetoa kipaumbele kikuu cha matumizi ya gesi safi ya ethanol kwenye viwanda magarina matumizi ya nyumbani,kupikia.(Ethanol fuel in Brazil - Wikipedia).

2.0. MADA KUU
2.1. Kwa nini kipaumbele kipewe MTAMA kama zao litakaloleta mabadiliko kwenye matumizi ya nishati mbadala
Hapa tunazingumzia mbegu ya MTAMA ambayo inaweza kutokeza juisi ya miwa tamu Kwa lugha ya kiingereza inaitwa Sweet sorghum bicolor.
Sababu zinazoweza kufanya zao la MTAMA liwe rahisi kuleta mabadiliko katoka matumizi ya nishati ya kupikia Tanzania hususani VIJIJINI ambako ndio chanzo cha ukataji miti ni kama zifuatazo.

-kijiografia Hali ya hewa ya tanzania (tropical)inafanana kw ukaribu na Brazil na MTAMA ni zao linaloweza kulimwa karibu SEHEMU yoyote Tanzania Kwa sababu ya kiwango cha joto tanzania (27na29 maeneo ya pwani na 20 na 30 maeneoo ya kati a, kusini mwa tanzania)
Hukomaa wa muda mfupi, kuanzia siku 90-120
Vilevile MTAMA hukubaliana na karibu aina zote za udongo, (mfinyanzi tifutifu na kichanga
NA isitoshe unaweza kulimwa pia hata sehemu uhaba wa mvua.,
MTAMA hauhitaji gharama kubwa sana kwenye utunzaji zao lkiwa shamban yaani matumizi ya mbolea, wadudu waharibifu na palizi ya mara Kwa mara
Mbali na matumizi ya chakula Cha binadamu na mifugo. unaweza kutokeza NISHATI YA KUPIKIA
Kuna mbegu ya kienyeji na za kisasa, zinazotoa juisi tamu ,Ikiwa zitatuzwa vizuri na Kwa utaalamu zaidi hotoa mavuno mengi.

Juisi inayovunwa kutokana na hii mbegu ya kisasa hutokeza kati ya galoni 400-800 za gesi ya ethanol Kwa ekari ambazo ni sawasawa na kama Lita -1800-3600 hivi za ethanol (galoni Moja ni kamaLita nne na nusu hivi) Sweet Sorghum Research | Department of Agronomy and Horticulture | Nebraska
Jambo kuu HAPA si wingi wa mavuno ila kumbe inawezekana kutokeza NISHATI kupitia MTAMA wa miwa (sweet sorghum bicolor).

Kuna mbegu za MTAMA ambazo hulimwa Kwa ajili ya kutokeza juisi tamu ambayo ikichachishwa(fermentation) inaweza kutokeza gesi ya ethanol Kwa wingi hivyo ikatumika kama chazo cha NISHATI kwa ajili ya kupikia

3.2. MAPENDEKEZO
Yafuatayo ni mapendekezo ya nini kifanyike ili kuleta mabadiliko ya matumizi ya nishati kutoka kwenye Kuni na mkaa Hadi kwenye gesi ya ETHANOL
KWANZA Napenda niipongeze serikali ya mama Samia Suluhu Hassan kupitia WIZARA YA NISHATI Kwa mipango kubadili matumizi ya kupikia kutoka Kuni na mkaa na kuwa ya ya gesi safi .(gazeti (Nishati | News)
PILI; Kama Kuna TAFITI zinazofanywa na ASASI mbalimbali za KILIMO nchini kuhusu zao la MTAMA wa miwa,basi zisilenge WIZARA tu ya Moja tu ya kilimo au nishati,Bali matokeo yake yanapaswa kufanyiwa kazi Kwa vitendo.yaani kugawa majukumu pia Kwa WIZARA tofautitofauti jinai gani?
SERIKALI kupitia sera na mipango inapaswa kuhusisha wizara zifuatazo;

Wizara za FEDHA NA UCHUMI, NISHATI, AFYA, KILIMO NA CHAKULA na ELIMU
Kwa mifano michache ifuatayo,mapendekezo yanaweza kufanyika kama serikiali itaona ni vyema,na ni kama ifuatavyo;

WIZARA YA FEDHA NA UCHUMI; Kwa kuwa ambo hili ni nyeti sana na linahitaji FEDHA hivyo, wizara hii inapaswa kuwa ndo mama wa wizara zotena inapaswa kufanya yafuatayo:

Kubuni sera zitakazoifanya serikali kutenga pesa za wizara tajwa hapo juu ili pesa hizo ziwe maalumu Kwa ajili ya kutekeleza mipango yote ya upatikanaji wa gesi inayotokana na juisi ya MTAMA.

WIZARA YA NISHATI; Tayari mikakati imeshaanza kuhusu kubadili matumizi ya nishati ya kupikia kutoka Kuni mkaa mabakii ya mimea na vinyesi vya wanyama (ambavyo hutokeza gesi chafu na kuharibu mazingira na afya za watumiaji)na kuingia kwenye nishati safi na mbadala,muhimu sana Kwa wizara hii ni kuongezea mbinu na mikakati zaidi ili kuona mabadiliko hayo yanafanywa Kwa vitendo, mathalani
Kuhakikisha ELIMU ya matumizi ya gesi itokanayo na MTAMA Inatiliwa mkazo zaidi si Kwa kuishia kuwapa ELIMU wabunge tu.

(https://www.nishati.go.tz/news/wabunge-wapata-elimu-ya-nishati-safi-ya-kupikia)Bali ELIMU inapaswa kuanzia ngazi ya chini ambako ndo walengwa wakuu.

Sambamba na hilo wizara inapaswa kuhakikisha sera zote khusu matumizi ya fedha katika kushughulikia gesi safi ya ETHANOL inayotokana na MTAMA zinatumika kama ilivyopangwa kwenye WIZARA nyingine zitakazohusika.

WIZARA YA VIWANDA;itungwe sheria ya uwekezajiu iwe wa ndani (local) au nje ambapo mwekezaje Kwa lazima l kama ikiwezekana kwenye uwekezaji wake unatumia nishati basinasilimia fulani iwe ni kutoka nishati safi na mbadala kutia ndani gesi ya ethanol itokanayo na MTAMA.

Kwa kuongezea ruzuku itolewe Kwa viwanda vitakavyojitolea kutengeneza majiko ya kupikia yanayotumia gesi ya ETHANOL na wananchi wauziwe kwa bei rahisi ikiwa ni pamoja na kutoa motisha Kwa wakulima(kuuziwa majiko Kwa mkopo ruzuku au zawadi Kwa atayejitahidi kufikia lengo na
WIZARA YA ELIMU sambamba na hilo elimu itolewe ngazi ya familia matumizi sahihi na faida za nishati mbadala(ili kuifikia jamii Kwa uharaka labda ianzie na semina Kwa walimu wachache na wao watoe maelekezo Kwa walimu wenzao mashuleni kwao na walimu iwe kama routine Kila siku watoe elimu Kwa vitendo Kwa wanafunzi ambao Kila siku kabla ya kuanza vipindi vya kawaida wachache waweza kuulizwa walisema Nini Kwa wazazi wao nyumbani.

Kwenye WIZARA YA KILIMO; itungwe sheria kwamba mojawapo ya masharrti ya kupata mbolea ya ruzuku ni lazima mkulima aoneshe Kwa maelezo na vitendo kutia ndani kusaini mkaatba wa utelelezaji kwamba atalima zao la Mtama angalau nusu ekari,hii itasaisia kutokeza miwa Kwa wingi kama malighafi Kwa ajili ya kutengeneza nishati safi ya ethanol.

Pia wizara ya kilimo kuhakikisha wanatafuta soko la miwa ya MTAMA Kupitia maafisa ugavi ;wanapaswa wapewe jukumu la kuhakikisha wanagawa au kuuza mbegu Bora ya MTAMA kutoka serikalini (inaweza ikafanywa Kam ilivyokuwa kwenye ALIZETI mwaka 2021/2022),
Kwa miwa itakayoatikana Kwa wakulima wadogowadogo na wakubwa pia,serikali ihakikishe inajenga vituo vya kuchakata juice ya miwa hata ikiwezekana Kila kata ili wanachi na Kila Mkulima aweze kupata soko la miwa yake. (Kuna mbegu za MTAMA zinazoweza kutokeza juisi tamu na na Kwa wingi kama vike BRS 508,509 na 511).

(https://www.sciencedirect.com/science/article/abs/pii/S0960148114002845)

Kile kinachoweza kufanyika kwenye WIZARA YA AFYA ni kama tu ambavyo serikali inagawia wajawazito na watoto vyandarua Madaktari na manesi wanaoshughulikia mama wajawazito wapewe semina elekezi na Kwa kuendelelea jinsi ya matumizi ya gesichafu yanavyoweza kuathiri afya zao ,za watoto wakiwa tumboni watoto wao wakubwa na familia nzima i najinsi gesi mbadala na safi kuboesha afya ya mama na mtoto, na familia nzima.

WIZARA inapaswa iangalie jambo hili liwe endelevu.
Kwa kujumuisha serkiali inapofanya teuzi mbalibali mojawaponya kupima kiongozi Bora ni kuangalia yule ambaye ama amefanya Nini katika kuchochea kutunza mazingira au atafanya nini atakapokuwa kiongozi kuhusu kutekeleza matumizi sahihi ya nishati mbadala hii itachochea utawala bora na uwajibikaji.

Wale viongozi Wazembe wanapaswa kushughulikiwa kulingana na masharrti ya utelelezaji waliyopangiwa.,hili kinaweza kuchochea UWAJIBIKAJI.

Kwa kuongezea sehemu zozote watu wanapokusanyika iwe kanisani au msikitini viongozi wa dini kwenye mahubiri Yao wasisitize matumizi sahihi ya gesi ya ethanol itokanayo na MTAMA

Vyombo vya usafiri kama vile Basi Ndege Meli na Garimoshi yawekwe matangazo jinsi ya kukabiliana na uchafuzi wa mazingira pamoja na matumizi sahihi ya gesi mbadala.

HITIMISHO
Sote tunafahamu kuwa si rahisi sana kufanya mabadiliko katika jamii ambayo vizazi na vizazi wana mazoea ya kufanya jambo fulani lakini Kila mmoja wetu Kwa sehemu yake awajibike, kuanzia ngazi ya familia hata viongozi wa juu kabisa Kwa kujitoa kabisa kivimilia
KUKIRI
MADILIKO YA MAGEUZI YA MATUMIZI YA NISHATI SAFI ILI KICHOCHEA UWAJIBIKAJI YAANZE NA MIMI.

ASANTE

REJEO/DONDOO
 
Back
Top Bottom