Waliosoma fani za kilimo na mifugo na Jinsi walivyotumia elimu zao mpaka sasa kujikomboa binafsi na kuleta mapinduzi kwenye sekta ya kilimo na mifugo

Binafsi wahitimu wa Kilimo na Mifugo naona kama haitendei haki nchi. Wanamaliza vyuo wengi wao hata kutengeneza tuta la mchicha wanazidiwa na wale wamama wanaozalisha mchicha Bonde la Msimbazi na pale Nyuma ya urafiki Dar. Ukimpeleka shamba ni shida kwa walio wengi.
Hatari kubwa hiyo
 
Certificate of general agriculture, mwajiriwa duka la pembejeo, maisha ni changamoto kwa wenye fani hii hasa ukizingatia ajira za kuajiriwa hakuna. Miaka mitano sasa tangu nimalize chuo usihofu sana kijana mwenzangu just prepare well your plans and commit yourself to complete them!

Sent using Jamii Forums mobile app
Diploma in General Agriculture Niko zangu bandari nabeba mizigo(ila sio kuli) tafuteni Jina lingine zuri zuri kidogo. Kama Wale wanaobeba mizuho kupandisha milimani wanaitwa porters
 
Kuna siku Spika wa Bunge akasema "nawazaga tu endapo siku moja wizara ya kilimo na wafanyakazi wake wote wakatolea hata kwa kipindi cha mwaka mmoja tu ivi kutakua na tofauti kweli kweny uzalishaji kweny nchi hiii"

Nilicheka sana, maana mimwenyew sioni umuhimu wa watu wakilimo hasa vijijin. Wa maofis makubwa nao wanachelewa kulipana per diem tu... wanajifanya utafiti tafiti zenyew miaka 10 hazileti matunda yoyote.
Ikiwa wataalamu wa kilimo hawana umuhimu,mbona kukitokea mlipuko wa magonjwa km vile Sumu kuvu kwenye mazao au wadudu km vile Viwavi jeshi vamizi huwa mnawasumbua wataalamu wa kilimo kuwa wasaidie kutatua changamoto hiyo?,

Kunapotokea mabadiliko ya hewa hata kutishia upungufu wa chakula kwanini huwa mnawabwatukia wataalamu wa kilimo kuwa wazalishe mbegu zinazovumia Ukame au mbegu stahimilivu,si mzalishe wenyewe?.Kukitokea shida kwenye Ufanisi wa Ubora wa Viuatilifu au mbolea mbona huwa mnatoa maagizo kibao kuwa Wataalamu Wa kilimo wachunguze,si mchunguze wenyewe?.

Ikiwa hawana mchango wowote ktk Jamii Serikali inawaajiri wa nini sasa,si waache?.Jamani mnyonge mnyongeni,haki yake mpatieni".
 
Je unahitaji kulima mahindi na hauna muda wa kusimamia? Au unataka upate mavuno mengi zaidi? Njoo ofisini kwetu.

Ofisi ya YAD yenye wataalamu wabobezi wa kilimo sasa inakuletea mpango wa kusimamia shughuli zote za shambani. Mkulima utatukabidhi shughuli zako pale shambani kwako sisi tutafanya kila kitu kwa utaalamu zaidi na kukukabidhi mazao yako yakiwa yamekomaa. Gharama zetu ni nafuu sana na tunakuhakikishia kwa ekari moja kuvuna mahindi zaidi ya gunia 30. Usihangaike sasa, sisi tupo kwa ajili yako, Kwa Wale ambao hawana mashamba tutakuwezesha kupata mashamba ya kukodi kwa elfu 40 tu na mashamba ya kununua kwa elfu 60 tu hata ukihitaji ekari 100 za kununua utazipata kwa bei hiyo hiyo.

Kwa maelezo zaidi fika ofisini kwetu.
Jengo la NSSF SONGEA
Ghorofa ya 3 chumba no. 317
Simu. 0621133117
 
Back
Top Bottom