SoC02 Mkakati wa Kukuza na Kuendeleza Sekta ya Kilimo

Stories of Change - 2022 Competition
Aug 18, 2022
11
4
Kilimo ni sayansi inayohusisha kulima mimea na mifugo. Kilimo ni moja kati ya shughuli za kwanza kabisa kufanywa na binadamu katika harakati za kujitafutia chakula.

Mazao ya kilimo yanaweza kugawanywa katika makundi ya vyakula, nyuzinyuzi, mafuta na malighafi kwa ajili ya shughuli za viwanda.

Pia mazao ya kilimo ni pamoja na nafaka, mboga mboga, matunda, mafuta, nyama, maziwa, mayai pamoja na kuvu.

Tangu kuanzishwa kwake kilimo kimepitia mabadiliko na mapinduzi makubwa kulingana na wakati husika na mahitaji ya jamii husika. Lengo kuu la kilimo, bila kujali aina yake na namna yake ya kufanya kazi, ni kuzalisha chakula kutokana na mimea pamoja na mifugo.

Nchini Tanzania kilimo kilianza kabla ya wakati wa ukoloni, kikaendelezwa wakati wa ukoloni na mpaka sasa kilipofikia kuwa uti wa mgongo wa taifa letu. Kwani zaidi ya 50% ya uchumi wetu unategemea ufanisi wa kilimo.

Tangu uongozi wa awamu ya kwanza mpaka sasa awamu ya sita, juhudi mbalimbali zimefanyika katika kukuza, kuboresha na kuendeleza kilimo cha Tanzania. Juhudi zote izo zimechangia kwa asilimia fulani maboresho katika kilimo nchini.

Lengo mahususi la makala hii ni kwenda kuchochea mabadiliko chanya katika sekta ya kilimo hivyo kuleta faida kubwa na endelevu katika shughuli nzima ya kuzalisha chakula kutokana na mazao ya mimea kama vile viazi, mpunga, alizeti, mtama, uwele, mahindi, ngano, mbaazi na mihogo. Ikijumuisha na mazao ya wanyama kama vile maziwa, nyama, mbolea, mayai, ngozi na samaki.

Mosi, kutumia mapinduzi ya kisayansi na teknolojia katika kukuza, kuboresha na kuendeleza kilimo. Tupo katika karne ya 21 ikiongozwa na upatikanaji mkubwa wa taarifa mbalimbali (information age). Na kilimo kama sekta nyingine haiwezi kujitenga kwa maendeleo haya. Hivyo haina budi kutumia mapinduzi haya ya sayansi na teknolojia katika kuongeza tija na kuzalisha kwa manufaa zaidi na gharama ndogo zaidi.

Tuachane na kilimo cha jembe la mkono na sasa tulime kwa njia za kisasa zaidi zilizoletwa na mapinduzi haya ya sayansi na teknolojia katika ulimwengu wetu wa sasa. Mapinduzi kama kilimo cha umwagiliaji, utumiaji wa mashine mbalimbali katika kilimo na uhandisi wa vinasaba kwa wanyama unaweza kusaidia kuboresha hali ya sasa ya kilimo na kuwa bora zaidi.

Pili, kwa serikali kupitia wizara ya ardhi na kilimo, kupima ardhi na kurasimisha maeneo maalumu kwa ajili ya shughuli za kilimo cha mazao mbalimbali na mifugo. Hii ni kutokana na sababu kwamba shughuli nyingi za kilimo hapa nchini zinaendeshwa kwa mfumo usio rasmi wa maeneo ya ardhi.

Hatua hii pia itasaidia kuepusha migogoro ya maeneo ya kilimo na shughuli nyingine za kijamii kama vile ujenzi na usafirishaji. Hii iendane sambamba na kuachana na matumizi yasiyo sahihi ya ardhi yanayodunisha ubora wa sekta ya kilimo na sekta zingine.

Tatu, utafiti wa kilimo (agricultural research). Pia ili kuchochea mabadiliko chanya katika kilimo hapa nchini ni vyema kufanyike utafiti wa kina juu ya njia mbalimbali za kilimo katika uzalishaji wa nafaka na mazao ya wanyama.

Hii itasaidia upatikanaji wa mbegu bora na za kisasa zenye sifa madhubuti katika kuboresha kilimo. Pia utafiti huu utasaidia kukuza sekta zingine zinazotegemea kilimo kwa namna moja au nyingine hivyo kukuza ufanisi wake.

Nne, serikali kuendelea kutoa ruzuku kwa wakulima nchini hasa wakulima wa hali ya chini ambao ni wengi. Mfano kwa kipindi hiki kinachoendelea serikali imetoa ruzuku ya zaidi ya shilingi bilioni 100 kwa ajili ya kupunguza bei ya mbolea ambayo ni nyenzo kuu katika kilimo.

Muendelezo wa hatua hizi na zingine zitawasaidia wakulima wengi wa chini ambao hawana uwezo wa kuzalisha kwa kiwango kikubwa na kuanza kuzalisha kwa tija na mkakati hivyo kuboresha uzalishaji wa mazao ya kilimo. Pia, ni muhimu kwa serikali kuongeza bajeti ya kilimo kwani itaongeza wigo mpana na ufanisi zaidi katika shughuli zote za kilimo hapa nchini.

Tano, Zianzishwe asasi, mifuko na benki maalumu za maendeleo ya kilimo. Hatua hii inajumuisha kuzipa nguvu na uwezo zaidi asasi, mifuko na benki za kilimo. Hii itaongeza tija na ufanisi katika kuzalisha mazao ya kilimo (kilimo biashara).

Pia ziundwe sheria, sera, taratibu na miongozo maalumu katika uendeshaji wa taasisi hizi ili ziweze kufanya kazi zao kwa ubora na unafuu zaidi. Pia elimu zaidi iendelee kutolewa kwa wakulima juu ya namna sahihi, bora na za kisasa katika uendeshaji wa kilimo chenye tija kwa maendeleo ya mkulima mmoja mmoja, jamii na taifa kwa ujumla wake.

Sita, watanzania tubadili mitazamo yetu juu ya kilimo. Imekuwa kawaida kwa watanzania wengi kuamini kwamba kilimo ni kwa ajili ya watu maskini na walioshindwa. Mtazamo huu ubadilishwe na kuwa kilimo ni biashara na ajira.

Hii itaongeza hamasa zaidi kwa watu wengi kuingia na kuendeleza kilimo hapa kwetu Tanzania. Hatua hii ni muhimu katika kukuza ubora na ufanisi wa kilimo hivyo kuongeza mchango wa kilimo chetu katika uchumi wa taifa. Mtazamo kwa sasa uwe kilimo ni biashara na ujasiriamali kilimoni.

Saba, kilimo cha umwagiliaji na kilimo hai (irrigation and organic agriculture). Tupo katika wakati ama nyakati zenye changamoto kubwa za hali ya hewa kama vile ukame na uhaba wa mvua kwa baadhi ya maeneo. Pia tunaishi nyakati ambazo magonjwa yamekua ni mengi. Hii inalazimu mabadiliko chanya na endelevu katika kilimo kama sekta pekee ya kuzalisha chakula.

Hii ni kwa kufanya kilimo cha umwagiliaji ambacho hakitegemei mvua. Pia kilimo hai kifanyike kwa kiwango kikubwa kwani faida zake ni nyingi sio kiafya tu bali hata kimazingira.

Hitimisho; Makala hii inahitimisha kwamba ni muhimu kuchukua hatua za makusudi zenye malengo katika kuboresha kilimo na ufugaji kama zilivyoainishwa hapo juu. Hii itachochea mabadiliko chanya katika sekta ya kilimo ambayo ina mchango mkubwa katika uchumi wa Tanzania. Kwani nchini Tanzania, sekta ya kilimo ni muhimili wa maendeleo ya uchumi.

Sekta hii inachangia kiasi cha nusu ya pato la Taifa, robo tatu ya bidhaa zinazouzwa nje ya nchi na chanzo cha chakula pamoja na utoaji wa fursa za ajira zaidi ya 65% ya watanzania. Kilimo kina uhusiano na sekta zisizo kuwa za kilimo kupitia uhusiano wa usafishaji kwenda kwenye usindikaji wa mazao ya kilimo, matumizi na uuzaji wa mazao ya kilimo nchi za nje, inatoa malighafi kwa viwanda na soko kwa bidhaa zilizotengenezwa.
 
Kwa ajili ya WATOTO wao wenye nguvu na wachawi sana kuelewa SEKTA YA KUPAMBANA… Taasisi za UMOJA WA MATAIFA UN {ILO, UNHCR, FAO} inampango wa kuleta matrekta 70,000 na utengenezaji wa matrekta zaidi ya 10,000 NCHINI TANZANIA kwa ajili ya kusaidia shughuli za kilimo.. Tunaomba mwananchi wa JF TOA MAONI nani apewe hayo matrekta pamoja na fedha za mkopo kutoka INDIA RUPEES MIL 78 kuboresha sekta ya kilimo ambayo wanasemaga ni kimbilio kwa zaidi ya asilimia 67% ya watanzania.

TALI

TARI Homepage

SUMA JKT

Kilimo, Ufugaji na Uvuvi

KAMPUNI BINAFSI

Kilimo

CHUO CHA SUA

Welcome to Sokoine University of Agriculture (SUA)
 
Back
Top Bottom