SoC03 Nguvu zaidi iwekezwe kwenye kilimo

Stories of Change - 2023 Competition

Moto mingi

Member
Jun 13, 2023
7
6
Maana ya neno kilimo
Kilimo ni shughuli muhimu ya uzalishaji wa mazao ya chakula na biashara.
Huu ni mchango mkubwa kwa jamii ya Tanzania kwa sababu zaidi ya asilimia 75 ya ajira zote zinategemea kilimo na zaidi ya asilimia 50 ya Pato la taifa hutokana na sekta hii ( kwa mujibu wa tovuti kuu ya serikali iliyochapishwa mwaka 2021 . Tovuti Kuu ya Serikali | Kilimo )

Kilimo kilianzaje kukua nchini?
Historia ya kilimo nchini Tanzania inaonesha kuwa, kabla ya wakoloni kuingia nchini, wakazi wa zamani wa Tanzania walikuwa wakilima mazao mbalimbali kwa ajili ya matumizi yao ya kila siku. Baadaye wakulima wa Tanzania walijiunga na mfumo wa kiuchumi wa kikoloni ambao ulikuwa ukilenga zaidi kuvuna mazao ya kibiashara kama vile pamba, kahawa, tumbaku, chai na korosho, ambapo mfumo huu ulianzishwa mwaka 1884 Hadi 1919 na wajerumani na baadae kuendeleza na waingereza kutoka 1919 mpaka 1961 nchi yetu ya Tanzania ilipo pata Uhuru wake.

Hata hivyo, baada ya uhuru wa Tanzania mwaka 1961, kulikuwa na jitihada za kuanzisha utaratibu wa kuboresha kilimo nchini. Serikali ilitambua nafasi na umuhimu wa kilimo kwa maendeleo ya uchumi na ustawi wa kijamii ya kitanzania kwani maendeleo haya yangewalenga watanzania na si kama mfumo wa unyonyaji wa kuwanufaisha wakoloni.

Nini umuhimu wa sekta ya kilimo nchini Tanzania

Katika maeneo mbalimbali nchini Tanzania, watu hujihusisha na kilimo kwa ajili ya kujipatia kipato, kuzalisha chakula cha kutosha na kusaidia katika utengenezaji wa bidhaa mbalimbali. Sekta ya kilimo ni muhimu sana kwa maendeleo ya uchumi wa Tanzania. Kwa mujibu wa takwimu za hivi karibuni za Benki Kuu ya Tanzania (BoT), sekta ya kilimo inachangia zaidi ya asilimia 25 ya Pato la Taifa na zaidi ya asilimia 65 ya ajira nchini. Hii inafanya sekta ya kilimo kuwa nguzo muhimu ya uchumi wa Tanzania.

Mbali na hilo, kilimo pia ni chanzo kikubwa cha malighafi kwa viwanda vingi vya ndani na nje ya nchi. Kwa mfano, Tanzania ni mojawapo ya nchi zinazozalisha mazao mengi ya biashara ikiwemo pamba, kahawa, chai, tumbaku na karanga ambayo yanasafirishwa na kuuza nchi za nje. Kilimo pia ni muhimu kwa ajili ya kuhakikisha usalama wa chakula nchini na kwa wakulima wadogo kuwa na uhakika wa kipato chao.

Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, katika hotuba yake ya kuapishwa Aprili 2021 alisisitiza umuhimu wa sekta ya kilimo kwa uchumi wa Tanzania akisema: “Hivyo basi, tutazitazama kwa jicho la tatu na kuhakikisha kwamba zinapata utatuzi wa kudumu inayostahili, pia natambua kuwa Kilimo ni uti wa mgongo wa uchumi wa Taifa letu na tumelenga kukiendeleza”

Hii inaonyesha jinsi serikali ya Tanzania inavyothamini na kupigania ustawi wa sekta ya kilimo, inatambua umuhimu wake kwa ukuaji wa uchumi na maendeleo ya nchi.

Changamoto zinazoikumba sekta ya kilimo nchini
Sekta ya kilimo bado inakabiliwa na changamoto nyingi. Baadhi ya changamoto hizo ni pamoja na upatikanaji wa pembejeo za kilimo na viuatilifu licha ya jitihada zinazofanywa na serikali kama vile wakulima kujiandikisha ili kipata pembejeo hizo pamoja na viuatilifu lakini wakati mwingine upatikanaji wake umekuwa kwa awamu au kupatikana mbali na maneno walipo wakulima hivyo kulazimika kusafiri kufuata pembejeo hizo.

mabadiliko ya hali ya hewa, ukosefu wa teknolojia sahihi ya kilimo, na ukosefu wa mtaji wa kutosha kwa wakulima wadogo licha ya serikali kutoa mikopo kwa vijana nchini bado wakulima wengi wadogo wanachangamoto hii ya mitaji.

Miundombinu mibovu ya uhifadhi ,kulingana na chapisho la TBC online mwaka 2016 liliandika taarifa iliyotolewa na mkurugenzi msaidizi wa usalama wa chakula wizara ya kilimo,uvuvi na ufugaji Josephine Amolo alithibitisha upotevu wa asilimia 30 za chakula na kusema kuwa serikali infanya jitihada za kujenga maghala ya kuhifadhia chakula .

Masoko, sekta ya kilimo bado inakabiliwa na changamoto ya ukosefu wa masoko ya uhakika ya bidhaa za kilimo mfano; (September 19mwaka2019) shirika la itangazaji la Azam TV walichapisha habari inayohusu changamoto ya masoko wilayani Babati mkoa wa Manyara Tanzania. Tatizo hili liliripotiwa tena miaka miwili baadae kupitia chapisho la wizara ya kilimo mwaka 2021, ambapo waziri wa kilimo ,mifugo na uvuvi wakati huo profesa Adolf Mkenda (mb) alisema "tutahakikisha tunaondoa changamoto za masoko ya mzao ya kilimo"

Jitihada za serikali kutatua changamoto zinazo ikumba sekta ya kilimo
Kutokana na changamoto hizi, serikali ya Tanzania imechukua hatua mbalimbali za kuboresha sekta ya kilimo. Hatua hizo ni pamoja na kutoa mikopo kwa wakulima wadogo ili waweze kununua pembejeo na mashine za kisasa za kilimo, kuanzisha mfumo wa utafiti wa kilimo na kupanua maeneo ya umwagiliaji ambayo yatasaidia wakulima kupata mazao mengi kwa kipindi cha mwaka mzima.

Pia, Serikali imeanzisha mpango wa ushirikiano wa umma na binafsi katika kilimo (PPP), ambao una lengo la kuboresha sekta ya kilimo na kupunguza umaskini kwa kuhusisha wadau mbalimbali wa sekta ya kilimo, ikiwemo serikali, mashirika ya kimataifa, na wakulima wenyewe. Hii itasaidia kuongeza upatikanaji wa pembejeo, teknolojia ya kilimo na mtaji, pamoja na kuimarisha uwezeshaji wa wakulima wadogo.

Wapi serikali ipaguse zaidi kwenye sekta ya kilimo?
Wataalamu wa kilimo waongezwe ili wawafikie wakulima kiurahisi na kutatua changamoto walizonazo wakulima kwani hapa ndipo serikali itakapo inatimiza malengo iliyo jiwekea Katika kuiboresha sekta hii kwa kuwa inagusa vyanzo vya uzalishaji moja kwa moja hivyo kuongeza na kuchochea kukua kwa kilimo.

Pawepo na bei linganishi kati ya wanunuzi wa mazao ya wakulima , hapa pamekuwa na tabia ya baadhi ya wanunuzi kuwalaghai wakulima kwa sababu ya kukosa taarifa juu ya masoko ya bidhaa zao hivyo kujipatia manufaa kwa njia ya wizi lakini kama serikali itaweka bei linganishi utaweza kuwa saidia wakulima kupata stahiki zao

Wabobezi wa kilimo , serikali iongeze vyou vinavyozalisha wabobezi wa kilimo na kuweka kitengo cha ubobezi kutoka hatua anayo soma mwanafunzi wa elimu ya upili, ili huyo mwanafunzi abaki na uelewa ambao utakuwa ni rahisi kuuendeleza . Pia ili kuzalisha watu bobezi kwenye fani mahususi zenye kuleta mapinduzi ya kilimo nchini serikali lazima iangalie suala la ubobezi kwenye sekta hii kama ilivyo kwa nchi za wenzetu mfano , uingereza na kwa kufanya hivyo hatutakuwa tuna bahatisha kwenye mipango mikubwa ya kimaendeleo.
 
Changamoto zinazo ikumba sekta ya kilimo nchini

Thanks 🙏
 
Back
Top Bottom