Ushirikiano kwenye sekta ya kilimo kati ya China na Tanzania unaendelea kuleta mafanikio

ldleo

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
1,008
1,031
VCG111379102101.jpg

Fadhili Mpunji

Sekta ya kilimo ni moja ya maeneo yenye fursa kubwa za ushirikiano kati ya China na nchi za Afrika, lakini hadi sasa eneo hilo liko nyuma ikilinganishwa na sekta nyingine. China ni nchi ambayo kilimo ni jadi yake, na katika miaka ya hivi karibuni maendeleo ya kiuchumi na teknolojia vimeleta mapinduzi mkubwa kwenye sekta ya kilimo. Bara la Afrika kwa upande mwingine, pia lina jadi ya kilimo lakini kutokana na changamoto mbalimbali za kiuchumi na teknolojia, sekta ya kilimo bado iko nyuma.

Tatizo la usalama wa chakula ni moja ya ajenda zinazotajwa kwenye majukwaa ya kisiasa na kitaaluma katika nchi mbalimbali za Afrika. Kuna mambo makuu mawili yanayotajwa kuhusu usalama wa chakula barani Afrika, moja ni upungufu au ukosefu wa chakula, na la pili ni kukosekana lishe. Katika miaka 40 au 50 iliyopita, China pia ilikabiliwa na matatizo kama haya, lakini hatua kwa hatua imeweza kutatua matatizo haya.

Kwa kutumia uzoefu wake katika kuendeleza sekta ya kilimo China, imekuwa ikijitahidi kushirikiana na nchi za Afrika kuboresha sekta ya kilimo na kuondokana na changamoto hizo kupitia mpango maalum wa AGRA. Kupitia mpango huo, kuna miradi katika nchi 11 za Afrika ( Kenya, Tanzania, Uganda, Rwanda, Malawi, Msumbiji, Mali, Burkina Faso, Ghana, Nigeria na Ethiopia). Miradi hii inalenga mazao mbalimbali, iwe ni ya chakula au biashara.

Changamoto za sekta ya kilimo zilizopo kwenye nchi hizi, si kubwa sana ikilinganishwa na nchi zenye hali mbaya ya hewa. Lakini tatizo kubwa ni kuwa kilimo kinafanywa katika hali ya jadi, kikitegemea mvua, jembe la mkono au nyenzo dunia, na matokeo yake ni kuwa na tija ndogo. Kupitia mpango wa AGRA, China inashirikiana na nchi hizo kuunda minyororo inayoanza kwenye uzalishaji hadi soko. Kwenye mpango huu China itaoa utaalamu wa matumizi ya mbolea, shughuli za ugani, biashara ya mazao ya kilimo, na hata vyanzo vya fedha kwa ajili ya kuendeleza sekta ya kilimo.

Ushirikiano huu umekuwa ukileta mafanikio kwa viwango tofauti katika nchi mbalimbali. Hivi karibuni nchini Tanzania mradi wa ushirikiano kati ya China na Tanzania kwenye kilimo cha maharage ya soya umeonekana kuwa na mafanikio makubwa. Wakulima wa maharage ya Soya wanaoshiriki kwenye mradi huo kwenye wilaya za Mvomero na Kilosa mkoani Morogoro, wameshuhudia ongezeko la uzalishaji wa zao hilo kwa kutumia mbinu bora za kilimo na teknolojia ya kisasa. Ongezeko hilo sio tu limefanya wajitosheleze kwa chakula, bali pia limewapatia ziada wanayoweza kuiuza.

Lakini kwa upande mwingine, wakulima hao wamepewa mbinu mpya za matumizi ya zao hilo. Licha ya kuwa zao hilo limekuwepo Tanzania kwa miaka mingi, lakini kinywaji kinachotengenezwa kwa maharage ya soya ni kigeni kwa watanzania wengi. Kupitia vifaa vya kisasa na vya bei nafuu vinavyotoka China, wakulima sasa wanaweza kutengeneza juisi ya maharage ya soya yenye virutubisho na kuitumia. Matumizi ya juisi hii ya bei yamechangia pia kupambana na changamoto ya kukosekana kwa lishe bora.

Licha kuwepo kwa ushirikiano kwenye sekta ya kilimo kati ya China na Afrika, kiwango cha ushirikiano kwenye sekta hiyo bado kiko chini ikilinganishwa na sekta nyingine. Changamoto kwenye usalama wa chakula katika nchi mbalimbali za Afrika bado ni kubwa.

Tayari China imekuwa na uwezo kamili wa kuendeleza sekta yake ya kilimo. Hii ina maana ushirikiano zaidi kati ya pande hizi mbili, sio tu inaweza kutatua changamoto ya usalama wa chakula barani Afrika, bali pia inaweza kufungua fursa zaidi ya kuunganisha maendeleo ya kilimo na sekta nyingine.
 
Back
Top Bottom