Waliosoma fani za kilimo na mifugo na Jinsi walivyotumia elimu zao mpaka sasa kujikomboa binafsi na kuleta mapinduzi kwenye sekta ya kilimo na mifugo

Habari wana JF,binafsi nimeanzisha uzi huu nikiwa kama mwanafunzi katika sekta ya mifugo ambaye muda si mrefu ntahitimu masomo yangu na kuingia katika mfumo wa kutafuta maisha.
LENGO: Ni kutaka kujua na kukutanisha pia wataalamu wote waliosoma sekta ya kilimo na mifugo na hatua walizopiga mpaka sasa wakitumia fani zao hizo kwa kujikomboa binafsi kiuchumi na kuleta mapinduzi katika sekta hii
MATARAJIO:Ni kupata changamoto,hamasa na ushuhuda ili usaidie kuleta ugunduzi mpya katika sekta hii na kuifanya iweze kuendelea zaid kama inavyojulikana kwamba ndo sekta mama katika ukombozi wa uchumi wa mtanzania wa kawaida kabisa.
ASANTENI,NA NATEGEMEA USHIRIKIANO WA KUTOSHA
Sent using Jamii Forums mobile app

Kiongozi tunakuhitaji kwa elimu ili nasi tuingie kwenye mifugo biashara.
 
Habari wana JF,binafsi nimeanzisha uzi huu nikiwa kama mwanafunzi katika sekta ya mifugo ambaye muda si mrefu ntahitimu masomo yangu na kuingia katika mfumo wa kutafuta maisha.
LENGO: Ni kutaka kujua na kukutanisha pia wataalamu wote waliosoma sekta ya kilimo na mifugo na hatua walizopiga mpaka sasa wakitumia fani zao hizo kwa kujikomboa binafsi kiuchumi na kuleta mapinduzi katika sekta hii
MATARAJIO:Ni kupata changamoto,hamasa na ushuhuda ili usaidie kuleta ugunduzi mpya katika sekta hii na kuifanya iweze kuendelea zaid kama inavyojulikana kwamba ndo sekta mama katika ukombozi wa uchumi wa mtanzania wa kawaida kabisa.

ASANTENI,NA NATEGEMEA USHIRIKIANO WA KUTOSHA

Sent using Jamii Forums mobile app
Mimi ni graduate wa Sua kama wewe utavyokuwa siku zijazo

Unapowaza kumaliza chuo ni vzr kuwaza mambo ya mtaani kama ulivyouliza ni jambo jema. Lakini wewe mpaka sasa una elimu lakini una ujuzi gani? (kuna tofaut kubwa sana kati ya elimu na ujuzi)
Ukishajua ujuzi ulionao changanya na elimu yako songa mbele, anzisha connection, biashara ndogo ndogo, hata hapa jukwaani kuna wateja wengi sana, anza kuandika na kuelimisha wadau kuhusu taaluma na ujuzi wako baada ya muda utaona unaanza kuona njia mwenyew na utaendelea vyema na maisha yatakuwa murua kabsaaaa
 
Wakuu naomba muongozo nahitaji nitume maombi kujiunga na chuo cha kilimo hivyo naomba nifahamu

Vigezo vya kujiunga na chuo cha kilimo ikiwa ufaulu wangu form 4 ni

History C
Geography D
English D
Kiswahili D
Biology D
Civics D
B/math F

Msaada wenu plz mana nahitaji sana kusoma kilimo
 
Mi ni miongoni mwa waajiriwa katika sekta ya Kilimo na nipo field kabisa Iringa vijijini. Huwa naumia mno nikisika Maafisa Kilimo hatuna impact katika sekta lakini ndio ukweli huo.
Miongoni mwa mambo yanayochangia kwa mtazamo wangu ni haya;
1. Kilimo hakipewi kipaumbele kulingana na umuhimu wake
2. Asilimia kubwa wakulima hawana uwezo kugharamia Kilimo chenye tija
3. Uhaba wa vitendea kazi kwa maafisa. Huwezi niambia ninunue mahitaji ya demo plot ni sawa na mwalimu kujinunulia chaki, scheme of work, lesson plan....
4. Ukosefu wa mafunzo ya Mara kwa Mara kwa maafisa Kilimo, wanaachwa nyuma na dunia.
5. Maafisa Kilimo hawana nguvu ya kumlazimisha mkulima afuate taratibu za Kilimo bora wao wanashauri tu. Mkulima afuate asifuate ni lwake.
6. Ukichwangumu wa wakulima katika kubadilika.

Mi nashauri tupewe nguvu kisheria itakayolazimisha wakulima kufuata mambo ya msingi wanayoshauriwa, Mtu hajapanda kwa mstari na nafasi stahiki faini!!!! Na changamoto zote nilizoorodhesha zitazamwe naamini umuhimu wetu utaonekana.
NB: Nazungumzia wataalamu wa kilimo wa serikali.
 
Kiongozi tukiachana na demo plot wewe huko uliko haulimi ile binafsi wakulima wakaona hata vile wewe unafanya na kupata katika mashamba yako binafsi?Maana naamini kama unafanya na una matokeo mazuri binafsi wakulima watatamani kujifunza kutoka kwako ili na wao wapate kama wewe.
 
Nalima, Mara zote mavuno yangu yako tofauti na wengine. Tatizo ni suala la mkulima kubadilika ambalo kimsingi lipo mikononi mwake na ni HIARI yake halizimishwi kufuata mazuri ya mtaalamu.
Kiongozi tukiachana na demo plot wewe huko uliko haulimi ile binafsi wakulima wakaona hata vile wewe unafanya na kupata katika mashamba yako binafsi?Maana naamini kama unafanya na una matokeo mazuri binafsi wakulima watatamani kujifunza kutoka kwako ili na wao wapate kama wewe
 
Kuna wakulima wachache kwa mfano mwaka huu wameshtuka na wananiambia nao watalima kama mimi msimu ujao ili mavuno yaongezeke. Licha ya kujifunza kwao vikwazo wanavyoviona ni gharama na upatikanaji wa pembejeo bora mfano mbegu, mbolea na viuatilifu ambavyo upatikanaji wake ni mjini pekee.
Nalima, Mara zote mavuno yangu yako tofauti na wengine.

Tatizo ni suala la mkulima kubadilika ambalo kimsingi lipo mikononi mwake na ni HIARI yake halizimishwi kufuata mazuri ya mtaalamu.
 
Kuna wakulima wachache kwa mfano mwaka huu wameshtuka na wananiambia nao watalima kama mimi msimu ujao ili mavuno yaongezeke. Licha ya kujifunza kwao vikwazo wanavyoviona ni gharama na upatikanaji wa pembejeo bora mfano mbegu, mbolea na viuatilifu ambavyo upatikanaji wake ni mjini pekee.
Fulsa hiyo mtaalam fungua duka la pembejeo za kilimo jiongeze!!!
 
Wakuu naomba muongozo nahitaji nitume maombi kujiunga na chuo cha kilimo hivyo naomba nifahamu

Vigezo vya kujiunga na chuo cha kilimo ikiwa ufaulu wangu form 4 ni

History C
Geography D
English D
Kiswahili D
Biology D
Civics D
B/math F

Msaada wenu plz mana nahitaji sana kusoma kilimo
Vigezo ni hivi
IMG-20190529-WA0005.jpg
 
Mi ni miongoni mwa waajiriwa katika sekta ya Kilimo na nipo field kabisa Iringa vijijini. Huwa naumia mno nikisika Maafisa Kilimo hatuna impact katika sekta lakini ndio ukweli huo.
Miongoni mwa mambo yanayochangia kwa mtazamo wangu ni haya;
1. Kilimo hakipewi kipaumbele kulingana na umuhimu wake
2. Asilimia kubwa wakulima hawana uwezo kugharamia Kilimo chenye tija
3. Uhaba wa vitendea kazi kwa maafisa. Huwezi niambia ninunue mahitaji ya demo plot ni sawa na mwalimu kujinunulia chaki, scheme of work, lesson plan....
4. Ukosefu wa mafunzo ya Mara kwa Mara kwa maafisa Kilimo, wanaachwa nyuma na dunia.
5. Maafisa Kilimo hawana nguvu ya kumlazimisha mkulima afuate taratibu za Kilimo bora wao wanashauri tu. Mkulima afuate asifuate ni lwake.
6. Ukichwangumu wa wakulima katika kubadilika.

Mi nashauri tupewe nguvu kisheria itakayolazimisha wakulima kufuata mambo ya msingi wanayoshauriwa, Mtu hajapanda kwa mstari na nafasi stahiki faini!!!! Na changamoto zote nilizoorodhesha zitazamwe naamini umuhimu wetu utaonekana.
NB: Nazungumzia wataalamu wa kilimo wa serikali.
Nipo Iringa Ifunda mkuu,tutafutane
 
Kuna wakulima wachache kwa mfano mwaka huu wameshtuka na wananiambia nao watalima kama mimi msimu ujao ili mavuno yaongezeke. Licha ya kujifunza kwao vikwazo wanavyoviona ni gharama na upatikanaji wa pembejeo bora mfano mbegu, mbolea na viuatilifu ambavyo upatikanaji wake ni mjini pekee.
Mkuu ulivokua chuo ulisema coarse ya extension?Kama ulisoma vizuri je unalitumia kiasi gani katika kuelimisha hao wakulima?
 
Extension nilisoma ndio! Naitumia inavyotakiwa ila weka akilini kwamba wakulima wa leo sio wa jana na ndio maana nasisitiza juu ya mafunzo rejea kwa maafisa ugani. Sambamba na extension, kuwepo na nguvu ya kisheria kuwabana wakulima wakaidi. Kwa mfano katika afya mwananchi asiye na choo Afisa Afya ana namna ya kumlazimisha awe na choo lakini Afisa ugani siwezi kumlazimisha mkulima atumie mbegu bora. Utasema nitumie extension nmshawishi, ndugu mabadiliko ya wakulima yapo mikononi mwao hasa hawa wa kileo.
 
Proff Mamiro uyo mama acha , Dr Rwegasira ni mpenda sifa hatari
Hy demo ya Zabibu hatimaye imeandaliwa....!! Prof. Mamilo alikuwa anapinga sana kuwa hali ya hewa ya moro haifai kwa Zabibu, anyway...fact for fact.

Nilimuulizaga Dr. Rwegasira installation ya hizo screen house za pale Horticulture Unit, alichonijibu ndio kilinifanya kuwaza kitu Kingine cha kufanya, na nikaamua kumaliza tu degree lakini nikaapa sitalima kamwe, labda mashamba ya miti.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom