Equation x
JF-Expert Member
- Sep 3, 2017
- 29,483
- 40,497
Maana yangu katika kufanikiwa:
Kufanikiwa ni kuwa na uhuru wa kifedha, kuwa na amani moyoni, bila kuwepo na nguvu ya ziada ya ushurutishaji; uwe wa kimawazo, kiuchumi au kimazingira.
Hii inatafsiri, aliyefanikiwa anaweza kujiamulia mambo yake mwenyewe bila kuwepo na ushurutishaji wa kufanya kitu/jambo fulani kwa muda fulani.
Aliyefanikiwa anaweza akajiamulia kuamka muda wowote anaotaka yeye, na kwenda sehemu yoyote anapojisikia bila kuwepo na nguvu ya kumhimiza kufanya jambo au kitu fulani kwa muda fulani.
Ukiona kwa upande wako, ili upate pesa lazima uende akateseke au uwahi kazini/kwenye biashara yako, ata kama inakupa milioni 500; bado wewe hujafanikiwa.
Alyefanikiwa, anakuwa tayari alishaweka mifumo ya watu kumfanyia kazi; ata akilala mpaka saa kumi jioni; mifumo inakuwa inamletea mahitaji yake; huyo ndiye aliyefanikiwa.
Ukiona ili upate kipato lazima uwahi asubuhi, utii maagizo ya bosi wako n.k ata kama unapata pesa nyingi; amini wewe bado hujafanikiwa, bali upo unateseka na kuhangaika.
Kwa mazingira hayo; wengi bado hatujafanikiwa zaidi ya kuhangaika tu.
Je, wewe umefanikiwa? Toa sababu.