Bright Smart
JF-Expert Member
- May 4, 2011
- 643
- 312
Mkuu JBITUNGO masaa 16 ni mengi sana ni two third ya sikuInkoskaz
Hivi kweli tuna jeshi la usalama barabarani? Huko wa IGP Mwema, yuko wapi Afande Mpinga....kwanini haya yanatokea kama vile hakuna serikali? Jana nimeshuhudia kwenye ITV taarifa ya habari saa 2 usiku walikuwepo askari polisi wakirandaranda eneo lile kumbe hawakuwa na msaada wowote hata kutoa taarifa ktk kitengo cha maafa ili kurescue wale watu. Watz watz watz mimi binafsi siamini kama tuko salama! Tafakari.
Kwa wale mnaofuatilia taarifa ya habari, kuna vijana waliokuwa wakizungumza wakiwa wamebanwa na malori baada ya kupata ajali na kuomba msaada kupitia vyombo vya habari.
Majeruhi wawili waliobanwa katika lori la mizigo katika ajali iliyotokea eneo la Maseyu barabara ya Morogoro - Chalinze wamefariki Dunia baada ya kuchelewa kuokolewa kwa zaidi ya masaa 16 kutokana na kukosekana kwa vifaa vya uokoaji.
Jambo la kusikitisha, pamoja na kwamba wamekaa hai kwa muda mrefu lakini vyombo sahihi vya kuwakwamua kutokana na kubanwa na malori vimekosekana hadi wakafa wanaona.
Mungu isaidie Tanzania, watu wanakufa baada ya kuwa hai kwa zaidi masaa 10.
Swali la kujiuliza, vipi kama Lori hilo lingekuwa limembana waziri au mkuu wa mkoa akiwa ndani ya gari lake?.
Bila kuoneana aibu, hapo serikali mmefanya uzembe! R.I.P my fellow poor
Mkuu Copper, tunachotakiwa kufanya mimi...wewe na kila Mtanzania ni kuamka katika huu usingizi mzito na kuchukua hatua. Ni maafa ..ajali na mambo mengi sana yametokea na yanaendelea kutokea. Kila siku zinaundwa TUME kwa kutumia pesa yetu Walipa Kodi. Tokea MV BUKOBA mpaka Leo hii sijawahi kusikia ripoti ya matokeo ya TUME na uwajibikaji kutokana na uzembe.Mkuu Bora69, kwa specific tukio tufanyeje? Ni ukweli ulio wazi zaidi 85% ya ajali zinasababishwa na uzembe, ila jana watu wamebanwa katika ajali na hapakuwa ja jitihada za maana za kuwanasua hadi wamekufa hapo ndio ninaposikitika. Ingekuwa ni mtu wa hadhi fulani jitihada zote zingefanyika ila kwa kuwa ni wanyonge ndio hivyo tena.
Wewe usifikiri una akili kuliko wote humu na mtazamo wako wa kimagamba.
Mimi binafsi nafikiri umefika muda sisi Watanzania kuwa responsible na maisha yetu na mambo yanayotuhusu kwenye jamii zetu. Tunalalamika sana bila kupata suluhisho la Matatizo yanayotukabili katika maisha yetu ya kila siku.
Tumeweka ushabiki katika mambo ya Mipira...Big Brothers n.k na kusahahau mambo muhimu kwenye maisha yetu ya kila siku.
Asilimia 90 ya ajali zinazotokea na maafa hapa Tanzania zinatokana na UZEMBE uliopitiliza. Halafu sisi Watanzania tunabaki tukilalamika bila kuwa na mipango fasaha ya kutatua matatizo yetu.
Tusitegemee Serikali ikafanya kila kitu. Kwa sababu hao Viongozi/WanaSiasa wameshalewa na madaraka.
Tuacheni kulalamika Watanzania na tuchukue hatua madhubuti ili kujikomboa na haya MAJANGA.
Hii kazi ni yangu mimi...wewe na kila Mtanzania anayetaka mabadiliko na Maendeleo.
Tuache Ushabiki na lawama za kutupiana mipira. CHUKUA HATUA.
RIP MAREHEMU....POLENI SANA WAFIWA NA WATANZANIA WOTE MLIOGUSWA NA HILI JANGA.