Dig the EA
JF-Expert Member
- Dec 7, 2017
- 279
- 270
Ni utaratibu wa kitaalamu, kitaaluma na ujifunzaji kisaikolojia wanafunzi na walimu kupata muda wa kupumzisha akili. Lengo la mapumziko hayo ni kuipa akili muda wa kupata nguvu za kusoma na kuelewa masomo yaliyo mbele.
Kitu cha ajabu na kinachoendelea miaka ya hivi karibuni ni likizo hizo za mwezi wa tatu na wa tisa kutokufungwa. Shule nyingi katika mikoa mingi nchini wanafunzi na walimu hawafungi Shule. Wako busy madarasani wakisoma kama vile si likizo. Pressure ya kusoma likizo inatoka mikoani (Elimu) na Halmashauri ya wilaya husika( idara ya Elimu).
Pressure hiyo inasukumwa na hofu ya matokeo ya mitihani ya mwisho iwe ni kwa darasa la nne, darasa la Saba, kidato cha pili, kidato cha nne au kidato cha sita. Kwa maneno mengine Kuna kutokuamini kuwa kilichofundishwa miezi au miaka yote hakitoshi hadi uhitaji wa kufundisha likizo. Hiyo ni hofu. Pia mfumo wa Elimu yetu unathamini mitihani kuliko kujifunza, hali hiyo hufanya viongozi hao kufanya chochote ili mradi waone matokeo mazuri.
Matokeo yake ndo hayo ya Shule kutokufungwa na kazi zinaendelea. Madhara ya hali hiyo wanafunzi wanachoka akili na mwili kiasi cha kutokujifunza wala kuelewa. Upande wa walimu wamejaa vinyongo na malalamiko sababu ya vitisho na kulazimishwa kufundisha kipindi cha likizo.
Ni Bora Kama serikali kupitia TAMISEMI ingetoa tamko kuwa likizo za mwezi March na September kuwa hazipo na zimefutwa, kuliko kuziweka harafu hazizingatiwi.