Mwisho wa siku ukichunguza sana, siku hizi wanawake wengi hasa wale waliojaliwa kazi za kipato/mshahara hata hizo kazi za ndani anazosema hawazifanyi. Na ki-ubinadamu rahisi kuelewa kwa nini hawafanyi, kwa sababu hizo kazi za mshahara nyingine ni ngumu na zinawachosha, kama zinavyowachosha wanaume. Lakini sasa wanatafuta na kuwaachia kazi zote ma-housemaids. Na kibaya zaidi hata mshahara wa hao housemaids wanataka me ndiyo walipe. Sasa unajiuliza nini maana ya mke kufanya kazi za kipato, maana kazi za ndani hafanyi tena, na faida ya kazi anazofanya huko nje anasema haina uhusiano na matumizi ya familia maana ni jukumu la mme kuitafutia familia yake. Kama ni hivyo nini hasa maana ya kuwa na mke kama huyo hapo nyumbani!! Wanawake wengine ni shida, they are too selfish & greedy