Kwanza nikupe pole sijui umeoa kabila gani (samahani lakini ) na umeoa Mji wa namna gani, kuanzia kushika dini, hali ya kiuchumi wazazi wake, yeye mwenyewe Elimu yake, km Kuna ndugu zake waliolewa, na je kalelewa na wazazi wote 2 au na single-mother (rejea mabandiko yangu humu). Hivyo vitu ni muhimu kuvijua.
Pili, kuanza kuomba tendo la ndoa nadhani siyo shida sn nadhani ni tabia ya baadhi ya akina dada either sababu ya aibu au kuona kuwa akikuanza utamuona kicheche. Wapo wanawake wengi tu wenye tabia hiyo, hivyo kwangu mimi hilo hakuna shida sn ingawa wakati mwingine ni wajibu wake pia kukumbushia pindi anapohitaj. Ila km hata unapomkubusha anakupa kwa manati, hiyo siyo sahihi, ni ujeuri.
Tatu, inaonekana huyo mwanamke wewe ndiye una shida naye yeye hakuhitaji kiviiile. Na inaonekana wewe ndiye ulitumia nguvu nyingi kumshawishi umuoe na alikubali kwa sababu anazojua yeye. Km una pesa au umesoma hizo ndiyo sababu.
Nne, hujatuambia km mkeo ulimtoa kijijini au mjini. Wengi wa kijijini wakija mjini mwanzoni huwa na haibu ila akizoea Mji balaa lake ni kubwa sn.
Tano, hujatuambia km mna mtoto au la ili tujue tukushauri vipi. Km hamna mtoto Kuna shida hapo. Yani ulale na mwanamke mara tano akiwa bado mbichi akose mimba?
Mwisho, MKEO siyo riziki, ana anayempenda kwa dhati. Kwa ufupi, kibri chake kinachangiwa na huyo bwana wa nje. Na wewe una miaka 31 unashindwaj kusimama km mwanaume alafu unasema "Kila mara amekuwa anakuaga anaenda kusalimia baba yake" acha ujinga kijana wangu huyo ni mkeo mwenye mamlaka ya kumpa ruhusa ni wewe. Achana na wehu wa mitandaoni wanaosema wao wanatoa tu taarifa kwa wame zao siyo kuomba ruhusa. Umeshamgundua ni jeuri mnyime sasa hizo route zake, huko anaendaga kukutana na bwana yake siyo baba yake.
Alafu mwanaume unawezaj ku-argue na mwanamke kwenye sm namna hiyo. Vijana wa siku hizi hovyo kabisa, kwanini mnataka kuendesha ndoa kizungu. Mnaendesha ndoa km hamjuhi Mila na tamaduni zenu za Kiafrika. Simama imara kijana wangu, ndoa siyo lelemama. Yakikushinda achana naye, huyo ni kichomi kitakutoboa hadi mbavu.