Wakurugenzi wa Makampuni ya Mafuta ya PUMA, Oryx, TOTAL na Lake Oil wakamatwa na Polisi kwa kuvuruga mfumo wa usambazaji!

Walivyoingia ktk biashara hii hawakujua kwamba kuna regulator ambaye ni Chombo cha serikali ??
Hawakukubaliana na bei ilekezi kufuatia mzigo ulinunuliwa kwa bei gani ??
Regulatory nyingi Tanzania ni kama mahakimu mahakamani. Tuna taasisi nyingi ambazo operation cost zao hutegemea wadau wanaowasimamia na siyo oc toka serikalini.
Hivyo mfanyabiashara amebebeshwa mzigo na kupelekea mwananchi wa kawaida kununua bidhaa kwa gharama kubwa sana.
 
Polisi jijini Dsm imewakamata wakurugenzi wakuu wa kampuni za mafuta za Puma, Total na Oryx waliokuwa kwenye kikao cha kibiashara.
Kadhalika polisi wanamsaka mkurugenzi mkuu wa Lake Oil ili aunganishwe na wenzake.

Imeelezwa wakurugenzi hao wanadaiwa kuvuruga mfumo wa usambazaji mafuta nchini.

Chanzo: ITV habari!
dah! MUNGU ni mwema, bado kidogo tutaifikia china, ukibugi serikali inakunyonga
 
Mkuu wanamjua jiwe hataniwi. Wewe hukuona ile habari ya kufungua petrol station ya serikali. I think it was in Dodoma. So kiama chao kinakaribia. Ila mkuu wewe fikiria mtu kutoka full tank ya 125k to 75k then wajinga wachache wanataka kuturudisha Misri wakati wenzao tushaanza kuenjoy maisha ya Kanani

Hivi unatambua tumefikaje kwenye hiyo bei ?
Unamjua MBS ?
Unaijiua OPEC?
Unaijua RUSSIA
Unajua COVID 19?
Lockdown je ?
 
Ewura waje na bei ya sh. 800 ili wafiche vizuri hayo mafuta, wamezoea kutunyonya na mabei yao huku wakitengeneza faida kubwa (windfall profit). Kuna wengine kila kukicha wanafungua vituo vipya, which means wanapata faida ya kufuru...
 
Ndio maana wakurugenzi wa makampuni hayo wamejenga majengo ya kufa mtu kama kule mbezi Kimara.
Mbona hata wakurugenziccm wote wana majumba nitajie mkurugenzi wa SU shirika la umma asiye na majumba? Viongozi wa CCM wote wana majumba hata Naibu Rais ndugu Daud Bashite ana majumba upanga masaki mwanza Dubai South Africa viongozi wote wa CCM wana majumba kila kona Tanzania
 
Ewura waje na bei ya sh. 800 ili wafiche vizuri hayo mafuta, wamezoea kutunyonya na mabei yao huku wakitengeneza faida kubwa (windfall profit). Kuna wengine kila kukicha wanafungua vituo vipya, which means wanapata faida ya kufuru...
Wafanyabiashara walinunua mafuta kwa bei kubwa hawakuyauza yote baada ya corona kupita hawajarejesha pesa zao faida na kodi wamelipa zote, ghafra mkashusha Bei kwa mafuta ya zamani ambayo alinunua Bei kubwa na kodi mlichukua huoni kama ni kuwaonea wafanyabiashara? Bei elekezi ijikite kwenye mafuta ya rahisi yakiyokuja na meli mpya siyo kushusha bei kwa mafuta ya zamani kisha kumpeleka mfanyabiashara jela kumpa kesi ya uhujumu uchumi, huo ni uonevu mkubwa sana na kama CCM wanataka pesa za kampeni ni kwa nini wasiwaombe msaada kwa wema kuliko kutumia mbinu hiyo haramu.
 
Ukinunua gunia la mahindi kwa laki moja ukalipa kodi lazima uuze kwa laki na ishirini ili kufidia gharama zako zote, ikija kauli kuwa uuze gunia kwa elfu 80 pasipo kujali kuwa ulinunua kwa laki moja ndipo Tatizo huanzia na lazima utahitaji kutunza mahindi yako usubirie bei ipande upate kurejesha pesa zako na faida, huu ni mfano kwa wale wafanyabiashara walionunua mafuta kwa bei kubwa lakini sasa wameambiwa washushe pasipo kushushiwa kodi pia lazima watakaa na mafuta yao kutafakari kwanza.
 
Si wameshapata mkopo kutoka ufaransa... Watumie hizo kuliko kuumiza watanyabiashara ambao ni wapiga kura na wafadhiri wa chama pendwa...
Watawatishia kesi za uhujumu uchumi kwa kuogopa kukaa jela kama Rugamalila watalipa faini mabilioni bila kosa watapata pesa za kampeni
 
serikali inapaswa kuchukua biashara ya mafuta ijenge vituo vyake kila mkoa itapiga mabilioni yanayokwenda nje kila siku biashara hii itawezekana kwa kuwa Mkulu hataniwi ni pesa chap chap na inalipa sana then tupungize kodi na ushuru kwenye maduka ya walalahoi!manake biashara nyingi za wapiga kura wa Mkulu zimeangushwa na kodi kubwa

hiki ni chanzo kipya cha mapato makubwa ya serikali wakichangamkie haraka tupate pesa ya kujenga SGR na kuwakomesha mabeberu, hili wazo lapaswa kutua mezani kwa Mkulu haraka! na amteu mwanajeshi mstaafu asimamie huo mradi mfano mkuu wa majeshi mstaafu nk na kila kituo kilindwe na mwanajeshi mwenye silaha ili staff waogope kuiba na kuwe na supervisor wanaokagua hesabu daily!
Ndugu umewahi kufanya biashara yoyote japo ya Genge la nyanya? naona unaongea vitu vya kufikirika unasema serikali iuze mafuta!! Serikali ipi unazungumzia hii iliyovuruga soko la korosho na sukari au?
 
Ndugu umewahi kufanya biashara yoyote japo ya Genge la nyanya? naona unaongea vitu vya kufikirika unasema serikali iuze mafuta!! Serikali ipi unazungumzia hii iliyovuruga soko la korosho na sukari au?

Mimi ni kijani naamini Mkulu atasikia hili namsihi achukue hii fursa kama chanzo kipya cha mapato ya serikali na kuleta nafuu kwa wapigakura wake kupitia kupunguza kodi za maduka mitaani ambayo mitaji inakata maduka yanafungwa kila siku kodi kubwa , mapato ya mafuta yatumike kufidia punguzo la kodi za maduka mitaani na kuwaletea raia nafuu ya maisha na hapo atawafunga mdomo Bwana Nape na Prof Mukandala ambao wanasema Mkulu hafuati ilani ya Chama inayomtaka kujali maendeleo ya watu kwanza na si miundombinu!!

Nashauri Mkulu tunaemkubali sana aunde kamati ya kudumu ya huu uwekezaji mpya wa mafuta, Mkuu wa Majeshi mstaafu awe Mwenyekiti , katibu awe Bashe ila asaidiwe na Zitto atakaempa mawazo mbadala na kinzani ( watu hawa wawili ni geniuses kwa mawazo yangu)

Naishauri serikali sasa iamue inunue na kuuza mafuta yenyewe kwenye vituo vyake nchini na ichukue tenda za mafuta nje ya nchi tutaona matunda yake muda mfupi tu kuna hela sana huko kwenye mafuta ndo maana mabeberu hawaachii na serikali wakipata faida tupunguziwe kodi za biashara za maduka yetu mitaani, muda wa mabeberu kuiba bongo umeisha!!

Inaitwa state capitalism, mkuu najua ninachosema nimekisomea tena nje si hapa elimu ya kukariri nakuhakikishia tatizo letu ni kukosa watu sahihi tu kusimamia miradi, hicho kinawezekana in one day, kupanga ni kuchagua! hata ukuta wa Mererani mlibeza leo yametolewa mawe ya ajabu!

mimi naishi kwa business ndugu i know everything about business
 
Polisi jijini Dsm imewakamata wakurugenzi wakuu wa kampuni za mafuta za Puma, Total na Oryx waliokuwa kwenye kikao cha kibiashara.
Kadhalika polisi wanamsaka mkurugenzi mkuu wa Lake Oil ili aunganishwe na wenzake.

Imeelezwa wakurugenzi hao wanadaiwa kuvuruga mfumo wa usambazaji mafuta nchini.

Chanzo: ITV habari!
Mkuu,Kosa lao ni nini?Ewura Inapanga Bei kwa kuangalia bei katika soko la dunia lakini je inaangalia hawa jamaa wana stock ya mafuta kiasi gani?Je kama bei inashuka kila mwezi ilhali wao wana stock kubwa je serikali inawafidiaje hio hasara?Profit margin ya Mafuta ni ndogo na unapokuwa na reserve kubwa kisha bei ikashuka ni bora usiuze mpaka bei itakapopanda tena.Mafuta yamepungua bei kwa kiwango kikubwa katika soko la dunia.Serikali kabla ya kushusha bei ilipaswa ikae na wadau kujua actual fuel stock sokoni ni kiasi gani.

Vile vile utaratibu wa kupandisha ama kushusha mafuta bei kila mwezi ungetakiwa uangaliwe na badala yake tuwe na ama 45days au hata three months.Na pia records za fuel reserve ziwapo tena very updated.

Kuna kampuni kama Tiper ambayo naamini kabisa inaweza kufanya kazi ya kuwa Reserve kwa niaba ya serikali na labda kampuni binafsi nyingine mbili ziruhusiwe kuwa reservers ambapo wengine wote wanunue mafuta kwao.Waweke to kiwango cha storage Capacity kama basis ya kuwa bulk importer.

Lazima kuna sababu ya hii sintofahamu.
 
Revealed: 7 oil firms control over 67pc of market share

View attachment 1492872

Imebidi ni google unapotaka kuangalia how things will work out in oil retail unahitaji data kujua how you will be affected

Umeona hapo Oryx 15.5% Puma 14.4% na Total 8.5% share yao kwa pamoja ya soko ni 38.4% jumlisha na Lake Oil inazidi 40%.

Sasa usidhani korosho hizo uchezee, ukifingia hao kichwa kichwa utatia akili aichukui mwezi uchumi utakuwa kwenye hali mbaya hatari. Embu acheni kujifurahisha.
Hizi statistics zako ni za muda sana, 2018 Total ilinunua kampuni ya mafuta ya Gapco, hivyo market share yake kwa sasa ni kubwa. Bado anakiwanda cha kutengeneza lubricants hapa hapa nchini.
 
Bei ya mafuta katika soko la dunia imeshuka.lakini hapa nchini Kuna sehemu watu wananunua Lita 1 ya petrol kwa zaidi ya shilingi elfu 4.hapana huu ni uhujumu uchumi.
Daa wapi huko!?? Hapa Moro bei ni 1578

California love
 
Polisi jijini Dsm imewakamata wakurugenzi wakuu wa kampuni za mafuta za Puma, Total na Oryx waliokuwa kwenye kikao cha kibiashara.
Kadhalika polisi wanamsaka mkurugenzi mkuu wa Lake Oil ili aunganishwe na wenzake.

Imeelezwa wakurugenzi hao wanadaiwa kuvuruga mfumo wa usambazaji mafuta nchini.

Chanzo: ITV habari!

Kwa hiyo polisi wameanza kuingilia vikao vya biashara Kama vikao vya siasa?!

Kama Wana makosa si wangepelekewa tu hati ya kuwaita kunakotakiwa wakajieleze?

Utaratibu wa namna hii haujengi bali utazidi kuchafua uhusiano wa serikali na wawekezaji.
 
Kwa hiyo polisi wameanza kuingilia vikao vya biashara Kama vikao vya siasa?!

Kama Wana makosa si wangepelekewa tu hati ya kuwaita kunakotakiwa wakajieleze?

Utaratibu wa mamma hii haujengi bali utazidi kuchafua uhusiano wa serikali na wawekezaji.
wawekezaji hatutaki kwasasa serikali ya Magu inauwezo wa kuwekeza! wezi tu wale wote waende tu!
 
Back
Top Bottom