EWURA: Tuna mafuta ya kutosha Nchini, wenye vituo lazima wawe na mikataba na waagizaji

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,308
5,460
Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imeendelea kuwahakikishia wananchi upatikanaji wa uhakika wa mafuta nchini baada ya kutembelea maghala ya kuhifadhia mafuta jijini Dar es Salaam, 23 Julai 2023.

Ziara hiyo iliyoongozwa na Waziri wa Nishati, January Makamba, na kujumuisha watendaji wa EWURA, PBPA, TAPSOA, TPA na Wizara ya Nishati, ilifanywa katika kampuni za mafuta za TIPPER, LAKE OIL, MOUNT MERU,MOIL,CAMEL OIL, TOTAL ENERGIES na PUMA.

Waziri Makamba na ujumbe wake pia walitembelea eneo la kupokelea mafuta katika bandari ya Dar es Salaam kwa lengo la kujiridhisha kuhusu uingiaji na upakuaji wa bidhaa za petroli.

Mkurugenzi Mkuu wa EWURA, Dkt James Andilile alisema ziara hiyo ni utekelezaji wa wajibu wa EWURA kusimamia na kufuatilia mwenendo wa upatikanaji wa mafuta nchini na ametumia fursa hiyo kuwasihi watumiaji wa mafuta kutokuwa na hofu kwani hakuna uhaba wa mafuta.

Amesema “Nchi ina mafuta ya kutosha, kwa sasa kinachofanyika ni kuendelea na utaratibu wa kusafirisha mafuta kuelekea maeneo mbalimbali hasa baada ya kujitokeza kwa changamoto katika maeneo ya mji.

“Suala la vituo ambavyo vipo pembezoni mwa miji, tumekubaliana kuna umuhimu wa wenye vituo kuwa na mikataba na waagizaji wa mafuta wa jumla na mikataba hiyo itawasilishwa EWURA kabla ya tarehe 31 Julai 2023 kwa mujibu wa Leseni aliyopewa kila mwenye kituo awe na mikataba angalau na waagizaji wawili.

“Lengo ni kuwawezesha wauzaji wa rejareja kuwa na uhakika wa kuuza mafuta badala ya kutegemea utaratibu wa kubahatisha.”

================

Waziri wa Nishati, January Makamba amesema hakuna uhaba wa mafuta nchini, huku Serikali ikiwa imejipanga kuhakikisha inatatua changamoto ya upatikanaji wa Dola kwa Wafanyabiashara.

Waziri Makamba ameyasema hayo wakati wa ziara ya ukaguzi wa maghala mbalimbali ya kuhifadhia mafuta na bandarini baada ya kuibuka kwa sintofahamu katika baadhi ya maeneo nchini Watu wakidai kuna uhaba wa mafuta ikiwemo Ifakara Mkoani Morogoro.

“Kama ambavyo mmeshuhudia huwezi kusema nchini kuna upungufu wa mafuta kutokana na mwenendo ulivyo kwa maana mafuta yanaendelea kusukumwa katika Depo nyingine”
 
Back
Top Bottom