Wakurugenzi wa Makampuni ya Mafuta ya PUMA, Oryx, TOTAL na Lake Oil wakamatwa na Polisi kwa kuvuruga mfumo wa usambazaji!

Utafurahi kiasi gani pale wewe unaponunua kitu chako kwa bei ya 2000 kwa ajili ya biashara then anatokea mtu anakuamuru uuze kwa 500?
Sio kweli,soko la dunia mafuta yameshuka sana.
lakini mbona mafuta yakipanda soko la dunia,wamiliki wa hizi petrol station na wao wanapandisha fasta hata kama anastock ya mafuta aliyonunua mwezi mmoja nyuma?
 
Mimi ni kijani naamini Mkulu atasikia hili namsihi achukue hii fursa kama chanzo kipya cha mapato ya serikali na kuleta nafuu kwa wapigakura wake kupitia kupunguza kodi za maduka mitaani ambayo mitaji inakata maduka yanafungwa kila siku kodi kubwa , mapato ya mafuta yatumike kufidia punguzo la kodi za maduka mitaani na kuwaletea raia nafuu ya maisha na hapo atawafunga mdomo Bwana Nape na Prof Mukandala ambao wanasema Mkulu hafuati ilani ya Chama inayomtaka kujali maendeleo ya watu kwanza na si miundombinu!!

Nashauri Mkulu tunaemkubali sana aunde kamati ya kudumu ya huu uwekezaji mpya wa mafuta, Mkuu wa Majeshi mstaafu awe Mwenyekiti , katibu awe Bashe ila asaidiwe na Zitto atakaempa mawazo mbadala na kinzani ( watu hawa wawili ni geniuses kwa mawazo yangu)

Naishauri serikali sasa iamue inunue na kuuza mafuta yenyewe kwenye vituo vyake nchini na ichukue tenda za mafuta nje ya nchi tutaona matunda yake muda mfupi tu kuna hela sana huko kwenye mafuta ndo maana mabeberu hawaachii na serikali wakipata faida tupunguziwe kodi za biashara za maduka yetu mitaani, muda wa mabeberu kuiba bongo umeisha!!

Inaitwa state capitalism, mkuu najua ninachosema nimekisomea tena nje si hapa elimu ya kukariri nakuhakikishia tatizo letu ni kukosa watu sahihi tu kusimamia miradi, hicho kinawezekana in one day, kupanga ni kuchagua! hata ukuta wa Mererani mlibeza leo yametolewa mawe ya ajabu!

mimi naishi kwa business ndugu i know everything about business
Ikiwa kuna mtanzani mpaka leo bado anaamini serikali inaweza kufanya biashara basi naona tatizo ni kubwa kuliko tunavyodhani anyway endelea kuamini unachamini Ila kwa mawazo ya namna hii ndio maana Nchi za Africa umaskini umejenga makao yakudumu
 
Bei ya mafuta imeshuka sana kutoka $60 na hivi sasa ipo kama $25. Hiyo ni kwa sababu hakuna soko la mafuta kutokana na COVID-19 ndege nyingi ziko parking. demanding ya mafuta kwenye ulimwengu wa kwanza imshuka sana kutokana na lockdown etc. BA wanawafukuza marubani karibu 300 na wengine watapunguza mishahara kuona mwelekeo, kwa hivi sasa mafuta yapo chini sana. Je, walikuwa wanapanga nini? Kuwakomoa Watanzania kwa bei ghali?
Utaratibu wa usambazaji/uagizaji na kutambua mahitaji ya mafuta huwa ni jukumu LA nani?Kwa nini hadi uhaba/ukosefu wa bidha muhimu utokee na kusababisha kero ndipo hatua zianze kuchukuliwa?Je,hapo waliokamatwa ndiyo waliosababisha tatizo LA ukosefu wa mafuta?Hatuna mifumo ya regulations of demand and supply in the country?
 
Bei ya mafuta imeshuka sana kutoka $60 na hivi sasa ipo kama $25. Hiyo ni kwa sababu hakuna soko la mafuta kutokana na COVID-19 ndege nyingi ziko parking. demanding ya mafuta kwenye ulimwengu wa kwanza imshuka sana kutokana na lockdown etc. BA wanawafukuza marubani karibu 300 na wengine watapunguza mishahara kuona mwelekeo, kwa hivi sasa mafuta yapo chini sana. Je, walikuwa wanapanga nini? Kuwakomoa Watanzania kwa bei ghali?
Ni q
18$
 
[SUP]View attachment 1492874[/SUP]

[SUP]View attachment 1492878[/SUP]

Kesho nchi ikiingia vitani ni storage za watu kama hawa serikali ndio itaanza kutaifisha maana sisi wenyewe hatuna. Kuna mambo mengine kupitia uwekezaji ni kama tunapata free ride principles. Kasheshe sasa na adui kwenye vita lengo la kwanza ni kulipua reserve za mafuta. Kama serikali huna budi kuwa na vyako ulivyovificha ardhini.

Ni hivi kama hawana wataalamu wa maswala ya Strategic za mafuta huko Ewura na TPDC wakae mbali na kuvuruga hiyo it is a very costly economic business.
Kwahiyo unaombea inchi iingie kwenye machafuko
 
Ukinunua gunia la mahindi kwa laki moja ukalipa kodi lazima uuze kwa laki na ishirini ili kufidia gharama zako zote, ikija kauli kuwa uuze gunia kwa elfu 80 pasipo kujali kuwa ulinunua kwa laki moja ndipo Tatizo huanzia na lazima utahitaji kutunza mahindi yako usubirie bei ipande upate kurejesha pesa zako na faida, huu ni mfano kwa wale wafanyabiashara walionunua mafuta kwa bei kubwa lakini sasa wameambiwa washushe pasipo kushushiwa kodi pia lazima watakaa na mafuta yao kutafakari kwanza.
Huwa najiuliza kwann serikali haitoi ruzuku kufidia hasara kwa hawa wafanya biashara.....?! Details za manunuzi yao si wanazo....?!
 
yes nimesomea hizi vitu najua sana , kufa mashirika ya umma sababu ziko nyingi tofauti kwa wakati tofauti, ila sera mbovu na usimamizi toka juu kwa Rais ukiwa legelege wenye kulindana mashirika yanakufa kutokana ufisadi na uzembe

kwa Nyerere alikuwa msomi peke yake na alielemewa na kujenga siasa na si uchumi , wengine kina Mwinyi, Mkapa na Kikwete raia hawakuwa na hofu nao sana watu waliiba tu bila hofu kwa kuwa sera ya kulindana ilikuwa ndo utaratibu wa maisha

kwasasa Magu hataniwi anatumbua na kunyoosha wazembe wajuaji na mafisadi akisaidiwa na Takukuru na polisi ni wakati huu tu Mashirika ya umma yakianzishwa yatasimama na faida inaonekana,

ni wakati huu wa Magu tu anaeogopewa na wasaidizi wake kwa hofu ya kutumbuliwa na kuwekwa bayana machafu yao tunaweza kutekeleza sera ya uchumi inaitwa State Capitalism ( serikali kuwa mwekezaji mkubwa) na kuizika Ujamaa na Kujitegemea iliyopitwa na wakati na isiyotekelezeka!!

kiuchumi huu Ni wakati sahihi kwa serikali kutosikiliza mayowe ya hali ngumu na kukazana kujenga miundombinu na si kujali maisha ya watu manake kwa nchi ni masikini lazima Rais uchague kimoja aidha ujali infrastructure development (Magu) au social welfare.( wote waliobaki) .

Wakati huu wafanyakazi wa serikali wanaiba kidogo kwa hofu ya kutumbuliwa ndio muda sahihi kwa Magu kujaza miradi mikubwa ya kimkakati na serikali kuwekeza katika vyanzo vikubwa vya mapato kama mafuta, umeme madini na usafiri wa anga na kuwaachia raia kuwekeza kwenye viwanda na huduma

Magu akitoka madarakani nchi inaweza kuchukua sera ya Free Market Economy kwakuwa miundombinu inakuwa imeboreshwa sana
Mbona shirika la ndege lina bei sana nauli zake na wakati tunategemea liwe chini kushinda zote, kama fastjet waliweza kuweka nauli ya daladala wao serikali wanashindwa wapi?!
 
Kwahiyo unaombea inchi iingie kwenye machafuko
Mbona jeshi wananunua mizinga na kuna askari wapo tu wanafanya mazoezi ina maana wanaombea machafuko.

Ilikuwa ni point tu kwenye maswala ya National security nishati ni sehemu ya silaha muhimu kuliko yoyote unayoijua wewe.
 
Utaratibu wa usambazaji/uagizaji na kutambua mahitaji ya mafuta huwa ni jukumu LA nani?Kwa nini hadi uhaba/ukosefu wa bidha muhimu utokee na kusababisha kero ndipo hatua zianze kuchukuliwa?Je,hapo waliokamatwa ndiyo waliosababisha tatizo LA ukosefu wa mafuta?Hatuna mifumo ya regulations of demand and supply in the country?
Are you sure?
 
Back
Top Bottom