Wakurugenzi wa Makampuni ya Mafuta ya PUMA, Oryx, TOTAL na Lake Oil wakamatwa na Polisi kwa kuvuruga mfumo wa usambazaji!

Kesho ni siku ya kutoa bei mpya ya mafuta, hapa nawaza nibeti kuweka mafuta full tank kwamba bei itapanda, au nisijaze kabisa leo nisubirie kesho inaweza kushuka tena?
 
Na kuna kipindi wanaagiza mafuta mengi kwa bei ndogo na ikija kupanda inakuwa faida kwao
Tatizo siku zote ni pale tu mafuta yanaposhuka, mwaka jana mwanzoni mafuta yalipanda hadi kufika 2300 kwa dsm, na wala hakukuwa na shida ila leo yameshuka wanaanza kulialia
Kwenye mafuta waweke misingi imara ya wazi jinsi ya kuangalia bei hasa mafuta ya ndani ya Nchi kwani huwa kuna kipindi waagizaji huagiza mafuta kwa bei kubwa wanalipa kodi zote na ikija kushuka bei wakati mafuta ya awali yakiwa bado yako sokoni huathirika kwa kupata hasara kubwa, yapo mapungufu mengi kwenye mfumo wa biashara ya mafuta yafaa Serikali waunde tume maalum kuliweka sawa hilo jambo.
 
Ewura waje na bei ya sh. 800 ili wafiche vizuri hayo mafuta, wamezoea kutunyonya na mabei yao huku wakitengeneza faida kubwa (windfall profit). Kuna wengine kila kukicha wanafungua vituo vipya, which means wanapata faida ya kufuru...
Hayo mafuta wayachimba chumbani kwako?
 
Tuombe Mungu Sheria ziwe zimebadilishwa vizuri ama la yatatutokea kama ya aftermath ya Azimio la Arusha, nafikiria kiumbea zaidi
 
Polisi jijini Dsm imewakamata wakurugenzi wakuu wa kampuni za mafuta za Puma, Total na Oryx waliokuwa kwenye kikao cha kibiashara.
Kadhalika polisi wanamsaka mkurugenzi mkuu wa Lake Oil ili aunganishwe na wenzake.

Imeelezwa wakurugenzi hao wanadaiwa kuvuruga mfumo wa usambazaji mafuta nchini.

Chanzo: ITV habari!
Harakati za kuibeba TPDC na Vituo vyake vya mafuta Zimeanza, Yale Yale ya Fastjet
 
Na kuna kipindi wanaagiza mafuta mengi kwa bei ndogo na ikija kupanda inakuwa faida kwao
Tatizo siku zote ni pale tu mafuta yanaposhuka, mwaka jana mwanzoni mafuta yalipanda hadi kufika 2300 kwa dsm, na wala hakukuwa na shida ila leo yameshuka wanaanza kulialia

Weka mafuta leo kesho bei inapanda mark my word kwa Tsh. 150- 170
 
Je wanayo mahesabu ya kuonyesha manunuzi na majuzi yao na stock zao ?
Kwa uelewa wangu mdogo wa stock mngt kuna system inaitwa first in, first out , sasa old stock either ulionunua bei kubwa au ile ulionunua kwa bei ya chini itakuwa imetoka, sasa mambo mengine yanaenda kwenye mahesabu yako mwisho wa mwaka mauzo vs manunuzi, utapata faida au hasara, na kufanya analysis ya hasara imetokana na selling price vs cost za manunuzi na related cost au mambo mengine??
Sasa sijui unajua mambo haya au nampigia mbuzi guitar

Lakini pia anapaswa ajue kuwa Price ya hapa nchini inaconsider cost za manunuzi kwa mwezi husika na ndio mfumo EWURA wanautumia kwahiyo sio wanalazimishwa kuuza kwa bei hiyo ila ni kuwa regulator anajua mafuta yalinunuliwa kwa cost zipi na yanapaswa kuuzwa kwa cost ipi ndio sababu inawezekana walikuwa wanataka kuhold sababu wanajua watatengeneza margin kidogo kwa mwezi unaofuata
 
Kazi kubwa ya efd mashine ni kumonitor mauzo ya mfanyabishara lakini, linapokuja suala la umenunua kiasi gani hilo hajali. Tambua sheria ya kodi mbogo huangalia umeuza nn
Unavyotengeneza fs purchases zako unajitungia au kunakuwa na documents kuthibitisha manunuzi mfano kwa mafuta import duty , vat on purchases n.k
Kwa hiyo hapa huoni kwamba utapata information unazotaka???
 
Mkuu price ya mafuta inategemea na vitu vingi sana. Bei ya shipping, gharama ya kupakua na kuhifadhi, gharama ya internal distribution, bado kodi kibao, wafanyakazi na gharama za kulipia petrol stations. Hivyo sikuona haja ya kutumia bunduki kuwatisha. Serikali inanguvu sana
Ingewaita wakae waongee. Hata wao sio wendawazimu, wanasababu zao. Naomba sana msitupeleke Mtwara na Lindi na Mtibwa na Kilombero plus TPC ( korosho na sukari). Piga ua serikali haiwezi kusambaza mafuta hata mkoa mzima tu wa Dar. Hata hapo Dodoma japo ni chimbo lao hawataweza kufika Dumila. Wataishia hapo Bungeni tu. Mark my words.
Mkuu mm nipo kilosa, shida ya huku ni moja shell mafuta wanapima ya 5000 tu, kwa wenye magari sijui lakini Bodaboda na wateja wengine wa mafuta hauekewi mafuta zaidi ya hiyo hela, na hilo tatizo halikuwepo kabla ya mafuta kushuka bei so that means kuna tatizo Lipo
 
Mkuu mm nipo kilosa, shida ya huku ni moja shell mafuta wanapima ya 5000 tu, kwa wenye magari sijui lakini Bodaboda na wateja wengine wa mafuta hauekewi mafuta zaidi ya hiyo hela, na hilo tatizo halikuwepo kabla ya mafuta kushuka bei so that means kuna tatizo Lipo
Wanadhani mafuta ni makinikia
 
Polisi jijini Dsm imewakamata wakurugenzi wakuu wa kampuni za mafuta za Puma, Total na Oryx waliokuwa kwenye kikao cha kibiashara.
Kadhalika polisi wanamsaka mkurugenzi mkuu wa Lake Oil ili aunganishwe na wenzake.

Imeelezwa wakurugenzi hao wanadaiwa kuvuruga mfumo wa usambazaji mafuta nchini.

Chanzo: ITV habari!
Microsoft Corp v Commission T-201/04 is a case brought by the European Commission of the European Union against Microsoft for abuse of its dominant position in the market. Wikipedia
 
Ninunue mafuta kwa 2300 kwa lita afu uje unilazimishe niuze kwa 1500? Omba yasikukute. Mnashabikia tu kwa vile hela sio zenu. Laiti kama ingekuwa ni wewe
 
Ni wakati sasa serikali kutumia shirika la TPDC kuagiza na kuuza mafuta ili kuondoa unyonyaji wa hawa wafanyabiashara binafsi..
 
Una uhakika na ulichokiandika!?

Jamaa hajui hata anayepanga bei ni EWURA. Ninadhani kuna nia mbaya dhidi ya makampuni haya. Kampuni za mafuta zinapata hasara sasa kwa sababu ya kuanguka kwa demand - huenda kampuni hizi hazijafanya importation ya mafuta (kukwepa hasara) na hivo kupungua kiasi cha mafuta nchini. Sijui importer analazimishwaje kufanya biashara!!
 
Back
Top Bottom