Hatua na ushauri upatikanaji wa mafuta na kuimarisha shilingi yetu

Hatua na ushauri upatikanaji wa mafuta na kuimarisha shilingi yetu

MTANZANIA620

Senior Member
Joined
Jun 20, 2023
Posts
101
Reaction score
112
Tanzania ina idadi ya vituo takribani 2,500 ambavyo kwa siku moja vinauza mafuta lita milioni 11-15.

Vituo hivi vya mafuta vimegawanyika katika aina kuu tatu:-

1. Vituo vidogo vya watu binafsi ambavyo hununua mafuta kwa waagizaji wakubwa toka nje (Dealer Owned Dealer Operated - DODO) mfano Bukoba Oil, ATN, Lexo, nk

2. Vituo vinavyomilikiwa na kampuni ambazo ni waagizaji wakubwa wa mafuta na wanaviendesha (Company Owned Dealer Operated - CODO) kama vile Oilcom, Lake Oil, Total, Gapco nk

3. Vituo vinavyomilikiwa na kampuni waagizaji wakubwa wa mafuta wenye depot lakini vimekodishwa na vinaendeshwa kwa mikataba na watu wengine (Company Owned Company Operated - COCO) kama vile Total, Oryx, Puma nk

Changamoto kubwa ni waagizaji wakubwa kutokua na mikataba ya kibiashara na hivi vituo vya watu binafsi ili kuwapa uhakika wa wanunuzi wa mafuta pale wanapoagiza kutoka nje hali inayofanya wabahatishe tu kwa kuleta mafuta ya kukidhi vituo vyao na kidogo watakayouza kwa watakaohitaji. Muhimu serikali kuliona hili.

Jingine muhimu ambalo serikali inafanya kusaidia kukabiliana na mabadiliko ya mara kwa mara kwa bei ya mafuta katika soko la dunia pamoja na uimara wa shilingi yetu dhidi ya dola ya Marekani pamoja na ushauri wa wazalendo ni:-

1. Tanzania imeingia mikataba na Nchi wazalishaji wa mafuta ili kusaidia kupata mafuta hayo kwa uhakika na bei nafuu bila kupitia kwa watu wa kati (makampuni)

2. Tanzania kuingia mikataba na Nchi wazalishaji wa mafuta kujenga reserve ya mafuta hapa nchini ili kuzifanya nchi zinazotuzunguka pamoja na sisi wenyewe kuagiza mafuta yao kutokea hapa hali itakayotupa uhakika wa fedha za kigeni na uhakika wa mafuta nchini.

Namba 1&2 zinatuwezesha kukabiliana na geopolitics za mataifa yanayozalisha mafuta kama vile umauzi wa kupunguza uzalishaji na uingizaji wa mafuta kwenye soko la dunia ili kutengeneza uhitaji na kuongeza bei pamoja na uhakika wa meli za usafirishaji hali inayotoa uhakika wa usafirishaji hivyo kupunguza gharama za kusafirisha mafuta hayo kwani kwa sasa Taifa lenye idadi kubwa ya meli za usafirishaji wa mafuta ni Urusi na imepunguza meli 250 kwenye soko hali iliyoleta uhitaji na kuongeza gharama za usafirishaji wa mafuta.

3. Tanzania kuanzisha mfuko wa maendeleo ya nishati ambao unaweza kutumika pia kuongeza ruzuku pale mafuta yanapokua yamepanda ili mafuta yapatikane kwa bei nafuu vivyo hivyo kwenye gesi.

4. Tuwekeze kwenye maeneo yatakayoongeza mauzo yetu nje ya nchi ikiwemo kuongeza uzalishaji wa mazao yetu ya biashara kama vile korosho, katani, kahawa, chai, pamba na tumbaku pamoja na mazao ya bustani. Aidha tuwekeze kwenye viwanda vinavyoongeza thamani mazao haya ili kunufaika zaidi na kuongeza ujazo/mapato ya fedha zetu za kigeni.

5. Tuongeze uwekezaji kwenye mazao na bidhaa tunazoweza kuzalisha wenyewe badala ya kuendelea kuagiza toka nje kama vile ngano, sukari, mafuta ya kupikia nk Itapunguza matumizi ya fedha za kigeni kuagiza bidhaa hizi.

6. Tuharakishe uwekezaji kwenye vituo vya kujaza gesi kwenye magari, bajaji, pikipiki ili tuhamasishe matumizi ya gesi na kupunguza matumizi ya mafuta ikiwemo kwenye magari ya serikali. Lengo kupunguza matumizi ya fedha zetu za kigeni kuagiza mafuta.

7. Tuimarishe viwanja vyetu vya ndege na bandari zetu ili kuchangia zaidi katika uchumi ikiwemo kuvifanya kuwa vituo bora vya usafirishaji wa mizigo aina zote ikiwemo mazao ya kilimo, mifugo na uvuvi. Itatuongezea upatikanaji wa fedha za kigeni.

8. Tayari Tanzania imeanza ujenzi wa bandari ya uvuvi hali itakayochochea shughuli za uvuvi katika bahari kuu. Fursa inayoweza kutuongezea fesha za kigeni.

Mbele iko sawa...😀

MZALENDOWAZALENDO40

(Picha zote ni ujenzi wa bandari ya Uvuvi Kilwa shilingi bilioni 266 kazi imeanza na inaendelea)

IMG-20230906-WA0030.jpg
IMG-20230906-WA0032.jpg
 
Back
Top Bottom