Kama ulikuwa hujui hii ndio mikataba ya Utafutaji wa mafuta na gesi na ugawanaji mapato

Meneja Wa Makampuni

JF-Expert Member
Jul 7, 2020
6,315
8,214
Dhana ya Mkataba wa Utafutaji wa mafuta na Ugawanaji Mapato - wazo la nchi la utafutaji wa mafuta na gesi na mgawanyo wa mapato na makampuni kama sehemu ya biashara lilianzishwa kwenye miaka ya 1950. Kwanza kabisa, wazo hili lilianzishwa Indonesia mwaka 1966. Mikataba ya Utafutaji wa mafuta na Ugawanaji Mapato inatumika katika zaidi ya nchi 40 duniani, ikiwemo Tanzania.

Mikataba hii ni moja kati ya njia mbili ambazo kampuni hupata haki ya kutafuta mafuta na gesi. Njia nyingine ni mfumo wa kodi, miradi inakatwa kodi kutokana na sheria za nchi, lakini hii inafanyika sehemu ambayo mikataba ya utafutaji wa mafuta na ugawanaji mapato haitumiki, na serikali inakuwa si miongoni mwa wenye mradi. Kuna tofauti nyingi kati ya njia hizi mbili.

Mkataba wa Utafutaji wa mafuta na Ugawanaji Mapato ni nini?
Kama jina linavyojieleza, ni mkataba kati ya nchi na makampuni binafsi ya mafuta. Kampuni ya mafuta inapewa leseni kwa sharti kwamba-ikifanikiwa kupata mafuta/gesi-itagawana mapato na nchi mwenyeji.

Nchi inahusika kwenye mkataba moja kwa moja au kupitia kwa kampuni ya mafuta ya serikali. Mara nyingi nchi huwa na haki ya kurudisha baadhi ya mapato. Kampuni ya mafuta ya kigeni inaleta wataalamu na uwezo wa kifedha, na hubeba gharama zote za utafiti. Kama utafiti huo hutofanikiwa basi nchi haipati hasara yoyote lakini, utafiti huo ukifanikiwa, nchi inakuwa ni miongoni mwa wenye mradi huo.

Kwenye Mkataba wa Utafutaji wa mafuta na Ugawanaji Mapato, kampuni ya utafutaji mafuta huwa inapewa kipaumbele cha kurudisha gharama zake za uwekezaji. Kitakachobakia hugawanywa kwa wahusika kwenye mkataba husika. Na itahusisha, mrahaba, kodi na uzalishaji.

Muundo wa Tanzania
Sekta ya mafuta na gesi Tanzania ni mchanganyiko wa mitindo mikuu miwili, ambayo imeibuka kutoka kwenye utamaduni kuliko sheria. Kwenye sheria inayosimamia maswala yote ya utafutaji na uzalishaji wa mafuta na gesi ya mwaka 1980, mwenye leseni anatakiwa kulipa mrahaba na kodi. Mwaka 1969 Shirika la maendeleo ya petroli Tanzania (TPDC) lilianzishwa. Kama kampuni binafsi ya kutafuta mafuta na gesi ikipewa leseni ya kutafuta mali ghafi ya mafuta, kwa uhalisia,leseni hiyo inakuwa imetolewa na serikali kwa Shirika la maendeleo ya petroli Tanzania (TPDC): Shirika la maendeleo ya petroli Tanzania ndio anakuwa mmiliki wa leseni hiyo na anatakiwa kutoa na kulipa mrahaba na kodi serikalini. Uhusianao kati ya Shirika la maendeleo ya petroli Tanzania (TPDC) na kampuni binafsi ya kutafuta mafuta na gesi unaongozwa na Mkataba wa Utafutaji wa mafuta na Ugawanaji Mapato (PSA). Kwa hiyo muundo wa Tanzania haungozwi na sheria za mkataba wa Utafutaji wa mafuta na Ugawanaji Mapato ila mkataba wa kibiashara kati ya wahusika (mapato hayagawanywi kati ya kampuni binafsi na serikali bali ni kati ya kampuni binafsi na Shirika la maendeleo ya petroli Tanzania TPDC). Kuna vizazi vitatu vikuu vya mapatano ya biashra: Miundo ya Mikataba elekezi ya Utafutaji wa mafuta na Ugawanaji Mapato (MPSA) ya 2004, 2008 na 2013. Kwa vile Mkataba wa Utafutaji wa mafuta na Ugawanaji Mapato ni wa kibiashara kati ya Shirika la maendeleo ya petrol Tanzania (TPDC) na kampuni binafsi ya mafuta, mfumo huu unaruhusu mabadiliko. Hii inaeleza utofauti mpana kama inavyooneka katika vipengele vya Mkataba wa Utafutaji wa mafuta na Ugawanaji Mapato.

Uhusiano huu unaonekana hapa chini:

Vipengele muhimu ndani ya mkataba wa Utafutaji wa mafuta na Ugawanaji
Mapato

(a) Gharama za Mafuta (Cost Oil):
Kama ilivyotajwa, kampuni ya mafuta ina haki- ya kurudisha kutoka kwenye uzalishaji gharama za uwekezaji. Zinarudi vipi, kuna utofauti: Mikataba ya Utafutaji wa mafuta na Ugawanaji Mapato ya mwanzoni kabisa ilikuwa inaruhusu uzalishaji kwanza kulipa gharama za utafutaji na uzalishaji. Lakini miradi mikubwa au ghali wakati mwingine huchukua mda mrefu kulipa gharama za uwekezaji na hii ina maana kuwa nchi haipati mapato kutoka kwenye hii miradi kwa mda mrefu. Ni kawaida kwa Mkataba wa Utafutaji wa mafuta na Ugawanaji Mapato kutoa sehemu ya uzalishaji kulipa gharama za mradi na kitakachobaki kugawanywa kati ya wahusika. Hii inafanya serikali kupata mapato mapema. Kumbuka kwamba mwekezaji hufidia gharama za utafutaji mafuta ili kufidia mtaji wake- hii sio faida. Kwa hali halisi (kwa kesi ya Tanzania), mwekezaji anabeba gharama zote za undelezaji mradi na analipwa kutokana na uwekezaji huu kwenye uzalishaji.

(b) Mirahaba (Royalties):
Mrahaba ni aina ya „kodi ya pango‟ –kodi ya nyongeza kwenye uzalishaji. Kawaida hutolewa „mkato wa juu‟ – maana yake ni tozo la kwanza kufanyika katika kukokotoa mtiririko wa fedha. Mrahaba huwa unatolewa kama „namna ya mali‟ (in kind) (yaani, gawio la uzalishaji) ama, nchi yenyewe itakavyochagua, pesa taslimu (in cash) sawa na bei ya mauzo ya gawio la mrahaba wa uzalishaji wa nchi. Iwe mrahaba unatolewa kama namna ya mali (in kind) au pesa taslimu (in cash) haileti tofauti kweye mtiririko wa fedha wa mwekezaji. Pia, kuna tofauti kati ya Mikataba ya Utafutaji wa mafuta na Ugawanaji Mapato jinsi mirahaba inavyotolewa na inakoenda: Nchi zingine husisitiza mirahaba ilipwe moja kwa moja serikali kuu na mikataba mingine inataka mirahaba kugawanywa kati ya serikali kuu na mikoa amabayo uzalishaji unafanyika.

(c) Mafuta ya faida (Profit Oil):
Mafuta yanayobakia baada ya mirahaba na gharama kulipwa (yanaitwa mafuta ya faida) yanagawanywa kati ya kampuni ya mafuta na nchi kulingana na kanuni mliokubaliana awali.
Kawaida, jinsi unavyozalisha kwa wingi, ndio wingi wa nchi kupata gawio katika kila ngazi (tranche) ya uzalishaji. Pia, kuna utofauti mkubwa – kunawezekana kukawa na ngazi (tranches) chache au nyingi; au ngazi zinaweza zikawa nyembamba au pana.

(d) Kodi (Income Tax):
Mwisho, kuna suala la kodi kwenye mafuta ya faida. Hii kodi inatolewa na kampuni ya mafuta ya taifa kwa niaba ya kampuni binafsi ya mafuta, ili kusiwe na mgongano wa kifedha kwenye kampuni binafsi ya mafuta (ndani ya mchakato huu , inachuliwa kuwa kodi imetolewa ndani ya Mkataba wa Utafutaji wa mafuta na Ugawanaji Mapato). Njia nyingine, kampuni binafsi ya mafuta inatakiwa kulipa kodi moja kwa moja serikalini.

Mtiririko wa fedha hizi ulivyo unaoneshwa hapa chini:

Mfano unaoonesha jinsi vipengele vya Mkataba vinavyofanya kazi kwa pamoja:

Chukulia kuendeleza mradi wa pipa milioni 50. Kwa bei ya $50 kwa pipa mapato kutokana na uzalishaji ni $2.5 bilioni (puuza mda wa thamani ya pesa “TVM”). Fikiria pia, gharama za utafiti, uhakiki, kuendeleza na uzalishaji wa huu mradi ni $10 kwa pipa moja. Kutoa mrahaba kwanza, chukulia ni 12.5%, inamaanisha kuwa serikali inapokea $312.5 milioni kutoka kwenye mradi. Hii inabakiza chini ya $2.2 bilioni tu ya kugawanywa.

Kwa gharama ya $10 kwa pipa, kampuni binafsi ya mafuta lazima irudishe $500 milioni ili kurudisha fedha zake alizowekeza kwa hatari au alizo hatarisha katika uwekezaji huo. Hii inabakiza chini ya $1.7 bilioni ya kugawanywa Zaidi.

Chini ya Mkataba wa Utafutaji wa mafuta na Ugawanaji Mapato wa sasa (Mkataba wa Utafutaji wa mafuta na Ugawanaji Mapato wa sasa wa mfano wa 2013), Shirika la maendeleo ya petroli Tanzania (TPDC) inaweza kupata japo 70% ya uzalishaji, sawa na chini ya $1.2 bilioni. $500 milioni iliyobakia inachukuliwa na kampuni binafsi ya mafuta.

Mwisho, kampuni binafsi ya mafuta na Shirika la maendeleo ya petroli Tanzania (TPDC) lazima zitoe kodi kutoka kwenye mapato yao. kama $150 milioni (kwa kampuni binafsi) na $ 370 milioni (kwa Shirika la maendeleo ya petroli Tanzania) Katika mfano huu, makadirio ya sehemu ya faida inayobaki kwa kampuni binafsi ni $350 milioni (kama. 18%), na Shirika la maendeleo ya petroli Tanzania inabaki na $830 milioni (kama. 42%) na sehemu inayobaki kwa serikali ni $812 milioni (kama. 40%). Kwa ujumla, kwenye huu mfano serikali inachukua 82%.

Mfano hapo juu unaoneshwa katika jedwali hapa chini:
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom