Wakulima waelimishwe waache kuchoma mabaki ya mazao wakati wa kuandaa mashamba

Freed Freed

JF-Expert Member
Jun 27, 2017
6,230
6,471
Kumekuwa na utamaduni wa kale wa wakulima kuchoma mabaki ya mazao kwa kigezo Cha kujiandaa na msimu mpya wa kilimo.

Mabaki hayo ni pamoja na mabua, magunzi na hata nyasi kavu. Hii ni MBOLEA YA MBOJI au composit Manure. Inarutubisha udongo hapo baadae na kupunguza umri wa aridhi yako kuchoka au kuongeza umri wa aridhi yako kuendelea kuwa na rutuba asili.

Cha ajabu maafisa Kilimo wapo ktk baadhi ya vijiji na kata lakini zoezi hili la kuchoma takataka hizi bado linaendelea miaka nenda rudi. Kinachopaswa kuobdolewa ni vichaka tu mashambani. Mimea mimgine ikikauka itaoza na kuwa mbolea.

Wizara ya Kilimo toeni ELIMU.
 
Back
Top Bottom