Mbunge Condester Sichalwe: Wananchi (wakulima) undeni vikundi vya ushirika ili mkopesheke kwenye mabenki kwaajili ya msimu ujao wa kilimo

Ojuolegbha

JF-Expert Member
Sep 6, 2020
741
479
Mbunge wa Jimbo la Momba Mkoa wa Songwe Mhe. Condester Mundy Michael Sichalwe tarehe 22 Julai, 2023 ameendelea na ziara katika Kijiji cha Yala na kuzungumza na wakulima wa Kijiji hicho.

Condester Sichalwe amewashauri wananchi kuunda vikundi vya ushirika ili wavitumie kama dhamana ya kuchukua mikopo kutoka benki kwani wananchi wengi wamekuwa hawakopesheki kwa sababu hawana mali za kuweka dhamana kwaajili ya kukopa na wengine hawana mashamba yenye ukubwa wa Hekari 50.

Condester Sichalwe amesema kuwa Wataalam kutoka Wizara ya Kilimo watafika katika Vijiji vyote vya Jimbo la Momba kwaajili ya kutoa elimu kuhusu mambo yote ya Kilimo ili wakulima wa Kijiji cha Yala na vijiji vyote wawe na Kilimo chenye tija.

Akizungumza katika Mkutano wa hadhara wa wananchi, Afisa Kilimo katika Kijiji cha Yala amesisitiza wananchi kutumia na kulima Kilimo chenye tija ili kuwa na mazao mengi huku akiainisha jaina ya mbolea na aina ya mbegu za kutumia zinazofaa kwa mkulima zinazoendana na jiografia ya eneo husika na hali ya hewa.

Condester Sichalwe amewasisitiza Mabalozi wa Vitongoji na Wenyeviti wa Vijiji kuhakikisha wanawatambua watu wote wanaokuja kuishi ndani ya maeneo yao ili iwe rahisi kutambua nani mgeni na nani mwenyeji huku akiwasisitiza kufikisha taarifa kwa wananchi wao.

Condester Sichalwe amesema Serikali imejitahidi kutekeleza majukumu yake ikiwemo Kusambaza Umeme Vijijini (REA), Hospitali, Shule na Skimu za Umwagiliaji huku akiwataka wananchi kuzitumia fursa zinazoletwa na Serikali kwa manufaa yao na nchi.

Wananchi wa Kijiji cha Yala wamemshukuru Mbunge wa Mbomba na Serikali kwa kujenga Madarasa Mawili na Ofisi, ujenzi wa soko, Skimu ya umwagiliaji, umeme kuwafikia Vijijini huku wengi wakiiomba Serikali kuwasaidia umaliziaji wa Zahanati, ujenzi wa nyumba za Walimu na kuajiri Walimu ili kuondoa upungufu wa walimu katika shule.

Diwani wa Viti Maalum amemshukuru na kumpongeza Mbunge wa Jimbo la Momba Mhe. Condester Sichalwe kwa kuwachangia Shilingi Milioni 2 (2,000,000) kwaajili ya ujenzi wa Zahanati na soko.

Diwani wa Kata ya Chitete amesema kuwa Serikali imepeleka Shilingi Milioni Hamsini (50,000,000) kwaajili ya ujenzi wa Zahanati ya Kata, na ujenzi wa Shule mpya Namingong'o na Yala.

Mwisho, Mhe. Condester Sichalwe amesema atawaleta watu wa TASAF Kijijini hapo huku akisema atafuatilia kwanini wananchi wamechangishwa fedha za NIDA na kujua ni lini vitambulisho vyao vitaletwa.

Condester Sichalwe amesema ataendelea kufuatilia suala la kuwa na walimu wa kutosha na kuwasisitiza Madiwani na viongozi wa Vitongoji kusimamia vizuri fedha za miradi inayoletwa na Serikali kwa ajili ya kuboresha huduma.

20230725_202029.jpg
 
View attachment 2699025
Ww ni chawa wake maana kwenye nchi hii hakuna anayeonekana lofa kama mkulima Nani anataka kulima kwenye nchi hii? Acheni propoganda kwenye mambo muhimu ndg zangu ww mwenyewe mtoa post tuambia unajishughulisha na kilimo gani je upo front kwenye kazi ya yako?

Je changamoto za kilimo za kilimo wazijua ndg yangu?
 
Afadhali umeweka na picha. Sijamuona siku nyingi huyu madam. Ushirika si tu kwa ajili ya mikopo, zaidi hasa ni katika kujitete. Hata wakulima wa maharage wanahitaji kuungana ili kuwa na nguvu ya kujitetea.
 
Ww ni chawa wake maana kwenye nchi hii hakuna anayeonekana lofa kama mkulima Nani anataka kulima kwenye nchi hii? Acheni propoganda kwenye mambo muhimu ndg zangu ww mwenyewe mtoa post tuambia unajishughulisha na kilimo gani je upo front kwenye kazi ya yako?

Je changamoto za kilimo za kilimo wazijua ndg yangu?
Sasa Madam Condester si ndiyo anawaambia waungane ili waachane na ulofa.
 
Back
Top Bottom