Kenya imekodi mashamba ya kulima mahindi Zambia. Wakulima wa Tanzania jiandaeni kwa kilio cha kukosa soko

ChoiceVariable

JF-Expert Member
May 23, 2017
43,051
49,735
Serikali ya Kenya na Zambia zimeingia makubaliano ya Zambia kuikodisha Kenya mamilioni ya ekari za mashamba Kwa Ajili ya Kilimo Cha mahindi na hivyo Kuepukana na njaa ya mara Kwa mara..

Hoja yangu Kwa nini Serikali yetu Kupitia Wizara ya Kilimo isiingie makubaliano na Kenya ya kuwatengea kiwango Fulani Cha nafaka Kila mwaka Kwa Ajili hiyo Kupitia Bodi ya mazao mchanganyiko na NFRA?

Sasa mambo ya ujasusi wa kiuchumi hapa Tanzania hufanyika wapi ikiwa jambo dogo kama hili inashindikana? Hivi ujasusi wa Kitanzania ni Kwa kujihami au kutafuta masoko?

Kwa hatua hii ya Kenya tayari tumeshapoteza soko la Mahindi la Kenya Kwa wakulima Wetu Kwa kuwanufaisha Zambia..

Wakulima na Vijana huko kwenye BBT mjiandae Kisaikolojia maana Viongozi wa Tanzania wengi wao hawaaminiki..

Mwisho Ushauri Kwa Serikali,Ili kujihakikishia soko Kwa Sasa ni Bora Sasa Serikali ianze kuhamasisha value addition yaani kuuza unga badala ya nafaka na pia kukuza sekta ya mifugo ya Kisasa kama ng'ombe, nguruwe,kuku nk Kwa Ajili ya exports Ili Sasa mazao ya wakulima Wetu yapate soko Kwa kuwa chakula Cha mifugo,kinyume na hapo Jiandaeni Kwa bei za 20,000 Kwa gunia msimu ujao..

 
Kwani wakilima WaZambia wenyewe au waKalima waKenya tofauti ni nini hasa? Au we unadhani atatoka mtu Kenya kwenda hadi Zambia na Trekta lake akalime? Ni hao hao waZambia ndio watalima na kwa kutukia nyenzo zao huko huko, kwahiyo hapa ni kwamba Kenya ananunua mahindi kabla hayajalimwa. Lengo kuhakikisha kwamba wanayapata kwa wakati na kwa bei nafuu. Ni kama mtu anayeweka order ya kitu ambacho hakijafika dukani bado, ili kikifika apewe priority.
 
Kwani wakilima WaZambia wenyewe au waKalima waKenya tofauti ni nini hasa? Au we unadhani atatoka mtu Kenya kwenda hadi Zambia na Trekta lake akalime? Ni hao hao waZambia ndio watalima na kwa kutukia nyenzo zao huko huko, kwahiyo hapa ni kwamba Kenya ananunua mahindi kabla hayajalimwa.
Una akili kisoda hata huelewi logic behind
 
Sidhani kama ni jambo la hatari kwa wakulima wetu. Kenya kama taifa ndio limeingia makubaliano, hivyo ni kuhakikisha kunakuwa na food security nchini;

Maswali ya kujiuliza hapa ni;
a) Je, gharama za uzalishaji za kiserikali huwa zina akisi gharama halisi ya uzalishaji?

Jibu siku zote ni hapana. Kwenye serikali yeyote duniani huwa kuna existence of bureaucracy inayosababisha kupanda gharama ya uzalishaji. Pia wenzetu rushwa lawatafuna. So it's an opportunity for government officials making more money.

b) Mbali na faida ya uzalishaji, yaani kutumia inputs za ndani; Je serikali ya Zambia wanufaika na nn kingine? Taxation.

Kupunguza urefu wa maneno, serikali ya Kenya haitoweza kuoffer competitive prices kwa kuwa gharama za uzalishaji lazima iwe juu.

Hivyo, sidhani kama kuna tishio lolote kwa wakulima wetu, ila kuwe na diversed market. Iisiwe Kenya tu, nadhani wizara tuangalie hivi kiundani
 
Sidhani kama ni jambo la hatari kwa wakulima wetu. Kenya kama taifa ndio limeingia makubaliano, hivyo ni kuhakikisha kunakuwa na food security nchini;

Maswali ya kujiuliza hapa ni;
a) Je, gharama za uzalishaji za kiserikali huwa zina akisi gharama halisi ya uzalishaji?

Jibu siku zote ni hapana. Kwenye serikali yeyote duniani huwa kuna existence of bureaucracy inayosababisha kupanda gharama ya uzalishaji. Pia wenzetu rushwa lawatafuna. So it's an opportunity for government officials making more money.

b) Mbali na faida ya uzalishaji, yaani kutumia inputs za ndani; Je serikali ya Zambia wanufaika na nn kingine? Taxation.....

Kupunguza urefu wa maneno, serikali ya Kenya haitoweza kuoffer competitive prices kwa kuwa gharama za uzalishaji lazima iwe juu..

Hivyo, sidhani kama kuna tishio lolote kwa wakulima wetu, ila kuwe na diversed market... isiwe Kenya tu, nadhani wizara tuangalie hivi kiundani
Muwe mnasoma kabla ya kuandika.Kama sio shida soko kubwa la Mahindi ya Tanzania ni wapi Sasa kama sio Kenya?

Yaani unachekelea Kwa kuporwa soko? Nimetoka way forward lakini watu Kwa kuwa hamjui hata maana ya kulima basi mnaropoka tuu.
 
Soma uelewe, soko ni huria. Hakuna aliekupora. Kuna document yeyote ya kuhalalisha kuwa kenya ni soko la Tanzania?

Kwani, ni mara moja Tanzania imechukua soko la wengine?

Hoja yangu juu ni; haijalishi wanatumia ardhi gani. Bei ikiwa rafiki lazima iuze, Kenya bei lazima iwe juu.
 
Back
Top Bottom