Wakristo mjitafakari kwenye suala la mahari, mnawakosea sana binti zenu. Kilichotokea hivi karibuni kwa jamaa yangu kina funzo

Rafiki yangu(37) ni single father with 3 kids, ana mchumba wake mganda ambaye naye ni single mother(37 yrs) with one kid. Alikuwa rafiki yake wakati wakisoma chuo, wakaja kukutana tena miaka kadhaa baada ya ku graduate, jamaa anaishi Dar, mrembo anaishi Kampala wakaanzisha uhusiano.

Muda wa kwenda kutoa mahari ulikuwa mwezi uliopita. Nilikuwa mmoja katika ujumbe uliyoongozana na rafiki yangu na matchmaker(mshenga) wake. Wakati wa kunegotiate mahari wazazi wakaanza na 15 million Ugandan ambayo ni kama milioni 9 ya Tanzania(walitaja idadi ya ng'ombe then ikawa converted to cash).

Tukakomaa wakashusha mpaka milioni kumi ya Uganda. Tutakomaa tana wakashusha mpaka milioni tano ya Uganda. Mwisho kabisa wakakomea shilingi milioni nne na point kadhaa ya Uganda ambayo ni sawa na milioni tatu ya Tanzania.

Hapo wakasema haipungui hata mia. Tukaomba tupewe muda tukatafakari kisha tutatoa taarifa ni lini tutarejea tena ukweni kukamilisha hiyo mahari. Kumbuka hapo tumefikia hotelini. Basi tulipoenda kujadiliana tukamuuliza muoaji kama bajeti yake ina mruhusu kulipa milioni tatu cash akasema no way out hawezi kulipa mahari yote hiyo.

Akasema alitegemea wangesema milioni moja halafu yeye angetoa laki tano au saba huku akitoa ahadi ya kumalizia mahari iliyo baki(waganda hakunaga kubakiza mahari). Wakati hapa Tz kutokumalizia mahari ni heshima kubwa sana kwa wakwe, kwasababu kwanza, inaonyesha kwamba bibi harusi sio bidhaa unayo weza kuinunua dukani na kwamba wazazi wa bibi harusi wamekutunuku binti yao ukaanzishe nae familia. Lakini pili Inaonyesha kwamba wewe muoaji unampenda sana mkeo kiasi kwamba haupo tayari kusubiri mpaka upate mahari kamili.

Mshenga akamuuliza bwana harusi. Hauna alternative mahali kwingine, yaani hauna mchumba mwingine?
Jamaa akajibu nina mchumba mwingine yupo Tanzania ila yeye ni muislamu na kwao wanataka tufunge ndoa ya kiislamu(mshenga akajibu nilitaka kushangaa unakosaje alternative?!).

Kisha akamuuliza. Upo tayari kufunga ndoa ya kiislamu? Jamaa akajibu yupo tayari. Mshenga akajibu tunasubiri nini? Mshenga akaenda kutoa taarifa ukweni kwamba tunarudi Dar kujipanga na tutarejea tutakapo kuwa tayari.

Jamaa karudi Dar ndani ya hizo wiki mbili kavuta jiko na harusi ikafanyika kwa gharama ya kawaida sana, na mtoto mwenyewe mbichi kabisa ndiyo kwanza kamaliza form four(anaweza kuwa bado hajawa dis flowered).

Baada ya kuoa jamaa kamjulisha mchumba wake wa uganda kwamba hayupo tena interested na ndoa kwa sababu hizo gharama haziwezi na kwamba ameamua kuoa sehemu nyingine. Mwanamke wa kiganda kachanganyikiwa sasa hivi anawalaumu wazazi wake tu.

Wakristo hizo zama za wanaume kutoa mahari za mamilioni hazipo tena. Jifunzeni kwa waislamu, mnawakosesha binti zenu ndoa kwa sababu ambazo hazina msingi. Kwanza karne hii ukiona mtu "amepandwa na kichaa " cha kutaka kuoa unapaswa kumpa mke haraka kabla kichaa hakija toweka, ili kichaa kiondoke tayari akiwa na mke ndani ndiyo akumbuke 'kumbe mimi fala hivi'.

NB: Kwa sababu ya complications zake, familia nyingi za kikristo huwa zina experience ndoa chache sana ikilinganishwa na familia za kiislamu. Dini ya kiislamu imerahisisha sana suala la ndoa. Matokeo yake familia nyingi za kikristo huwa hazifahamu saikolojia siasa za waoaji.

Ni hivi muoaji anapo kuja kwenye familia yako, usifikiri hajaona mwanamke mwingine au hana option nyingine. Most of the time muoaji anapofikia hatua ya kuja kujitambulisha nyumbani kwenu tayari anakuwa na option zingine kama mbili, tatu au hata nne.

Nikija kwenye familia yako kuchumbia, halafu ukaniletea complications ngumu, mimi nitakacho kifanya nita kuachia binti yako nitaenda kwenye familia ambayo haitaniwekea complications ngumu.

Ninapokuja kwenye familia yako usinichukulie kwanza kama mtu ambae ninataka kumuoa binti yako, nichukulie kama mtu ambae nimekuja kutazama kama familia yako ina complications au la!
Tatizo wazazi wengi kutokana na umasikini au utajiri wao wanawapangia watu mahari nyingi ili wajikwamuwe kidogo.Sisi kwetu tulimwambia bint yetu we wamjuwa mumeo uwezo wake upange mahali wewe isije mtu akakimbia kisa eti hawezi kulipa mali.Hata mimi ukinikomoa nasepa.Bora nifanye biashara au kulima.
 
asilimia 100% upande wa wakristo ndio umeleta ugumu sana maswala ya ndoa japo kutojitafakari.

Haya mambo yanapelekea wakristo wengi kushindwa kuoa au kuolewa.

kuanzia ghalama za mahali mpaka sheree.

na tunajikuta wengi wetu tukiishi unyumba hata ndoa kufanyika.

ukitaka kufahamu we nenda makanisani yani unakuta familia lakini baba na mama hawakufunga ndoa na ndo wanafunga ndoa
 
Nakazia
 
Mkuu so unataka mtu aende ukweni amevaa ndala?

Hiyo kumpiga mkwe mtarajiwa mahari ya bei kubwa kuna tofauti gani na machinga kumtajia mnunuaji bei kubwa kwa sababu ya muonekano wa mnunuaji? Sio maadili hata kidogo.

Hiyo ya kusema mahari ni makubaliano Kati ya mwanamke na mwanaume ipo kwa waislamu tu hiyo mkuu. Wakristo hawanaga hiyo
ACHA ubishi wewe makubaliano ya mahali yanaanzia ktk mazungumzo ya mwanaume na mwanamke then mwanamke anaenda kwao anasema kutokana na hali aliyonayo mchumba wangu mtarajiwa atamudu mahali kias fulani... Wazaz hawawez kutaja mahali bila kujua uwezo wa mwanaume... Huyo rafiki yako itakua alikua anaigiza maisha kwa huyo mwanamke kujionyesha ana pesa ili amu win mwanamke...
 
kama ni hivyo basi hawa wanawake wanaomkomoa mwanaume aliyeonyesha niya ya kumuoa ni mapoyoyo kwa kama wao ndiyo hupanga mahali basi
 
ACHA ubishi wewe makubaliano ya mahali yanaanzia ktk mazungumzo ya mwanaume na mwanamke then mwanamke anaenda kwao anasema kutokana na hali aliyonayo mchumba wangu mtarajiwa atamudu mahali kias fulani... Wazaz hawawez kutaja mahali bila kujua uwezo wa mwanaume... Huyo rafiki yako itakua alikua anaigiza maisha kwa huyo mwanamke kujionyesha ana pesa ili amu win mwanamke...
Hii ni kwa waislamu sio wakristo. Jamaa hela anayo hana njaa. Usicho kifahamu ni kwamba ukiwa una shika hela unakuwa na.nidhamu ya kuitumia pesa yako. Hutumii pesa hovyo kwa sababu unayo.

Unaanzaje kumuigizia maisha mwanamke single mother mwenye miaka 37 ili umu win moyo wake?

Jamaa anasema alizungumza na mwanamke before kuhusu hicho unacho kisema mwanamke akamwambia yeye hana mamlaka kuhusu mahari .

Jamaa alimwambia mwanamke aongee na mama ake mama aongee na baba, apozewe kwenye mahari na point ya jamaa kwa mwanamke ni kwamba hiyo mahari hata ikiwa nyingi kiasi gani yeye mwanamke na mama ake hawawezi kupata chochote italiwa na baba wadogo/wakubwa etc.

Inawexekana hiyo mahari waliyo taja ndio wame mpunguzia labda kwa.sababu wamejua jamaa ana.pesa kwa sababu pesa anayo kweli.
 
Jamaa yupo 37 anaoa "kibinti kibichi" angalau 18-20 hivi. Hapo ndoa itapumulia machine sio mda mrefu. Huyo alikuwa senior bachelor hawezi kuishi na mtoto mdogo.

Kuhusu mahari, ni tamaduni zetu wakristo, japo binafsi sioni umuhimu wa mahari lakini ndio utamaduni hatuna jinsi lazima tuishi hivyo.
 
Mwanamke ndie anaeafiki mume wake apewe mahari kiasi gani kulingana na uwezo wa mume wake,

sasa kama mwanamke wako kakubali uletewe bili ya 15m kama mahari na yeye anakenua tu meno,shida iko kwa wazazi au hata toto lenyewe ni tatzo?

mke wa kweli utamjua tangu mwanzo,akipunguza gharama na akikusaidia kwa namna flani upewe mahari ambayo unai mudu, ila kama mke ndio kakaa pembeni kama bidhaa ipo dukani halafu badae unasepa ndio anajitia kujiliza huo ni unafki.

Nitaendelea kusisitiza swala sio mahari,swala sio wazazi,sio wakristo shida ni hawa tunaotaka kuwaoa hawa wanawake ndio shida inapoanzia hapo.

mwanamke anakuona kabisa maisha yako ya kuchovya chovya ila picha linaanzia kwenye mahari ukitoka kwenye mahari movie linakuja kwenye HARUSI, ukiweza chomoka haya maeneo mawili salama, usimshukuru MUNGU ila mshukuru huyo mwanamke wako.

Hakuna Harusi kubwa yoyote ambayo imefanyika kwa ukubwa ule kama sio "mwanamke hajataka iwe hivyo" hakuna mahari yyte ile iliyolipwa kwa ukubwa ule "kama sio mwanamke ametaka" Diva alisema mahari yake ni 500mil (huo n mfano)

wanawake ndio hufanya mambo yawe mepesi au mambo kuwa magumu, Wanaume kuweni makini sana mnapochagua wanawake wa kuoa,eneo hilo ni la muhimu sana.

Mwanamke utakaemchagua leo ndio atakupa jibu la mahari utakayolipa na harusi utakayoifanya kwenye siku yenu.

Wanawake ni wengi lakini wanawake wakuolewa ni "wachache"
 
Vizuri, ulichokiandika ndicho mleta mada alipaswa kukijua kabla hajaleta uzi wake.
Mapokeo yamewathiri wakristo especially insu ya mahari.
Mbona kwangu mimi naona Mila na desturi za makabila ndio Zina determine mambo ya mahari.
Jamaa yangu alioa binti ya Mchungaji Mlokole, mchungaji huyo alibishana sana na ndugu zake waliotaka amdai kijana mahari ya ng'ombe tano (gharama ya ng'ombe mmoja laki 500,000) Mchungaji alikataa kabisa
Mwishoni alikubali kijana atoe blanket ya bibi na Vicente kwa mashangazi.
Mila na desturi zimetawala sana kwenye mambo haya na wala sio dini.
Je hao waliotuletea Ukristo wana mahari? Ni Tanzania tu?
Ukitaka kuoa Tanzania kila kabila watatoa taratibu zao! Nenda Kate usukumani! Utaulia wakifuata Mila na desturi zao!
Sidhani ni Ukristo mkuu! Ni mila tu!
 
Absolutely true...ukristo Hauna shida kabisa na swala mahari.
Nyei oaneni kwa makubaliano yoyote yale as long as taratibu za kiimani zimefanyika
 
Kwa kifupi alikua anatafuta hausigeli aliyepanda vyeo ,basi wazazi wa mganda walikua sahihi kudai mahari kubwa
Jua tofauti Kati ya kubadili dini kuwa muislamu na kutunga ndoa ya kiislamu, ni vitu viwili tofauti.

Jamaa anataka mke wa kumuangalizia watoto wake.
 
Mimi bado naziheshimu ndoa za waislam very cheap and nzuri na mwanamke kama amekulia kwenye dini hutakuja kujuta sema misimamo yao ya tofauti za didi otherwise i still opting to muslam ladies
Mfumo wao hauthamini sana ndoa unampa mwanaume unafuu aoe wanawake wengine aoendavyo kwa mahari ndogo sana akiwa na elfu 20 aweza oa wake wanne na uislamu unampa mwanamke unafuu wa kuondoka muda wowote kwani alicholipiwa kama mahari ni kama nauli tu ya daladala aweza mrudishia hata kwa kumtupia usoni mwanaume Kuwa mahari ulliipa elfu tano shika elfu tano yako mbwa wewe nimepata mwanaume mwenye pesa mshenzi wewe.

Na mwanaume kuacha kitu kidogo tu after all haikumgharimu kuoa.Hasikii.uchungu wa kuacha mke.Alilipa mahari elfu tano haikuumi kumbwaga

Ukristo mwanamke kutoka ngumu akiwaza mahari aliyotolewa tu kichwa chake lazima kitulie na mwanaume kuacha mke ngumu akiwaza gharama za mahari alizotoa lazima atulie mwenyewe
 
kuolewa kwa kulipiwa mahari kubwa siyo determinant ya upendo ndani ya ndoa........heshima ya mwanamke kwa mwanau,me au mume wake hauiji kwa aina ya harusi au ukubwa wa mahali au kutimiza matakwa ya wazazi wa mwanamke kipindi cha kuoa.
 
Mfumo wao hauthamini sana ndoa unampa mwanaume unafuu aoe wanawake wengine aoendavyo kwa mahari ndogo sana akiwa na elfu 20 aweza oa wake wanne na uislamu unampa mwanamke unafuu wa kuondoka muda wowote kwani alicholipiwa kama mahari ni kama nauli tu ya daladala aweza mrudishia hata kwa kumtupia usoni mwanaume Kuwa mahari ulliipa elfu tano shika elfu tano yako mbwa wewe nimepata mwanaume mwenye pesa mshenzi wewe.

Na mwanaume kuacha kitu kidogo tu after all haikumgharimu kuoa.Hasikii.uchungu wa kuacha mke.Alilipa mahari elfu tano haikuumi kumbwaga

Ukristo mwanamke kutoka ngumu akiwaza mahari aliyotolewa tu kichwa chake lazima kitulie na mwanaume kuacha mke ngumu akiwaza gharama za mahari alizotoa lazima atulie mwenyewe
Kwahiyo mahari inatumiwa kama black mail hapo mtauana sana maana upendo ukiisha huwa hakuna mbadala zaidi ya watu kuachana
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom