Tunaishi kwa upendo sisi ni jamii mmoja, ki-historia waislam ndo wanachinja miaka yote, na hata kijijini kwetu ikiwa kuna sherehe kwa mkiristo anaitwa muislam achinje ili sisi ambao tunaamini mkiristo hawezi kuchinja tule nyama hiyo..! Hatufanyi mashindano ya kuchinja au kitu cha aina hiyo na ndo maana mabucha ya kiti moto yapo kibao na tunayaheshimu..! Ni suala la kiimani kwamba nyama akichinja muislam mkiristo anao uwezo wa uila bila shida wakati muislam hali nyama aliyochinja mukristo. Hili siyo suala la jana wa juzi ni tokea enzi na enzi, labda uniambie kuwa mnataka mabadiliko sasa