Wakristo bucha hii hapa

Wakristo bucha hii hapa

hakyamungu! Julius Nyerere akirudi atakataa sikuwahi kukaa nchi hii!
 
Hii ndiyo sawa. Kila mtu ale nyama iliyochinjwa kwa ibada yake. Safi kabisa hapa hakuna vita.
 
529706_343894205716285_672154241_n.jpg

“Tumefika hapa kwa sababu ya udhaifu wa Rais Jakaya Kikwete, kwa uzembe wa Bunge na kwa sababu ya upuuzi wa CCM.” tafakari kisha chukua hatua

tafakari wewe kwanza kabla ya kiandika upuuzi wako huu,uliloandika apa linajenga nini,ww umechukia hatua gani sa kuweza kisaidia hayo yasitokee?
 
Jamani ndg zangu, itakuwa ni kichekesho na sisi Watz tutaonekana ni taifa la kipuuzi kuwahi kutokea duniani kama ishu ya kuondoa uhai wa mnyama kwa ajili ya kitoweo itufanye tufikie hali ya wale ndugu zetu wa Nigeria ambaye hali ya kiusalama si shwari kwa sababu tu ya udini.
Nafikiri we have so many problems to deal with...,should we add this...?
Kwa ninavyofikiri, vurugu za dini ni miongoni mwa migogoro ambayo suluhu yake inachukua muda mrefu, pengine hiyo vurugu ikisambaa yaweza kuondoa maisha ya either mimi, wewe au ndugu zako/zangu wa karibu au wote. Tukiwaachia hao waliokuwa wanachinja Imani zetu zitayumba kwa kiwango gani... au pengine imani zetu zimekuwa zaidi baada ya kuanzishwa kwa mchakato wa katiba mpya?
Nawasilisha.
"Usichokoze nyuki kwa kutegemea mbio
"
 
Mimi ni muislam lakini waislam wenzangu hamuwawezi wakristo, kwanza wako wengi na wana elimu kuliko sisi, sisi tumekalia majungu, uchawi na kulilia upendeleo. Kuchinja tunapata faida gani??? au hizo elfu tanotano? kwa nini tusisome tufanye kazi tuwe tunazipata zaidi ya hizo? hii dini nitaondoka siku za karibuni kujiunga na ukristu. Rais wetu hawezi kuongea lolote kututetea anajua litakalotokea hiyo siku atakaposema chochote. pia anatuogopa waislam kuwa tumamwita kafiri kama akiponda, anajua fujo zetu. Sijawahi kuona rais asiye na maamuzi kama huyu ni kama bendera anasubiri afundishwe nini cha kusema. Im out:majani7:
 
Kikrstu hakuna kitu inayoitwa kunyonga.... Hivyo basi usiingize imani ya kiislamu kwa wakristu
Tunaishi kwa upendo sisi ni jamii mmoja, ki-historia waislam ndo wanachinja miaka yote, na hata kijijini kwetu ikiwa kuna sherehe kwa mkiristo anaitwa muislam achinje ili sisi ambao tunaamini mkiristo hawezi kuchinja tule nyama hiyo..! Hatufanyi mashindano ya kuchinja au kitu cha aina hiyo na ndo maana mabucha ya kiti moto yapo kibao na tunayaheshimu..! Ni suala la kiimani kwamba nyama akichinja muislam mkiristo anao uwezo wa uila bila shida wakati muislam hali nyama aliyochinja mukristo. Hili siyo suala la jana wa juzi ni tokea enzi na enzi, labda uniambie kuwa mnataka mabadiliko sasa
 
Unajuwa walifanya nini kwenye bucha za nguruwe huku dar?
 
Ndugu zangu,vijana wenzangu naomba hili la dini tusilishabikie sana coz mwisho wake sio mzuri,bora ya ukabila unaweza ukakosa rafiki wa kabila fulani lakini nani hana jamaa au rafiki wa dini tofauti na yake....ebu tafakari hili kuna kina Peter Omar,John Mohamed,Mwajuma Rafael na wengine tuliochanganyika mtatuweka kundi gani?Stop this please.
 
bora kuwepo HALAL waislam na hiyo UNHALAL wakristo butcher

Nijuavyo mimi huwa kuna halal meat for muslims and Good Meat for christians:

Ukiita Unhalal,nyamafu,kunyonga au jina lolote lile, sisi halitutishi.Kitu muhimu ni kuchinja sisi wenyewe kuliko kula nyama iliyochinjwa kwa dua za ajabuajabu!
 
Hii ndiyo sawa. Kila mtu ale nyama iliyochinjwa kwa ibada yake. Safi kabisa hapa hakuna vita.
Ndio maana mimi nyama nayokula ni Kitimoto tu nikiwa mjini, uku nakoishi yangekuwepo mabucha ya Kikristo ningekuwa nabadilisha nyama mara kwa mara. Nikikosa Kitimoto uwa nakula samaki.
 
Ndugu zangu,vijana wenzangu naomba hili la dini tusilishabikie sana coz mwisho wake sio mzuri,bora ya ukabila unaweza ukakosa rafiki wa kabila fulani lakini nani hana jamaa au rafiki wa dini tofauti na yake....ebu tafakari hili kuna kina Peter Omar,John Mohamed,Mwajuma Rafael na wengine tuliochanganyika mtatuweka kundi gani?Stop this please.
Sisi hatuna ugomvi na mtu,tunachotaka ni kuchinja wanyama wetu wenyewe!Kama kuchinja ni vurugu,basi na iwe hivyo!
 
Bila shaka na kiti moto safi haikosekani hapo
 
Hii c dalili nzuri hata kidogo.. Tumeanza na mabucha.. Nini kitakachofuata baadae..? Maana tunashabikia lakini hebu tuangalie huko mbele kwa mwendo huu.. Ninawafikiria wanangu wanaokuwa katika mkanganyiko huu.. Ninawatengenezea mazingira gani ya kuishi kama Watanzania..? Naogopa sana.. Serious..
Mkuu sosoliso, nakusihi wala usipeleke mawazo yako mbali. Lione hili kama jambo la kawaida tu. Kwenye baadhi ya nchi kuna maduka ya vyakula ambamo wanauza nyama halal na wanaandika na kunadi hivyo. Wala halionekani jambo la ajabu. Na hili tukilichukulia kama ni jambo la kawaida tu, wala hatutafika kule watu wanakohofia.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom