Wako wapi watu wako mliosoma wote

Wako wapi watu wako mliosoma wote

Ndoa ni chanzo cha hayo mengine yote, laiti ningalirudi Nina miaka 30 nisingeoa Kabisa, na ningekuwa mbali sana, mtu yeyote anayepanga maisha chini ya umri wa miaka 50 au 45, akiwa na mwanamke ajue mambo yanaweza kubadilika mda wowote na akarudi sifuri.
Pamoja na yote tusi regret.. Ni hatima ambato
😁 Brother mshana tumia I'd yako inginee utusimulie..

Just joke

NB. Ulicho KIELEZEA ni UKWELI wa wazi na TUPU.
Sina zaidi ya hii ningeshafanya hivyo😁😀
 
Nafikiri nipo connected jamii forums kuliko na ndugu au marafiki, Kuna wakati maisha yanakutaka uwe peke yako
 
Marafiki wema wapo aisee
Nikiwa primary mwaka 2005 nilikuwa na mshikaji wangu wa utotoni, alikuwa mshikaji wangu sana

Nikiwa O level pale katoke seminary nilikuwa na wanangu wawili tulikuwa wahuni ila Sasa ni mapdre basi tukikutana Huwa tunakumbuka na kufurahia

Chuoni pale SAUT nilimpata jamaa angu ambaye hadi Sasa ni jamaa angu Huwa tunasaidiana sana, jamaa angu ana roho nyeupe
 
stori yako inafanana na yangu kdg, mshkaji kutokana na kumpa gheto kila akitaka kula mbususu akanambia baada ya six twende j.k.t uhakika wa maisha ni 100% nikaleta ujuaji

jamaa akaenda sasa hivi ana nyota 2 JWTZ mie hapa hadi leo naunga unga mishe mishe
Mtafute akupe mtaji
 
Best friend wa shule ya msingi alifariki tukiwa hatujamaliza

O level tulikuwa kundi watu watano tunasumbua sana... kama siku ikitokea kuna mechi kila mmoja atakuja na kilevi anachotakiwa kuleta (tulipeana vitengo, mimi nilikua in charge kuleta weed), kulikua na wa ugoro, pombe kali, wa ulanzi n.k
a) Mmoja alifariki tukiwa form 4
b) mwingine ni ile aina ya watu wanasemwa, "yule alikua zamani"
c) Mmoja anapiga debe stendi
d) Huyu mwingine taarifa zake sina

Advance na chuo sikuwa na marafiki ambao nilivuka nao hizo hatua. Nje ya mada, hivi ni kweli kwamba marafiki wengi wa ukweli tunawapata O level?
KWELI AISEE
 
Girl friend wangu wa o level nimezaa nae na sasa kila mtu ana familia yake. Tulipendana sana na mpaka kesho tunapendana ila suala la ndoa ilishindikana. Kasepa na mtoto wangu wa kiume.
 
Nilisoma na Juma ikifika brake time anaenda kuvizia watu walionunua mihogo yao anawapora kwa kupita mbio kama kishada mfano wa mwewe anavyopita na kifaranga.

Sahivi amekua expert anajua magereza yote yana Selo ngapi na kaweka chata zake kwenye ukuta wa selo za magereza na vituo vya polisi, sijaonana nae kitambo nadhani yuko gerezani kapumzishwa
 
Best friend wa shule ya msingi alifariki tukiwa hatujamaliza

O level tulikuwa kundi watu watano tunasumbua sana... kama siku ikitokea kuna mechi kila mmoja atakuja na kilevi anachotakiwa kuleta (tulipeana vitengo, mimi nilikua in charge kuleta weed), kulikua na wa ugoro, pombe kali, wa ulanzi n.k
a) Mmoja alifariki tukiwa form 4
b) mwingine ni ile aina ya watu wanasemwa, "yule alikua zamani"
c) Mmoja anapiga debe stendi
d) Huyu mwingine taarifa zake sina

Advance na chuo sikuwa na marafiki ambao nilivuka nao hizo hatua. Nje ya mada, hivi ni kweli kwamba marafiki wengi wa ukweli tunawapata O level?
O level na primary. Hawa mara nyingi asili zenu zinafanana, eneo, Kabila, Mila dini, wazazi na kuoleana.
Ingawa kuna washkaji wa chuo wapo wazuri lakini hawawezi kuzidi wawili na mmoja snitch.
 
Back
Top Bottom