Hii imenikumbusha A-Level, si mnajua tena yale mambo ya kuchaguliwa vipaji maalum haya twende kazi;
Kuna jamaa tumuite Mr. B tulikutana mkondo mmoja PCM ila sikuwahi kuwa na urafiki nae wa karibu ni ile tu Hi, au kwenye group discussion walimu walizotipanga.
Kimbebe kilitokea siku ya NECTA form 6 kwenye practical ya Physics, nakumbuka ilikua ni practical ya Simple Harmonic Motion (Mliopiga Physics Mtakua mnaelewa hapa ninachokisema). Ile pendulum Bob niliyokua nimepewa ili jam na mie kichwa kika'jam, aisee hamna siku nilidata kwenye pepa kama ile.
Sasa huyo Mr. B alikua pembeni yangu kumcheki yeye anatembea tu na data kashamaliza ku'record, uzalendo ukanishinda, pimia huku na kule msimamizi haoni nikaipeleka sheet yangu kwake nikasema potelea mbali, Mr. B hakuwa na hiana akaweka data japo na yeye kidogo apanic, baadae kanionesha ishara kwamba nitulie, baada kama ya dk 10 akanipa ile sheet nikaanza tena kushusha vitu hadi mwisho.
Matokeo kutoka Mr. B ana I.6 huku Physics kabamiza A, na mie II.10 huku Physics nikilamba D. Na huo ndio ukawa mwisho wa mahusiano yangu na Physics na Mwanzo Mpya wa urafiki kati yangu na Mr. B hadi hivi leo.
Mr. B kwa sasa ni Engineer Mkubwa katika Sector ya Oil & Gas.