Wakili Albert Msando akatwa katwa mapanga Dar

Wakili Albert Msando akatwa katwa mapanga Dar

You have learned things the hard way!
Pole sana Albert!
 
Nampa pole ndugu Albert, huu ni dhahiri ujambazi wa aina mpya kabisa. Tumepata fundisho, mtu akijaribu kukusimamisha na kavaa vizuri , usikubali mwambie tuongozane mpaka kituo cha polisi karibu na hapo. Na mwambie chukua nbr ya gari kama anafikiri utakimbia.

Kwa wale wapendao kuzusha mambo na kuwachonganisha watanzania haya fursa hiyo, njooni muitumie kujenga hoja zenu za kinafiki
Wewe ndio mchanganishi, mnafiki mkubwa. Hadi hapa hakuna aliye-comment uchochezi wala uchonganishi ila wewe ndio unaanzisha
 
Pole wakili msomi. Nilikuwa naendesha gari wiki ilopita, nikafika kwenye cross roads, ikanibidi kusimama. Nilipoondoka nikasikia kama mlango wa pili nyuma umeburuta kitu au nimekanyaga kitu kwa tairi ya nyuma. Kucheck kwenye side mirror nikamuona mtu mzima anazunguka kama kuku aliyekatwa kichwa huku ameushika mguu wake mmoja. Mimi nikaendelea na safari yangu taratiibu at 20kph. Kufika mbele kama mita 500 kuna tuta nilipopunguza mwendo tu nikaona pikipiki inataka kunipita na kuweka ishara ya kuchomekea. Imepakia watu 2 mmoja mjahidina kwa kilemba na kanzu yake. Wakaniashiria kuwa nisimame. Sikuwapa nafasi nikaendelea. Wakanifuata tena, nikashusha kioo nikamwambia boda huutaki uhai?? Endelea nikuoneshe matumbo yako.
Mbele kukawa na cross roads nyingine, ikabidi nisimame ila this time kukawa na gari mbili mbele na moja nyuma. Bodaboda akasimama, mwenzie kashuka akanifuata. Nilikuwa nimesha lock milango yote na madirisha nimepandisha. Nikaanza kumpima jinsi nitakavyo swing gari nimmalize mmoja wao nadhani jamaa aliisoma namba usoni mwangu kwani walipotea kiaina. Jamani, msimu huu wa sikukuu, tujihadhari
 
Mungu Ampe wepesi wa kupona Ndugu Msando. Wanadamu kwa sasa utu umepotea kabisa.

Ni Afadhali ukutane na Mbwa usiku kuliko ukutane na Mwanadamu mwenzako.
 
0b258c8f1ba3c0c8c2701acb17f49612.jpg

Haya ndio aliyoandika baada ya tukio!

Ndugu zangu, nawashukuruni wote mliojaribu kunitafuta na kunipa pole toka jana. Sikuwa napatikana kwa sababu walionivamia waliiba simu pamoja na vitu vingine.

Kilichotokea: Usiku wa saa tano siku ya Alhamisi (juzi) nilisimamishwa na gari baada kupigiwa honi na kuwashiwa taa na gari iliyokuwa nyuma yangu. Niliposhusha kioo driver akawa anaongea haraka haraka kwamba nimewagonga wakati narudi nyuma parking na nakimbia. Nikamjibu kwamba sijamgonga.

Akaniambia umetugonga angalia bampa. Kweli bampa lilikuwa limelegea. Ila sikuwa nimewagonga hivyo nikaendelea kubisha. Akaniambia shuka uangalie hata pembeni. Alikuwa amevaa smart tu so nikashuka. Wakati naangalia anaposema nimemgonga wakashuka wengine wawili kutoka kwenye gari na kunishika. Wakaanza kunishambulia huku wakinipora wallet, saa nk. Then wakanikata panga kichwani na kupekua gari wakaondoka na laptop na simu pamoja na funguo wa gari.

Kwa sasa naendelea vizuri baada ya kupata matibabu. Nawashukuru wote.

Albert Msando
Umafia Upo tanzania
 
Duh ila hiyo mbinu ya kuiba ni kali, kwa waungwana kama mimi lazima nisimame ili tuyamalize kumbe tena ni hatari. Basi mimi kuanzia sasa sishushi hata vioo, ubaya ubaya tu
Tunakuchomea humo humo kwenye gari lako!!
 
Nyie mnaofanya quote ndefu mnakera cna.
 
0b258c8f1ba3c0c8c2701acb17f49612.jpg

Haya ndio aliyoandika baada ya tukio!

Ndugu zangu, nawashukuruni wote mliojaribu kunitafuta na kunipa pole toka jana. Sikuwa napatikana kwa sababu walionivamia waliiba simu pamoja na vitu vingine.

Kilichotokea: Usiku wa saa tano siku ya Alhamisi (juzi) nilisimamishwa na gari baada kupigiwa honi na kuwashiwa taa na gari iliyokuwa nyuma yangu. Niliposhusha kioo driver akawa anaongea haraka haraka kwamba nimewagonga wakati narudi nyuma parking na nakimbia. Nikamjibu kwamba sijamgonga.

Akaniambia umetugonga angalia bampa. Kweli bampa lilikuwa limelegea. Ila sikuwa nimewagonga hivyo nikaendelea kubisha. Akaniambia shuka uangalie hata pembeni. Alikuwa amevaa smart tu so nikashuka. Wakati naangalia anaposema nimemgonga wakashuka wengine wawili kutoka kwenye gari na kunishika. Wakaanza kunishambulia huku wakinipora wallet, saa nk. Then wakanikata panga kichwani na kupekua gari wakaondoka na laptop na simu pamoja na funguo wa gari.

Kwa sasa naendelea vizuri baada ya kupata matibabu. Nawashukuru wote.

Albert Msando
Dar si salama usije ukapigiwa honi au ikatokea bodaboda zikakufukuzia kwa madai umesababisha ajali usije ukathubusu ukasimama au ukashuka kwenye gari jitahidi kuendelea na safari mpaka ufike kituo cha polisi kilicho karibu
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom